Sio kama kweli ndugu yangu....ni kweli, baraza na wizara walifanya wao kimya kimya! Watu pekee ambao walihusihwa kwenye maamuzi hayo ni TCU peke yao ambao ONLY One member ndiye alikuwepo! Kwa jinsi inavyoonekana, member wa TCU alienda pale kama mdau asiye na siye, kwani wakati TCU member alikuwa mmoja, Baraza na Wizara waliwakilishwa na member si chini ya watatu kila upande! Ikumbukwe kwamba, member pekee wa TCU ambae alikuwepo ni huyu Profesa Mchome ambae Kamati yake ndiyo ilipendekeza matumizi ya viwango vya zamani. Hii inaonesha wazi kwamba, yeye pale hakuwa na "say" na inawezekana kabisa hakuona busara yake.
Aidha, kikao ambacho kiliamua matumizi ya new system kilifanyika December 10, 2012....maana yake ni kwamba, maamuzi yalifanyika wakati mitihani imeshafanyika huku wanafunzi wakiwa nyumbani wanafahamu old system! Sasa kitu kama hiki ni wapi duniani kinaweza kufanyika kama sio Tanzania peke yake!? KImsingi, walichopata sasa madogo ndiyo haki yao ingawaje watu wanabeza! Awali, walifanyiwa hujuma na Baraza kwa kushirikiana na wizara!