Waliogushi barua za kujitolea wachukuliwe hatua

Ndugu Acha Roho Ya Umimi,Huwaonei Huruma Wanavyoteseka Mtaani Bila Ajira?

Kamwe Usifurahie Anguko la Mwenzako.
Sasa kama wanateseka ndio wafoji, huoni wanawaonea wengine ambao hawajafoji?
 
Juzi nilienda stationery kushughulikia mambo yangu, nikakuta vijana wengi wamejazana pale wanatuma maombi ya ajira za ualimu, kwenye maombi ya Kuna kipengele cha uzoefu kama umewahi fundisha shule yeyote, cha ajabu kila kijana aliyekuwa anaingia pale alikuwa na barua ya kuonesha kwamba alikuwa anajitolea shule fulani, na wale ambao walikuwa hawana wenzao walikuwa wanawaelekeza namna ya kuzipata.
Huu ni udanganyifu kwenye ajira, ni wakati sasa serikali kupitia wizara ya Tamisemi iwachukulie hatua wote waliogushi kwamba wanauzoefu na wamejitolea shule kadhaa na kama Kuna wakuu wa shule na walimu wakuu watakuwa wamehusika nao vile vile wachukuliwe hatua.
Kipengele cha uzoevu kina dhumuni gani kama sio uonevu. Mtu kamaliza chuo unataka uzoevu ataupata wapi. Wewe ndie ulipaswa umwajiri ndipo apate huo uzoevu. Kwa nini tunawatesa vijana wetu bila sababu za msingi??????
 
Watanzania bhana,tuna shida!Baadaye wakija wakijulikana wameghushi mnarudi mnasema walipwe haki zao kama wa vyeti feki!?Hatujui tunacho hitaji!Kama huna uzoefu alafu una ghushi,then hata kuuza mitihani huwezi kushindwa!Wanaosema wewe sijui masikini sijui mlozi sijui mchawi ni wale wanaopenda kughushi,wizi,utapeli,ujambazi na ushirikina.You a fuckin Right pal!
 
Huu upuuzi wa kujitolea inabidi upigwe marufuku, unawafanya waajiri kupenda mteremko sana na kuwalalia waajiriwa.

Hivi mfano tu umejitolea kufanya kazi bure kwenye taasisi X huku ukiwa na degree yako, hapo unampa kiburi muajiri kukulipa anavyotaka yeye (Kama umeweza kufanya bure basi hata akikulipa laki utafanya tu).

Ikiwezekana hili jambo lizungumzwe mpaka bungeni. Tuache kuchukulia poa upumbavu kama huu. Watu wanafanya field wakiwa vyuoni, kwanini wakajitolee tena?
 
Wakati unajitolea utakuwa unakula wapi ?

Na let's assume utakuwa unaishi kwa kuombaomba, haya utajitolea mpaka lini au hizo ajira kwa wanaojitolea inafahamika siku watakayopata.
Suala sio kujitolea bali kufoji kuwa umejitolea kudanganya ili upate ajira unakuwa unawaonea wengine ambao hawajajitolea na waliojitolea.
 
Huu upuuzi wa kujitolea inabidi upigwe marufuku, unawafanya waajiri kupenda mteremko sana na kuwalalia waajiriwa.

Hivi mfano tu umejitolea kufanya kazi bure kwenye taasisi X huku ukiwa na degree yako, hapo unampa kiburi muajiri kukulipa anavyotaka yeye (Kama umeweza kufanya bure basi hata akikulipa laki utafanya tu).

Ikiwezekana hili jambo lizungumzwe mpaka bungeni. Tuache kuchukulia poa upumbavu kama huu. Watu wanafanya field wakiwa vyuoni, kwanini wakajitolee tena?
Na sasa hivi makampuni yamebuni mbinu ya kufanyisha kazi watu bure kupitia kujitolea au internship.

Hayatoi ajira.

Yanakutumikisha kwa internship au kujitolea mkimalizana yanatafuna interns wengine.
 
Ndugu Acha Roho Ya Umimi,Huwaonei Huruma Wanavyoteseka Mtaani Bila Ajira?

Kamwe Usifurahie Anguko la Mwenzako.
Umimi wanao hao wanaodanganya ili wapate ajira wawaache wenzao mtaani.
 
Nyie ndio wale hampendi wengine wafanikiwe kwenye ukoo.

Mijitu ya hivi seems ndio wale hawataki hata watoto wao wafanikiwe ili waonekane ndio top top kwenye familia. Kwetu Rombo / Marangu Utaja tengwa hadi na Familia yako.

BADILIKA
Mafanikio sio lazima yafanikiwe kwa kudanganya na kufoji, unataka tetea ujinga na inaonesha ulivyo mjinga.
 
Suala sio kujitolea bali kufoji kuwa umejitolea kudanganya ili upate ajira unakuwa unawaonea wengine ambao hawajajitolea na waliojitolea.
Mfumo rasmi ni Internship. Huu mfumo wa kuajiri serikalini waliojitolea ni upuuzi kama upuuzi mwingine.

Hivyo mimi simlaumu mtu aliyetoa suluhisho la kipuuzi kwa maamuzi ya kipuuzi.
 
Juzi nilienda stationery kushughulikia mambo yangu, nikakuta vijana wengi wamejazana pale wanatuma maombi ya ajira za ualimu, kwenye maombi ya Kuna kipengele cha uzoefu kama umewahi fundisha shule yeyote, cha ajabu kila kijana aliyekuwa anaingia pale alikuwa na barua ya kuonesha kwamba alikuwa anajitolea shule fulani, na wale ambao walikuwa hawana wenzao walikuwa wanawaelekeza namna ya kuzipata.
Huu ni udanganyifu kwenye ajira, ni wakati sasa serikali kupitia wizara ya Tamisemi iwachukulie hatua wote waliogushi kwamba wanauzoefu na wamejitolea shule kadhaa na kama Kuna wakuu wa shule na walimu wakuu watakuwa wamehusika nao vile vile wachukuliwe hatua.
WALIMU nfdio zao ndio maana ni kada inayotumika na serikali kama "tishu".
 
Mafanikio sio lazima yafanikiwe kwa kudanganya na kufoji, unataka tetea ujinga na inaonesha ulivyo mjinga.

Peleka ujinga wako huko....we unajua hali mtaani ilivyo kula kulala wewe

Nina ndugu kwenye hyo fani nayaona maisha yao yalivyo....na mmoja nimepa capital afanye mengine.
 
Wewe mpumbavu sana, kwahiyo unataka apate ajira kwa kudanganya awaache wengine mtaani?
 
Wakati wapo mtaani uliwatetea kwa lipi?au ulishia kusema wajiajiri
 
Mfumo rasmi ni Internship. Huu mfumo wa kuajiri serikalini waliojitolea ni upuuzi kama upuuzi mwingine.

Hivyo mimi simlaumu mtu aliyetoa suluhisho la kipuuzi kwa maamuzi ya kipuuzi.
Wala sio upuuzi, fikria pale mtaani kuna shule ina upungufu wa walimu wa somo fulani kijana akaamua kuwa anawasaidia wale watoto kwa muda wake ni halali serikali iajiri mtu mwingine aje kuchukua nafasi yake.
 
Wakati anajitolea hapo atakuwa anaishi vipi ?

Serikali inaajiri mwisho miaka 45 sasa ukianza kuajiri kwa kigezo cha kujitolea badala ya kuajiri kulingana na uhitaji na watu waliohitimu miaka ya nyuma huoni utanyima haki za ajira kwa watu wengi?
 
Juzi nilienda stationery kushughulikia mambo yangu, nikakuta vijana wengi wamejazana pale wanatuma maombi ya ajira za ualimu, kwenye maombi ya Kuna kipengele cha uzoefu kama umewahi fundisha shule yeyote, cha ajabu kila kijana aliyekuwa anaingia pale alikuwa na barua ya kuonesha kwamba alikuwa anajitolea shule fulani, na wale ambao walikuwa hawana wenzao walikuwa wanawaelekeza namna ya kuzipata.
Huu ni udanganyifu kwenye ajira, ni wakati sasa serikali kupitia wizara ya Tamisemi iwachukulie hatua wote waliogushi kwamba wanauzoefu na wamejitolea shule kadhaa na kama Kuna wakuu wa shule na walimu wakuu watakuwa wamehusika nao vile vile wachukuliwe hatua.

We ulitakaje ? mbona mna roho mbaya ivyo ?
 
Back
Top Bottom