Waliochochea vurugu washughulikiwe

Waliochochea vurugu washughulikiwe

Watu wameuawa, biashara, makazi, miundombinu imechomwa, maisha yametatizwa, nchi imechafuliwa
Yote haya yanatokana na wanasiasa na wanaharakati wao kuchochea vurugu mitandaoni na kauli zao za kuhamasisha kwenye majukwaa ya kisiasa.

Wanasiasa na wanaharakati wote washughulikiwe mara moja Ili kuepusha hili kujirudia
Kufanya hilo kwa sasa ni kumwaga petrol kwenye mafuta. Kama umefanya jitihada kusikiliza pande zote mbili, serikali na vyombo vyake kwa upande mmoja na wananchi walioandamana kwa upande mwingine, utakubaliana na mm hakuna upande innocent 100%, some how, pande zote zina cha kulaumiwa kwenye hili. Chamsingi ifanyike tathmini ya kina kwanini tumefika hapa ili tujiwekee mikakati ya kuzuia yaliyotokea yasitokee tena.
 
Kipi kiliwafanya wachome miundombinu na mali za watu?..kata vidole na mikono waliopiga kura?..wasingedhibitiwa hali ingekuaje?.. unataka wasikilizwe nini?.. mikutano waliruhusiwa kufanya, maandamano waliongozwa na polisi,umesusia uchaguzi,kwa nini upange maandamano siku ya uchaguzi?..Sheria inasemaje ukiziwia uchaguzi?
Nakubaliana na wewe kuwa walichofanya si sahihi!

Ila mamlaka nayo inavyowafanyia raia wake si sahihi!

Ajabu, unakemea raia lakini kwenye mamlaka hutaki kukemea.

Hii ni haki ya namna ipi unataka kuiongelea ewe Sheikh?
 
Sheikh, ina maana kweli haki huijui? Au unatetea kile ambacho kinakupatia manufaa?
Sinufaiki na chochote zaidi ya shughuli zangu za kilimo,ila huu mchezo wa 'kidini' huenda huuelewi
 
Nakubaliana na wewe kuwa walichofanya si sahihi!

Ila mamlaka nayo inavyowafanyia raia wake si sahihi!

Ajabu, unakemea raia lakini kwenye mamlaka hutaki kukemea.

Hii ni haki ya namna ipi unataka kuiongelea ewe Sheikh?
Sheikh,yale yalikua mapinduzi, unadhani zile vurugu zingetulizwa na mabomu ya machozi ambayo dawa yake maji na mafuta ya nazi?..yasingedhibitiwa leo tungekua tunaongea nini?.. tungekua na dar,Arusha,mwanza,mbeya!?..au ingebaki majivu?.. mapinduzi huzimwa kwa kumwaga damu
 
Asili ya haya yote siyo wananchi bali wanasiasa walafi wa upinzani na wanaharakati wao wanaotaka mabadiliko ya utaratibu wa uchaguzi wakiamini itawaongezea uwezekano wa kushika nafasi kubwa za umma Ili nao wale
Sasa nimeelewa kwa nini kwenye dini unafiki umezungumziwa ni mbaya sana! Na nimeelewa kwa nini Mtume anasema wanafiki wapo kwenye daraja la chini la moto!

Ashukuriwe Allah aliyemleta Mtume, maneno aliyoyazungumza ni ya kweli.
 
Siyo mtume aliyesema wanafiki watakua moto wa chini kabisa bali mwenyezi Mungu kwenye Quran suratul munaafiquun
 
Sinufaiki na chochote zaidi ya shughuli zangu za kilimo,ila huu mchezo wa 'kidini' huenda huuelewi
Daima, mimi siangalii udini! Daima, naangalia kilichozungumzwa kwenye dini.

Hivyo, hukumu zangu zinatoka kwenye misingi ya dini, na wala si michezo inayochezwa na wahusika wanaojivalisha uhusika wa udini.
 
Siyo mtume aliyesema wanafiki watakua moto wa chini kabisa bali mwenyezi Mungu kwenye Quran suratul munaafiquun
Upo sahihi!

Na kwa msingi huo, simama katika njia ya kweli.

Wayahudi hila zao zinafahamika tangu karne kwa karne. Kipindi cha Imam Ghazal, Qadhi wa hilo eneo alitoa hukumu ambayo haikuwa katika misingi ya sheria za dini bali misingi ya ghadhabu aliyonayo kuhusu wayahudi. Akatoa hukumu wayahudi wote wanayang'anywe mali zao.

Imam Ghazal akamwambia hukumu unayoitoa si sahihi! Yule Qadhi akamhukumu Imam Ghazal kuwa naye ni ya myahudi.

Huu ndiyo mchezo ambao unaoucheza wewe! Pengine tujaalie kuna udini. Lakini je, hukumu unayosimamia na maazimio yanayofanyika yamo katika misingi ya haki ya Mungu na Mtume wake alivyoamrisha?
 
Nikusahihishe,inapaswa kuwa haki ya mwenyezi Mungu siyo na mtume wake,hiyo ni shirki
Tuje kwenye unayoyaona si haki,japo sijui unalenga nini hasa,ila tuchukulie ni vurugu za uchaguzi
Wewe ulitaka zile vurugu zidhibitiwe vipi?
 
Sheikh,yale yalikua mapinduzi, unadhani zile vurugu zingetulizwa na mabomu ya machozi ambayo dawa yake maji na mafuta ya nazi?..yasingedhibitiwa leo tungekua tunaongea nini?.. tungekua na dar,Arusha,mwanza,mbeya!?..au ingebaki majivu?.. mapinduzi huzimwa kwa kumwaga damu
Sasa hayo ni matokeo!

Lakini asili ya haya yote ni nini?!

Hivyo ukiwa unataka kutibu tatizo rudi kwenye chanzo!

Hao waliyoandamana ni raia wa nchi hii! Wasikilizwe hoja zao! Kama zina mantiki zifanyiwe kazi, na kama hazina mantiki waelimishwe uhakika wa mambo jinsi ulivyo!

Kwa sababu waliyoandamana walikuwa na hoja zao. Na huo ndiyo utaratibu mzuri.
 
Nikusahihishe,inapaswa kuwa haki ya mwenyezi Mungu siyo na mtume wake,hiyo ni shirki
Inakupasa uifahamu lugha.

Mtume anasema: Manistaraqqa wamanistawa wapo mbali na kumtegemea Allah!

Yaani, anayetibu na anayetibiwa wapo mbali na kumtegemea Allah!

Hii ni hadithi sahihi!

Umeelewaje hayo maneno? Na unafafanuaje?
Tuje kwenye unayoyaona si haki,japo sijui unalenga nini hasa,ila tuchukulie ni vurugu za uchaguzi
Wewe ulitaka zile vurugu zidhibitiwe vipi?
Hoja zako zinajikita kwenye masuala ya udini na unashikwa na upofu na kuchupq mipaka ya kushindwa kuitambua haki.
 
Sasa nimeelewa kwa nini kwenye dini unafiki umezungumziwa ni mbaya sana! Na nimeelewa kwa nini Mtume anasema wanafiki wapo kwenye daraja la chini la moto!

Ashukuriwe Allah aliyemleta Mtume, maneno aliyoyazungumza ni ya kweli.
hakuna mtu ambae sio mnafki, ata wewe kuna sehem ni mnafki japo hatutaki kujua sana maisha ya mtu, unafki ni hulka ya binadam ndo maaana ni neno halisi

2) ushawahi kuona wap mwananchi anashindana na serikali? kiuhalisia unatakiwa uwe na heshima nayo ndo maaana Mwenyezi Mungu mwenyewe akasema HESHIMUNI MAMLAKA ILOPO JUU YENU

tatizo vijana mnafuata siasa za upepo na pia hamtaki kuambiwa ukwel, mnatumika na watu ambai hamjui dhumuni lao ni nn, serikali mkono wake ni mrefu yatakayotokea yapokee, uliyatafuta
 
Sasa hayo ni matokeo!

Lakini asili ya haya yote ni nini?!

Hivyo ukiwa unataka kutibu tatizo rudi kwenye chanzo!

Hao waliyoandamana ni raia wa nchi hii! Wasikilizwe hoja zao! Kama zina mantiki zifanyiwe kazi, na kama hazina mantiki waelimishwe uhakika wa mambo jinsi ulivyo!

Kwa sababu waliyoandamana walikuwa na hoja zao. Na huo ndiyo utaratibu mzuri.
je walioandamana walileta hoja? waliweka mabango?
 
Sasa hayo ni matokeo!

Lakini asili ya haya yote ni nini?!

Hivyo ukiwa unataka kutibu tatizo rudi kwenye chanzo!

Hao waliyoandamana ni raia wa nchi hii! Wasikilizwe hoja zao! Kama zina mantiki zifanyiwe kazi, na kama hazina mantiki waelimishwe uhakika wa mambo jinsi ulivyo!

Kwa sababu waliyoandamana walikuwa na hoja zao. Na huo ndiyo utaratibu mzuri.
Hoja zipi?..katiba mpya mchakato uliahidiwa mwakani,watu kutekwa tumeona mapadre wawili walivyojiteka,tumeona waganga wa kienyeji kule dom na singida walivyohusika,tumeona sheikh alivyojiteka singida,tumeona jaribio la utekaji kibaha hawakuwa polisi na wahusika wamefungwa miaka saba
 
hakuna mtu ambae sio mnafki, ata wewe kuna sehem ni mnafki japo hatutaki kujua sana maisha ya mtu, unafki ni hulka ya binadam ndo maaana ni neno halisi

2) ushawahi kuona wap mwananchi anashindana na serikali? kiuhalisia unatakiwa uwe na heshima nayo ndo maaana Mwenyezi Mungu mwenyewe akasema HESHIMUNI MAMLAKA ILOPO JUU YENU

tatizo vijana mnafuata siasa za upepo na pia hamtaki kuambiwa ukwel, mnatumika na watu ambai hamjui dhumuni lao ni nn, serikali mkono wake ni mrefu yatakayotokea yapokee, uliyatafuta
Serikali ni watu mkuu na ipo hapo kwa ajiri ya watu, serikali inaundwa na watu kama mimi na wewe tu hivyo usifanye ionekane ni kitu cha ajabu sana.
 
Samia aliahidi na kuwahakikishia kama amiri jeshi mkuu kuwa hakutakuwa na vurugu zozote kwenye uchaguzi, ila kilichotokea akaamuru kufanyike mauwaji hadi kwa wasiohusika na vurugu.
 
Serikali ni watu mkuu na ipo hapo kwa ajiri ya watu, serikali inaundwa na watu kama mimi na wewe tu hivyo usifanye ionekane ni kitu cha ajabu sana.
sawa mkuu, unadhan tutawashauri tena
 
sawa mkuu, unadhan tutawashauri tena
Umshauri nani wakati wote ni wahanga tu wewe kuiogopa au kuiheshimu serikali haikufanyi kuwa salama tofauti na wengine, tazima mauwaji ya polisi waliyoyafanya hawakuangalia nani anahusika na vurugu wala nani anaheshimu serikali.
 
Back
Top Bottom