Superbug
JF-Expert Member
- Jan 31, 2018
- 12,417
- 30,929
Ni jambo la kusikitika sana, ukitafakari siasa za Tanzania. Kitendo cha wanasiasa walioaminika na wananchi kwa kupigiwa kura kuhamia CCM kwasababu za kipumbavu kama wanazotoa ni jambo litakalohojiwa sana na vizazi vijavyo.
Nadiriki kusema miaka kumi ijayo hawa WALIOHAMIA CCM watakuwa wazee ila uzee wao utakuwa wa aibu fedheha na mashaka.
Kwanza vijana wa miaka kumi ijayo ambao kwasasa ni watoto under eighteen watajiuliza hivi kweli hawa watu walioaminika na wananchi katika capacities mbalimbali za KISIASA waliwezaje kuhama na kukimbilia CCM kwasababu za kuunga juhudi mkono, eti za Rais Magufuli!
Yani wenye akili wa miaka hiyo niliyotaja hapo juu watahoji huu upuuzi kwa kina sana. Na watashawishi wajukuu zao wasiaminiwe katika nafasi nyeti za serikali za awamu zitakazokuwa na akili kuliko hii serikali tulionayo sasa.
Hivi juhudi za kumuunga mkono Rais Magufuli ni zipi? Je, za kuua demokrasia yetu iliyoanza kushamiri aliyotuachia JK?
Au je, juhudi za kuteka watu kupoteza watu kunyamazisha jamii kupiga wanasiasa risasi kuwa na upendeleo usiomithilika au ni juhudi zipi hizo?
Serikali za awamu zote zilifanya makubwa kwa wakati wake ila haikuwahi kutokea ujinga kama huu wa awamu ya tano eti usaliti kura za wananchi maelfu waliokuchagua kisa kuunga juhudi mkono zipi?
Kuna kila sababu ya TAKUKURU ya miaka ijayo kuchunguza huu upuuzi wa awamu hii miaka ijayo.
Kama Watanzania hatukuwahi katika wakati wowote ule katika uhai wa taifa letu kutamani viongozi wetu kupelekwa mahakama ya uhalifu kama wakati huu.
Kwa hakika na yakini mnara wa babeli utakapokubali kuanguka watatafutwa popote walipo wajibu haya wanayoyafanya leo.