Candid Scope
JF-Expert Member
- Nov 8, 2010
- 11,883
- 6,884
Mkuu, unachosema ni sahihi na naona hoja yako ni ya msingi kabisa. Hata hivyo, inabidi ujiulize huo mkataba utakaoufunga na serikali utafungwa kwa kutumia sheria ipi? Hakuna mkataba bila sheria. Ndio maana nikasema ipitie sheria ya manunuzi ya mwaka 2004.
Pamoja na uwepo wa sheria ya manunuzi, sheria hiyo imezingatia tenda zinazotangwazwa na serikali, lakini upo mwanya pia wa raia ye yote kuomba idhini ya serikali kushughulikia kile ambacho serikali haijatangaza. Kwa utaratibu huo, ombi la mhusika hufikishwa kwenye vikao husika. Vikao vikikubaliana na ombi hilo, serikali itatoa tangazo kwenye gazeti la serikali kwa muda muafaka kuona kama kuna pingamizi la kisheria. Kusipotokea pingamizi la kisheria lenye kuweka zuio la ajenda hiyo, basi serikali itakuwa imejiridhisha kumpa mkataba mhusika.
Ulichosema wewe ni sawa, lakini umebana zaidi kwenye sheria ya manunuzi inayotangazwa na serikali, ila katika sheria hiyo haijaweka kipengela cha hoja aliyosema Njele.
Kuna baraza la madiwani ambalo mara nyingi ndilo linaloweza kutoa baraka wakiona jambo hilo ni la manufaa kwa umma. Binafsi ningeshauri Mdau Njele kuongea na ofisi ya Madiwani wa eneo husika, hao mara nyingi wapo karibu ya wananchi na wanajali masilahi ya wananchi na wanaweza kumsaidia kufikia malengo yenye manufaa kwa wananchi.