Waliochochea vurugu washughulikiwe

Waliochochea vurugu washughulikiwe

Dola ilijua, ndiyo maana palikua na movement ya vyombo vya usalama,na wali-note raia nchi jirani wakiingia, ndiyo maana JF ilifungiwa, viongozi chadema walitiwa korokoroni,they knew,wakaandaa na strategy ya kukabili,mama akajiandikisha Dodoma
Sheikh gallow bird

Usiwe mtu wa kugeuza maneno kutoka katika muktadha wake au kuharibu hukumu ya haki.

Unapindisha uhalisia ndugu yangu? Hivi tumefikia hatua hii ya kutomuogopa Allah?
 
Kwa hiyo unahalalisha mauaji? Kwa nini msiwasikilize? Hiyo misingi unaiona ni ya haki?

Siku ya Qiyama ijapokuwa Allah ni mjuzi wa tunayoyafanya lakini bado atasikiliza waja wake kipi kilochokufanya ufanye hivi na hivi na hukumu yako uione mwenyewe.

Ibilisi laanatullahi alayhi alikataa kutii amri ya Allah, lakini Allah hakumuhukumu kabla bali alimsikiliza kwa kumuuliza kipi kilichokufanya kutotii amri yangu nilipokuamrisha. Baada ya majibu yake ndipo Allah alimuhukumu.

Misingi ya haki kabla ya kumuhukumu inakupasa umsikilize mhusika, na ndiyo hata mahakama ya Qadhi inavyofanya.

Kwa nini usitengwe muda wa kuwasikiliza hawa raia ambao kwa mtazamo wao wanaona mambo hayapo sawa kisha tujue kama ni mbivu au mbichi ndipo hukumu ipite?!
Kipi kiliwafanya wachome miundombinu na mali za watu?..kata vidole na mikono waliopiga kura?..wasingedhibitiwa hali ingekuaje?.. unataka wasikilizwe nini?.. mikutano waliruhusiwa kufanya, maandamano waliongozwa na polisi,umesusia uchaguzi,kwa nini upange maandamano siku ya uchaguzi?..Sheria inasemaje ukiziwia uchaguzi?
 
Gen z walikua hawajui serikali ni nini,walidhani wazee wao wajinga kuogopa serikali,sasa wameijua
awam ijayo hawatakuja mikono mitupu , jifanyie mnapuuzia malalamiko yao
leo Liberia , Somalia , Drc , Nigeria , Libya , Syria , Iraq , Msumbiji zimepitia hali gan kisa viongoz viziw
 
Ndugu gallow bird

Katika kitabu cha Ihayaa Ulumiddin cha Imam Ghazal anasema; "ukitaka kutibu tatizo inabidi uwe kama daktari. Usitibu athari/matokeo ya ugonjwa bali ili kuutibu inakupasa urudi kwenye chanzo cha ugonjwa."

Hakuna ambaye anakataa kuwa maandamano yalighubikwa na vurugu. Lakini turudi kwenye asili, chanzo cha haya yote ni nini?

Raia kweli miongoni mwao walifanya makosa lakini haya yote yamesababishwa na wenye mamlaka kwa raia kuwazalishia hasira ambazo zimejaa chuki, na chuki huzalisha uharibifu.

Hivyo, ikiwa kweli kama sisi ni wapenda haki basi tuisimamie kama ilivyo, tusiwe watu wa kuchagua.
Asili ya haya yote siyo wananchi bali wanasiasa walafi wa upinzani na wanaharakati wao wanaotaka mabadiliko ya utaratibu wa uchaguzi wakiamini itawaongezea uwezekano wa kushika nafasi kubwa za umma Ili nao wale
 
awam ijayo hawatakuja mikono mitupu , jifanyie mnapuuzia malalamiko yao
leo Liberia , Somalia , Drc , Nigeria , Libya , Syria , Iraq , Msumbiji zimepitia hali gan kisa viongoz viziw
Unadhani silaha ni kalamu unanunua kiosk
 
Ni kweli kabisa, hata hao diaspora watu me arrest warrant ili wauaji washitakiwe
 
Haki kuchoma moto mali za watu!?
Bob Marley aliwahi kusema "You'll never find justice in the world that criminals make the rules"
Baada Raia kuwaondoa madarakani mafisadi, wataenda Kwa machawa wote and that time haitakuwa Tena kuchoma biashara, watawachoma moto chawa wote, Mark My words!
 
Kwanin mtu mmoja, 2 nje wa nchi, hana mamlaka yeyote anawaambia watu watoke waikomboe nchi yao, Bibi yenu, polisi, ma Rc, Dc walisema watu wasiandame lakin hawakusikilizwa?

Unadhani kwanini?
 
Kwenye hii miaka mitano Mama asiwachekee hawa wahuni. Iwe bendera chuma mlingoti chuma.. alikosea sana kuanza utawala wake kwa kuwabembeleza kupita 4R zake. Magufuli aliwajua hawa wachumia tumbo ndo maana aliwapelekea moto.
Magufuli hakuteka hakuua hakuwabambikia kesi chadema, yeye alizuia mikutano na kuwaibia kura tu
 
Nyi wakosa adabu mtaendelea kuoneshwa serikali ni nini, nadhani mmeijua sasa..unahamasishwa na mdangaji yuko marekani,eti jeshi lipo na wananchi!
Serikali ya ccm kazi yake ni kukalia uonevu mda mwingi badala ya maendeleo imekuwa serikali ya kupenda kesi kesi kuwabambikia kesi chadema badala ya maendeleo
 
Msingefanya vurugu asingeuawa mtu,kwa nini mlichoma mwendokasi?..sheli, biashara za watu?
Kwa nini uteke kuua watu yupo wapi mdude na wenzake? Chanzo cha vurugu ni wewe na ushetani wako
 
Watu wameuawa, biashara, makazi, miundombinu imechomwa, maisha yametatizwa, nchi imechafuliwa
Yote haya yanatokana na wanasiasa na wanaharakati wao kuchochea vurugu mitandaoni na kauli zao za kuhamasisha kwenye majukwaa ya kisiasa.

Wanasiasa na wanaharakati wote washughulikiwe mara moja Ili kuepusha hili kujirudia
Hakuna historia inayorukwa katika ustawi wa taifa. Tunaodhani kuwa wao ni chanzo Cha vurugu inatupasa kufanya utafiti nini hasa chanzo Cha vurugu, akina nani wamepelekea watu kuandamana na kufanya vurugu hizo, nini maana ya vurugu hizo?
Mimi ilinishangaza kuona siku Moja kabla ya uchaguzi viongozi wa dini walitumika sana kuhuburi Amani, wakati muda mwingi walikaa kimya. Tusilaumu mambo yaliyotokea Bali tuyachunguze matendo yetu
 
Kipi kiliwafanya wachome miundombinu na mali za watu?..kata vidole na mikono waliopiga kura?..wasingedhibitiwa hali ingekuaje?.. unataka wasikilizwe nini?.. mikutano waliruhusiwa kufanya, maandamano waliongozwa na polisi,umesusia uchaguzi,kwa nini upange maandamano siku ya uchaguzi?..Sheria inasemaje ukiziwia uchaguzi?
Tume ipi ya uchaguzi? Tume ya ccm isimamie uchaguzi? na Tanzania kuna uchaguzi? acha kufananisha maigizo ya uchaguzi na uchaguzi wa kweli, nani kapiga kura? Vituo vilikuwa vitupu
 
Hakuna historia inayorukwa katika ustawi wa taifa. Tunaodhani kuwa wao ni chanzo Cha vurugu inatupasa kufanya utafiti nini hasa chanzo Cha vurugu, akina nani wamepelekea watu kuandamana na kufanya vurugu hizo, nini maana ya vurugu hizo?
Mimi ilinishangaza kuona siku Moja kabla ya uchaguzi viongozi wa dini walitumika sana kuhuburi Amani, wakati muda mwingi walikaa kimya. Tusilaumu mambo yaliyotokea Bali tuyachunguze matendo yetu
Bakwata huwa hawakemei manyanyaso ya ccm kwa wapinzani, hawajawahi kukemea utekaji mauaji na hata ccm kuwabambikia kesi za uongo chadema
 
Back
Top Bottom