Wafikishwa Mahakamani kwa kudukua Mfumo wa Kompyuta wa CRDB

BARD AI

JF-Expert Member
Jul 24, 2018
3,376
8,120
Watu wawili wamefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu wakikabiliwa na mashtaka manne likiwemo la kuingilia mfumo wa kompyuta wa benki ya CRDB na kujipatia kiasi cha Sh Milioni 13.8.

Washtakiwa hao ni Riziki Kanena (22) ambaye ni mkazi wa Mikocheni na Laulentina Yastaf Mkazi wa Akamea Karagwe mkoani Kagera.

Wakili wa Serikali,Titus Aron akiwasomea mashtaka hayo amedai kati ya Januari 3, 2023 na Juni 3, 2023 mshtakiwa Riziki akiwa Mikocheni wilaya ya Kinondoni kwa nia ovu aliingilia mfumo wa kompyuta wa benki ya CRDB kisha kujipatia kiasi cha Sh.Milioni 13.8.

Imedaiwa kuwa tarehe hizo mshtakiwa Riziki alitumia laini ya simu iliyosajiliwa kwa jina la Yusuph Mboko kisha aliiba kiasi hicho kwa kutumia laini ya simu ya Mboko bila kutoa taarifa kwa umiliki wa mtandao.

Pia katika shtaka la nne linalomkabili Laulentina , inadaiwa tarehe hiyo akiwa eneo la Akamea Karagwe mtaa wa Mlamba vijijini mkoani Kagera alipokea Sh. Milioni 5.4 wakati akijua ni mali ya wizi.

Aron amedai upelelezi wa shauri hilo haujakamilika hivyo aliomba mahakama hiyo ipange tarehe nyingine.

Baada ya kusomewa mashtaka hayo Hakimu Mkazi Mkuu, Pamela Mazengo amesema washtakiwa hao hawaruhusiwi kujibu chochote kwa sababu mahakama hiyo haina mamlaka ya kusikiliza kesi ya uhujumu uchumi.

Hakimu Pamela, ameahirisha kesi hiyo hadi Agosti 14,2023 kwa ajili ya kutajwa na washtakiwa hao wamerudishwa rumande.

BONGO 5
 
Wameiba hela chache sana
 
Wanatakiwa wapewe pongezi maana kama mtu wa ndani mtanzania ameona udhaifu kwenye mfumo wao ina maana amewaokoa wasiibiwe fedha nyingi zaid na mtu wa nje si kila kosa la kumuukumu mtu mengine ni funzo watu wajifunze na vitengo wa one umuhimu wa hao vijana
 
Sidhani kama ni udukuzi, nilichoelewa Mimi huyo jamaa mmoja aliiba password za SIM Bank ya muhusika mwenye laini ya simu then akahamisha pesa na kuzituma kwa huyo ndugu yake alieko Karagwe, ni sawa tu na mtu anaejua password za ATM card yako aiibe na kwenda kutoa pesa bila wewe kujua
 
Kama ni hivo wapo sahihi sheria ifate mkondo wake
 
Back
Top Bottom