Waliokuwa 10 bora Tanzania (PCB) nane kati yao wamenyimwa mkopo

Mubby777

JF-Expert Member
Oct 17, 2018
1,639
5,638
Sometime inachekesha mnaweza sema kwa sababu wamesoma shule za gharama
Ooh wazazi wao wana pesa wawalilie na chuo
But turud katika ukweli “ hawa ni watu wenye uwezo mkubwa na vipaji vikubwa sana ingetakiwa serikali iinvest kwao, iwatafutie vyuo bora na kuwasomesha ili kutoa madaktari bora kabisa wa kuja kulisaidia taifa”
Inashangaza kuona nane kati yao wamekosa mkopo na wawili ndo wamepata ufadhiri kutoka taasisi binafsi

Sawa wamesoma shule za gharama but hawa ni watu muhim sana wenye uwezo mkubwa wa kulisaidia Taifa mbeleni
 
Waliosoma private hawatakiwi kupewa mkopo.

Ufaulu wake utafaidisha familia yake
 
Sometime inachekesha mnaweza sema kwa sababu wamesoma shule za gharama
Ooh wazazi wao wana pesa wawalilie na chuo
But turud katika ukweli “ hawa ni watu wenye uwezo mkubwa na vipaji vikubwa sana ingetakiwa serikali iinvest kwao, iwatafutie vyuo bora na kuwasomesha ili kutoa madaktari bora kabisa wa kuja kulisaidia taifa”
Inashangaza kuona nane kati yao wamekosa mkopo na wawili ndo wamepata ufadhiri kutoka taasisi binafsi

Sawa wamesoma shule za gharama but hawa ni watu muhim sana wenye uwezo mkubwa wa kulisaidia Taifa mbeleni
Hamna kitu kama hicho...kwanza nimegundua watu valuable katika jamii ni watu wenye ufaulu wa kati..div 2 ad 3....hao div one kwenye utendaji kazi ni mapunga kabisa, ukiangalia hata serikalini wasomi hao ndo mapoyoyo wakubwa tena from UD, kwenye kung'amua mambo ni poor...yaan ni one way thinking..hata shuleni huwez kuta wanapewa hata ukiranja....!!!.wapambane na hali zao
 
Ni full vinyongo,kukomoana na roho mbaya! Kodi tulipe wote ila waifaidi wachache kwa matakwa ya watu fulani tu....

Halafu tunataka kwenda tanzania ya viwanda na uchumi wa kati..Kama hatuwezi kuthamini watu kama hawa sijui tunataka nini.. But CCM hazina yao ni mabumbumbu na vilaza wala tusishangae. Mwalimu Nyerere angeamua kufanya kama wanavyofanya wao sijui wangekua wapi tena wengien Maprofesa wamesoma kwa fedha zetu bure kabisa.

Nchi za wenzetu watu kama hawa wala hawakopeshwi ila wanasomeshwa bure tena scholarship za serikali au Chuo moja kwa moja! Tuendelee kudhulumu watu korosho zao tu ndicho tunachoweza.
 
Hamna kitu kama hicho...kwanza nimegundua watu valuable katika jamii ni watu wenye ufaulu wa kati..div 2 ad 3....hao div one kwenye utendaji kazi ni mapunga kabisa...yaan ni one way thinking..hata shuleni huwez kuta wanapewa hata ukiranja....!!!.wapambane na hali zao
HIzi ndio thinking za kimaskini na kipuuzi kabisa, Na tutaendelea kubaki hapa hapa wallahi.. kwa hiyo ulitaka wote wapate Div 2 and 3?
 
Hv nini maana ya mkopo unaanzaje kumkopesha mtu aliyesoma shule ya ada milion tano kwa mwaka akapat division one halafu umuache yule aliyesona shule ada laki moja akapt division two. Embu acheni kulaum kila kitu.
Christeve88 kumbuka tunazungumzia mkopo si ruzuku,huo ni mkopo ambao utalipwa,hivyo hujaambiwa umkopeshe wa ada ml5 dv 1 na umuache wa ada laki 1 dv2,hoja hapa ni kila mwanafunzi anahitaji mkopo
 
Tatizo una hasira sana na inaonekana unatumia makalio kufikri....mkopo ninkwa ajili ya kusaidia wasiojiweza na sio reward kwa aliyefaulu.....alaf hii ni Tanzania na sio nchi za wenzetu
Asante
 
Kipaji ninini? Tuanzie na hapo kwanza.... Mtoto anasoma kwenye mazingira rafiki, anawezeshwa kwa kila hitaji halafu mnasema vipaji maalumu. Ungeandika tu hoja ya kwamba wasaidiwe ingetosha. Mtoto aliyesoma 'sitimbi' pcb, akapata divisheni 2,au 3. Bila mwalimu, na mazingira mengine wezeshi huyu unaweza kum-tegorise , kwenye vipaji. Na huyu ndiye anayehitaji more assistance.
 
Sometime inachekesha mnaweza sema kwa sababu wamesoma shule za gharama
Ooh wazazi wao wana pesa wawalilie na chuo
But turud katika ukweli “ hawa ni watu wenye uwezo mkubwa na vipaji vikubwa sana ingetakiwa serikali iinvest kwao, iwatafutie vyuo bora na kuwasomesha ili kutoa madaktari bora kabisa wa kuja kulisaidia taifa”
Inashangaza kuona nane kati yao wamekosa mkopo na wawili ndo wamepata ufadhiri kutoka taasisi binafsi

Sawa wamesoma shule za gharama but hawa ni watu muhim sana wenye uwezo mkubwa wa kulisaidia Taifa mbeleni
Kweli kuna ambao wamesoma private za gharama na wanaweza mudu cost za chuo but bodi itazame, si kila aliyesoma private anaweza kujilipia chuo. Private nyingine tukijikongoja zinalipika.

Mf. Mimi namsomesha dogo private. Ada na michango yao ni 1.8M kwa mwaka. Ni wastani wa 150K kwa mwezi. Hii napambana nalipa. Sasa nawaza, chuo akinyimwa mkopo, Ada ya udaktari smtms inafika 8-10M. Bado chakula&malazi. Ntaweza?

Ni hiyo shule ya 1.8M ndio ina determine kuwa naweza gharamia zaidi ya 12M kwa mwaka tena kwa miaka mitano?
 
Sometime inachekesha mnaweza sema kwa sababu wamesoma shule za gharama
Ooh wazazi wao wana pesa wawalilie na chuo
But turud katika ukweli “ hawa ni watu wenye uwezo mkubwa na vipaji vikubwa sana ingetakiwa serikali iinvest kwao, iwatafutie vyuo bora na kuwasomesha ili kutoa madaktari bora kabisa wa kuja kulisaidia taifa”
Inashangaza kuona nane kati yao wamekosa mkopo na wawili ndo wamepata ufadhiri kutoka taasisi binafsi

Sawa wamesoma shule za gharama but hawa ni watu muhim sana wenye uwezo mkubwa wa kulisaidia Taifa mbeleni

Kufaulu mitihani ya nadharia wakati mtoto anasoma private school ambapo anapata kila kitu(sometimes hata maji ya moto ya kuogea na dobi wa kumfulia uniforms zake) hakumfanyi mwanafunzi kuwa na kipaji kikubwa unavyofikiria wewe..... vipaji vikubwa wanavyo wale wanafunzi waliosoma kwenye mazingira magumu na wameweza kuyageuza yale mazingira "magumu"kuwa "fursa "ya wao kufaulu vizuri na hakika wanafunzi wa aina hii hufika mbali sana.
Lengo la ELIMU ni kumkomboa mwanafunzi aweze kuitumia ELIMU anayopata kukabiliana na mazingira yake....sio kuandaa kizazi cha MATAJIRI kupata AJIRA.
 
Hili swala la mikopo kwa kweli bado ni changamoto nafakiri kuna haja serikali kufanya review katika hili vigezo na masharti havicorrespond na mwishowe unabaki kusema walionacho wataongezewa mtoto anatoka O level Mazinde Juu High school Marian/Feza chuo Muhas mkopo 100% baba ni mdau flani katika wizara na huyu mwengine amesoma keko magurumbasi high school Azania chuo UD anakula sifuri nadhani pia kuna haja ya hizi coz ambazo hazina mikopo mwisho wa masomo watu kupewa grant ya kuwekeza katika mawazo yao either kwa mtu mmoja mmoja au kwa kikundi cha watu walau watano watano sio wanarundikana huku mtaani
 
Hamna kitu kama hicho...kwanza nimegundua watu valuable katika jamii ni watu wenye ufaulu wa kati..div 2 ad 3....hao div one kwenye utendaji kazi ni mapunga kabisa, ukiangalia hata serikalini wasomi hao ndo mapoyoyo wakubwa tena from UD, kwenye kung'amua mambo ni poor...yaan ni one way thinking..hata shuleni huwez kuta wanapewa hata ukiranja....!!!.wapambane na hali zao
Ficha chuki yako dhidi ya udsm, kama uliomba wakakutosa vumilia ndio maisha, kuna kupata na kukosa!
 
11 Reactions
Reply
Back
Top Bottom