Elimu yetu ya Tanzania iko kwenye kipindi cha mpito ninaweza nikasema hivyo, manake siasa inaonekana inaingilia rasmi mabo ambayo ni ya msingi na yenye mstakabali wa kitaifa. Kizazi cha leo ndio maana hakina uelewa wa haraka hata madarasani. Haya mambo ya uchakachuaji wa elimu hata vyuo vikuu yapo sana ingawa hayajasondowa vidole tu. kuibuka kwa vyuo vingi vya elimu ya juu nchini ambavyo havina vigezo ni dalili tosha ya kutoa elimu isiyozingatia miiko ya taalumu, na cha kushangaza serikali kupitia TCU inaangalia tu!