Waliokuwa 10 bora Tanzania (PCB) nane kati yao wamenyimwa mkopo

Tumia akili siku ingine, serikali haina hasara iko radhi imtoe daktari popote ulaya na imlipe kila kituu kuliko kufanya long term plan
 
Christeve88 kumbuka tunazungumzia mkopo si ruzuku,huo ni mkopo ambao utalipwa,hivyo hujaambiwa umkopeshe wa ada ml5 dv 1 na umuache wa ada laki 1 dv2,hoja hapa ni kila mwanafunzi anahitaji mkopo
Ni kweli boss ni haki ya kila mwanafunzi aliyefaulu kupata mkopo, shida inakuja kwenye sifa za kupata mkopo, ukianzia sifa ya kwanza mpaka ya mwisho na ukizingatia na bajeti ni lazima wamchukue yule masikini maana ukimuacha ndo kumuangamiza kabisa maana hatoweza kumudu ada.

Ni bora huyo mwingine angalau anaweza thubutu kujilipia maana yeye keshazoea hayo maisha yakulipa maada makubwa makubwa.
 
Mie nasikitika tu kuwa bado wapo bongo, nilitegemea top 10 wawe nje kwa maarifa zaidi.
 
Acha ujinga wewe, usome feza boys/girls halafu ufaulu vizuri ndio iwe tiketi ya kuwanyima watoto wa masikini mkopo upewe wewe unaeweza kulipa ada milioni 40 kwa mwaka? Uwe na aibu kidogo aisee..
 
Tumia akili kufikiria mkuu..huo ni mkopo kwa wale wasioweza kujisomesha chuo na sio fadhila kwa waliofaulu
Na kama ni MKOPO kwa nini umnyime mkopaji? Kwa nini uangalie shule aliyotoka wakati yeye anahitaji mkopo na atafanya kazi au biashara au kilimo alipe huo mkopo? Kama kufaulu ni janga basi waliopata division ziro nao serikali iwakopeshe kiasi cha hela cha kufanyia mradi wowote watakao.
 
Tumia akili kufikiria mkuu..huo ni mkopo kwa wale wasioweza kujisomesha chuo na sio fadhila kwa waliofaulu
Ni kichekesho sana

Kuona MTU kasoma shule ya sekondari ada 6mil

Afu analia lia na SERIKALI akopeshwe ada ya 1mil Chuo Kikuu

VITU VINGINE MNATAKA TU KUMCHOSHA RAISI WETU MPENDWA.
 
Ni full vinyongo,kukomoana na roho mbaya! Kodi tulipe wote ila waifaidi wachache kwa matakwa ya watu fulani tu....

Halafu tunataka kwenda tanzania ya viwanda na uchumi wa kati..Kama hatuwezi kuthamini watu kama hawa sijui tunataka nini.. But CCM hazina yao ni mabumbumbu na vilaza wala tusishangae. Mwalimu Nyerere angeamua kufanya kama wanavyofanya wao sijui wangekua wapi tena wengien Maprofesa wamesoma kwa fedha zetu bure kabisa.

Nchi za wenzetu watu kama hawa wala hawakopeshwi ila wanasomeshwa bure tena scholarship za serikali au Chuo moja kwa moja! Tuendelee kudhulumu watu korosho zao tu ndicho tunachoweza.
Mtoa mada, Hebu acha Ujinga bana.

Serikali yetu haina bajeti hizo za kuchezea kama unazowaza wewe.

Kuna vitu Vingi vya kushughurikia kwenye nchi yetu zaid ya kusomesha hao unaowaita ma-geneous

Kwa sasa,
Tunaumiza kichwa kuhusu afya, elimu bure, fly over, dreamliner, Sgr, stiglers n.k

Hao ma-geneous wako inabd wasubiri labda kwenye AWAMU zinazofuata.

Awamu hii ya 5 ni special kwa ajili ya wanyonge wa nchi hii kama mamantilie,machinga na wakulima wa korosho.

Hebu Kua serious buana.

tapatalk_1544299120592.jpeg
 
Back
Top Bottom