Mkirua
JF-Expert Member
- Sep 9, 2010
- 5,647
- 2,513
Panaponitatiza ni pale wanaposema kuna wanafunzi 2,500 ambao kwa kutumia viwango vipya ufaulu wao umeshuka ila wakaamua kuwapa matokeo yao yale yale ya zamani. Swali ni kuwa inawezekana vipi kwa viwango vya zamani (vya juu) wawe na ufaulu halafu kwa viwango vipya (vya chini) matokeo ya ufaulu wao yashuke?
Kwa kifupi kinachofanyika ni standardization....unachukua alama mathalan tano kwa wanafunzi waliopata alama za juu (e.g. 85) halafu unawapa waliopata alama za chini (e.g 25) so alama ya juu inasomeka 80 badala ya 85 na ya chini inakuwa 30 badala ya 25. Sasa kama A ni 81 basi aliyekuwa na 85 atakuwa na 80 ambayo ni B. Na kama D ni 30 basi aliyekuwa na 25 ambayo awali ilikuwa ni F atakuwa na 30 ambayo ni D.... Hiyo ndiyo maana ya standardization kwa lugha nyepesi kabisa. Hii inatakiwa kufanyika kabla ya matokeo kutangazwa. Sasa ukishatangaza kuwa Fulani bin Fulani alikuwa na A leo unamwambia ana B andaa polisi na wanajeshi wa kutosha kuzuia maandamano... huyu wa 25 atabaki akichekelea tu kwani ndicho alichokitaka. Ndiyo maana sipendi siasa kwani it seems that to remain successful in politics, you must fool your people.