Waliogushi barua za kujitolea wachukuliwe hatua

Waliogushi barua za kujitolea wachukuliwe hatua

Mkuu watanzania tumezoea ujanja ujanja na wizi. Tegemea kutukanwa sana humu lakini hoja yako ni ya msingi.

Kama wanadanganya ili waajiriwe hawatashindwa kudanganya kwenye wizi wa mitihani na kutuletea wahitimu bomu kwenye jamii.

Lakini pia serikali iondoe kigezo cha uzoefu kwenye hizi ajira zake. Hizi ni entry level position uzoefu wa nini? Hii ndio inapelekea watu wanaamua kudanganya.
Utaratibu wa enzi za JK urudishwe, hakukuwa na mambo kama haya.

Utaratibu mpya ndio unaoibua haya mambo.

Watu wakisikia wale waliowahi kujitolea ndio watapewa vipaumbele, lazima watafute uchochoro ili na wao wapate hizo nafasi.

Wa kulaumiwa hapa ni Mamlaka na wala sio hawa wanaoomba kazi.
 
Utaratibu wa enzi za JK urudishwe, hakukuwa na mambo kama haya.

Utaratibu mpya ndio unaoibua haya mambo.

Watu wakisikia wale waliowahi kujitolea ndio watapewa vipaumbele, lazima watafute uchochoro ili na wao wapate hizo nafasi.

Wa kulaumiwa hapa ni Mamlaka na wala sio hawa wanaoomba kazi.
Kwani kujitolea ni deal sana kuliko taaluma? Wacha wafoji ata wamejitolea adi Harvard university ni sawaaa
 
KARIBU Nchi yangu Tanzania. Nchi ambayo mwenye kazi yake na maisha yake ana mwonea wivu jirani yake ambaya hata huyu jirani hawajuani wala kuishi jirani ila chuki binafsi tu, Ndio nchi pekee mtu ana kuambia kuna amani na upendo lakini bado ana chongea wenzake ambao wana taja kujiinua wapate ajira, ndio nchi pekee kwa ajili mtu kapitia mateso kupata ajira ana taka wanao tafuta ajira wateseke kama yeye.
Conclusion TUPENDANE NDUGU ZANGU. Mafanikio ya mwenzako ni yako pia usichukie ukiona mwenzio ana pata. Hao waalimu kesho na kesho kutwa ndio hao wana kwenda pelekwa vijijini kwenye hali ngumu ili tu kuboresha elimu mashuleni leo wewe una umia nini?
 
Wakati unasoma uliambiwa baada ya masomo ukajitolee na siyo kusubiri ajira?

Viongozi wa serikali wanaposistiza vijana wajiajiri, kujitolea nako ni mojawapo ya kujiajiri?

Kwanza nawapongeza waliosaidia vijana kupata barua za kujitolea kwao hata kama hawakujitolea kweli. Hawa ndiyo wenye mioyo safi. Maana wanataka kuona kila mwenye sifa anaajiriwa.

Acha hizo.
 
Kujitolea ni ugonjwa mbaya sana.bora hata nkapige ngeta watu.serikali ndo inatakiwa ijitolee kwa raia wake na sio sisi
Ndugu Acha Roho Yatak Umimi,Huwaonei Huruma Wanavyoteseka Mtaani Bila Ajira?

Kamwe Usifurahie Anguko la Mwenzako.
 
Ila ww jamaa unaonekana una roho ya korosho narudia tena una roho ya karosho sasa kwanini nakwambia una roho ya korosho ni kwasababu

1.roho yako ni roho ambayo hupendi kuoana mtu akipiga hatua ktk maisha yake

2.roho yako ikiona mtu kafanikiwa moyo wako unaanza kuchukia na kumchukia mtu bila sababu

Watu wa aina hii ndio aina ya watu mkifika umri kuanzia miaka 60 ndo huwa mnalalamika mmetelekezwa na watoto wenu

Ndio huwa mnalalamika marafiki mliosoma nao wamewasahau
Mtoa mada ni miongoni mwao waliotuma maombi, bahati mbaya ana mashaka na CV yake. (Ndicho kilimpeleka startionary).

Anafikiria iweje waliogushi barua wana cv nzuri kuliko yeye na wanatishia kum overtake.

Kila mtu na fungu lake.

Hatuungi mkono kughushi barua, lakini ni lini na wapi alipiga kelele kwa serikali kutoa ajira ili kuepusha msongamano wa watu wasio na ajira mtaani.

Sawa hawakujitolea, lakini siyo wajinga kiasi cha kushindwa kujipambania.
 
Acha ukuda ndugu kama unatafuta ajira tafuta kivyako.
Tangazo linasema umewahi kujitolea ndiyo au hapana.
Ukisema hapana maombi yako hayawezi kukamilika 100% na yasipokamilika maombi yako hayatumwi TAMISEMI.
Pili katika application TAMISEMI ukisema NDIYO barua ya kujitolea inatakiwa ,haya nambie ni shughuli gani huwa inatoa barua ya kujitolea...
Mara nyingi kujitolea huwa ni mdomo labda kwa shule za sekondari hata hizi za shule ya msingi unajibiwa tu kienyeji.
Labda kada ya Afya ukitaka kujitolea itahitajika barua ya DMO.

Just imagine kipindi cha Kikwete watu waliajiriwa bila uzoefu.
Mwisho kwenye maombi ya kujitolea shule nyingi hazikupata access ya internet kutuma taarifa kwa wakati ni walimu wangapi walikuwa wanajitolea baadhi yao waliachwa na majina machache yalitumwa ,unataka ambao majina hayo pia yabaki.?
 
Acha wivu mkuuu.

Huna hela alafu wivu mwingi utakufa maskini bwege wewe.

Umepanic utadhani ajira hizo unatoa wewe😀😀😀😀😀😀😀😀😀😀
 
Katika mambo yatayo mchafua mama ni pamoja na hiki kigezo cha kujitolea!

Walimu wa kujitolea wangeangaliwa kwa namna nyingine kwa mfano kulipwa posho kila mwezi ila huku kwenye ajira watu waajiriwe kulingana na sifa zilizoainishwa kwenye tangazo! Kusema kipaumbele cha ajira ni walimu waliojitolea ni upumbavu mkubwa ambao hauvumiliki!

Mama Samia tunaomba uwaangalie hawa watendaji wako wa tamisemi huenda wana lengo la kukuhujumu maana ikitokea kigezo cha kujitolea kikatumika kwenye hizi ajira ndio utakuwa mwanzo wa anguko la serikali yako!

Mama ingilia kati!
 
Walimu wakuu wamepiga kweli hela rafiki yangu sijui serikali ilijipangaje ,Mimi nilijua imllitumia njia ya kupata taarifa zawanaojitolea kabla...sasa hapo patamu ngoja tusubiri motowake walimu wakuu waliodanganya
 
Kijitolea wanachomaanisha NI kwa shule za serikali Tu......na sio private,kwa maana ukiangalia mfumo kwa upande wa Kada za elimu, kwenye mfumo wameweka shule za serikali Tu,hakuna shule za private, lakini walimu wengi wapo shule za private wameajiliwa au wamejitolea.....so tamisemi wanamajina Yao yangu zamani,na waliogush barua imekula kwao
 
Mkuu kujitokeza sio upumbafu Bali ni njia nzuri ya kukufanya improve competency. Sio rahisi kuwa imara pindi unapoanza kazi Kama hukuwahi kujitolea. Mara nyingi new employees wanahitaji çlose supervision kuepuka kujaribu kazi. Lakini ukiwa umejitolea kwa muda wa kutosha, ukiajiliwa eneo Hilo una enjoy kazi.
Kwa maana hiyo mkuu..nin maana ya kwenda field. Kwa mm kujitolea n kupoteza muda
 
Kwahiyo wao kufoji ili wapate ajira ni sahihi?
Struggle for existence mkuu......Kwani kitaharibika kitu gani?, ingekua ni vyeti ingekua sio sahihi

Yani serikali imeshindwa kuwa na mfumo wa kuwatambua waliojitolea, hizi sasa ni dharau
 
Kama hukusema nao... then unachapa humu hizo ni dalili za awali kuwa Shogaa
 
Kabla ya tangazo la ajira kutoka tamisemi nadhani walikwisha omba orodha ya walimu waojitolea hivo kwa ambaye haku forge tangu hapo ana wakati mgumu.
 
Back
Top Bottom