Waliochagua kubaki kupiga box majuu waliona mbali | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Waliochagua kubaki kupiga box majuu waliona mbali

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Njele, Aug 19, 2012.

 1. N

  Njele JF-Expert Member

  #1
  Aug 19, 2012
  Joined: Jan 5, 2012
  Messages: 275
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Hali ya mazingira ya kukatisha tamaa kwa watanzania kutokana na serikali kutojali maisha ya watumishi wa umma na wananchi, nabadili mawazo na kuwa waliobahatika kuwa huko majuu na kupata nafasi ya kupiga box waliona mbali kuliko tulioamua kurudi kwani tumepoteza hata mafao tuliopigia box. Inakatisha tamaa mambo yasiyvyoleta matumaini na kwa kuwa sikutupa jongoo na mti wake naamua kuridi kupiga box ughaibuni pamoja na kwamba nako maisha magumu yanawafungua macho wazungu waliozoea kutupa hifadhi katika nchi zao.

  Nimejitahidi kuishawishi serikali katika mambo kadhaa ikiwa ni pamoja na kutaka kuchukua maeneo ya wazi kimkataba ambayo yalitengwa kwa ajili ya michezo na burudani mbalimbali ili niyaendeleze kwa malengo yayo hayo kuwa viwanja vizuri vya michezo na bustani za mapumziko, nimeishiwa kutishiwa mambo ambayo sikutegemea. Kitu kama hicho ndicho kinachofanyika katika nchi nilikokuwa napiga box na mtu anayejitolea kufanya hivyo anaonekana yupo kwenye chanda cha dhahabu ndani ya kisahani lakini bongo unaonekana usiyefaa na wa kutaka kujineemesha wakati sitahitaji pesa toka serikalini na maeneo hayo yanazidi kutia aibu kila kukicha. Kuna mengi ila sipendi kuyatapika hapa.
   
 2. Kijakazi

  Kijakazi JF-Expert Member

  #2
  Aug 19, 2012
  Joined: Jun 26, 2007
  Messages: 3,546
  Likes Received: 44
  Trophy Points: 135

  Kama kawaida, kulinganisha vitu ambavyo havilingani! nani alikwambia watanzaia shida yao maeneo ya kupumzikia? Hivi ni kwa nini wote mnaoishi nje ya nchi mnafanana? Kama kweli ni Mtanzania, ulizaliwa na ukakulia hapa ulipaswa kuwa wa kwanza kuelewa kwamba mambo kama hayo hayajulikani hapa na utaonekana wa ajabu ukianza kuyaongelea!

  Hivi mbona mko tofauti na wazungu? mbona wao hawako hivyo? Mbona wao wanakuja hapa na kuanzisha vitu ambavyo vinaendana na matakwa ya jamii yetu na wanafanikiwa? Mbona huwasikii wakilialia kama ninyi tena ambao mmezaliwa hapa? Hata wahindi hawako hivyo mbona hawalilii hovyo kama nyinyi, kuna mambo mengi unaweza kufanya Tz na yakakubalika angalia mfano yule mhindi wa Haki Elimu kasoma Marekani kaja hapa kaanzisha kitu leo hii kinaleta tofauti katika jamii, mbona wao hawalilii hovyo kama nyinyi? ni kwa nini lakini wakati mmezaliwa hapa na mnaielewa hii jamii kwa maana na nyie sehemu yake?

  Hivi kweli mtanzania wa kawaida utamwambia mambo ya sehemu ya kumpumzika atakuelea? kwa nini usifanye vitu amabvyo vinaendana na mazingira yetu kama wenzenu wazungu wakitoka huko wanavyofanya?

   
 3. kupe

  kupe JF-Expert Member

  #3
  Aug 19, 2012
  Joined: Jul 26, 2012
  Messages: 1,025
  Likes Received: 93
  Trophy Points: 145
  hahahahaha kupunzika bongo. hiyo foleni yenyewe ya kwenye daladala ukiwa unatoka kazini ni mapunziko tosha . unafika nyumbani usiku umechoka unafikia kujitupa kitandani uamke mapema kesho saa kumi usiku. (WATANZANIA HAWAHITAJI GARDEN ZAKUPUNZIKIA WALA VIWANJA VYA MICHEZO) utapunzika vipi wakati unaishi kwa dhiki na mawazo
   
 4. N

  Njele JF-Expert Member

  #4
  Aug 20, 2012
  Joined: Jan 5, 2012
  Messages: 275
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Kila mtu ana utume wake kwa jamii. Wahindi wamekuja na mambo yako ya biashara ndizo wanazozifisha. Wazungu toka huko walikotoka walishajua nini wanakuja kufanya kama ni kuanzisha makampuni ya simu, au kuchimba madini, au kufanya kazi mahospitalini, au kuchimba visima vya maji, katu hawatabadili kwa kuwa vibali na visa walivyoingilia ndio hivyo.

  Mzawa unatakiwa kuangalia kipana kwa vile si mtu wa kupita, ni nyumbani. Maeneo yaliyotengwa kuwa wazi yanatia huruma kuwa vichaka vya vibaka, timu za mitaani ambazo ni chumbuko la vipaji kukosa viwanja vyenye hadhi vya kuchezea. Watoto kukosa social life ya michezo ya kiwango ambayo humsaidia kukua vizuri kimwili na kiakili, na mengineyo tusiwe wachoyo, kwani niliyojifunza huko nilipokuwa chuo na kupiga box yaliyo mazuri napenda kuyaendeleza, ila viongozi hawako tayari kuruhusu maendeleo haya..
   
 5. N

  Njele JF-Expert Member

  #5
  Aug 20, 2012
  Joined: Jan 5, 2012
  Messages: 275
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Nilijitutumua kuingia mpaka office ya Mkurugenzi wa maendeleo Mkoa wa Dar kumshauri kuhusu tatizo la msongamano wa magari kwamba ni shida inayowezekana kuondokana katika muda mfupi iwapo tu watafanya yafuatayo:
  1. Kujenga belt-way (park way) ambayo itaanzia Mbezi beach kupitia Mbezi Juu, Pugu, Mbagala hadi kuunganisha kule Mji Mwema kwa Abdu Jumbe na kuishia Kivukoni kwa kiwango cha express high way.
  2. Kujenga barabara kadhaa ambazo zitaunganisha na hiyo belt-way (park way) kuunganisha na maeneo mengine, na kubuni barabara nyingi mitaani zinazounganika na barabara kubwa kama Kilwa Road, Bagamoyo Road, Morogoro Road, Pugu Road.
  3. Kuhakikisha barabara zote za mitaani ni nzuri na zinapitika wakati wote ili watu wawe na alternative ya kuchagua njia.
  4. Kuruhusu commuter bus zenye kuchukua watu kuanzia 45 sitters badala ya madogo ambayo huongeza msongamano kwa wingi wake.
  5. Kuwepo na usafiri wa train kwa baadhi ya maendo ambayo yana msongamano msongamano zaidi. Mfano Gongolamboto kuna reli imepita pale, kama kungekuwa na train ingerahisisha kupunguza watu kudandia kupitia madirishani.

  Ushauri wangu huo ulijikita katika maana ya kwamba miji mkubwa daima njia zinatengenezwa kwa kichocheo cha kuvutia watu kupita nje kidogo ya mji ili kupunguza msongamano, la sivyo kujanga fly overs katikati ya jiji kwa sasa hivi maana yake ni kuendelea kuweka vivutio vya magari kujaa mjini ambako hakuna sababu, ampapo magari yanayoenda mjini yangekuwa ni yale yanayohitaji kwenda huko tu.
   
 6. sunshine1

  sunshine1 JF-Expert Member

  #6
  Aug 20, 2012
  Joined: Sep 30, 2011
  Messages: 523
  Likes Received: 91
  Trophy Points: 45
  Pole sana ndugu. Nakuelewa sana unachomaanisha. Ila kwa bahati mbaya mtu ukshakuwa nje ya nchi unarudi na mtazamo na uelewa ambao kiukweli kama mtu hajawahi kufika hata hapo Kenya ni ngumu sana kuelewa. Kuna swala laku supply kulingana na demand ila pia kuna possibility zaku create demand ili uweze kusuply. Tz bado sana! Unajua mtu ukiwa hapo Tz unafurahia kusema mi mnyakyusa, mpare, mchaga n.k. Ila siku ukitoka nje ya Tz ndiyo unaelewa nikwajinsi gani utanzania unakuhusu na jinsi hali ya nchi inavyoweza kukufanya ukafeel guilty kama vile wewe ndiyo rais wa nchi. Still we have a long way to go for people to understand the meaning, value and worth of being Tanzanian


   
 7. N

  Njele JF-Expert Member

  #7
  Aug 20, 2012
  Joined: Jan 5, 2012
  Messages: 275
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Nimekuelewa sana, uliyosema ni ukweli ambao nimeushuhudia, kwani nisawa na kumpigia mbuzi muziki mzuri lakini yeye anaendelea na hamsini zake kuhangaika kutafuta majani ya kula, kwani jasho lote na jitihada zote za kupiga marimba mbuzi hana habari. Ipo kazi kweli kweli.
   
 8. Z

  ZeMarcopolo JF-Expert Member

  #8
  Aug 20, 2012
  Joined: May 11, 2008
  Messages: 13,589
  Likes Received: 480
  Trophy Points: 180
  Mkuu, ulichotaka kufanya wewe ni kuuza huduma. Ulichotakiwa kufanya ni kusoma vizuri na kuielewa Public Procurement Act ya mwaka 2004, halafu ungejua nini cha kufaya ili ufanikiwe kuuza huduma yako.
   
 9. Candid Scope

  Candid Scope JF-Expert Member

  #9
  Aug 20, 2012
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 11,896
  Likes Received: 119
  Trophy Points: 160
  Kama una bahati ya kurudia huko ulikokuwa unapiga box ni bora, maana haya uliyoelezea yanakatisha tamaa kwa mwenye kutaka kutumia utashi wake kwa manufaa yetu sote watanzania. Sishangai kwa yaliyokupata kwani hali halisi ya serikali ya CCM ndivyo hivyo, ukilazimisha utageuka muokota makopo.

  Kumbuka huko kama umefanya kazi kwa kiwango (miaka isiyopungua 10) kinachokufaa utakuwa na mafao stahiki uzeeni kwa kuwa na kipato cha kila mwezi hadi utakapomwendea baba wa Milele. Ila jitahidi kuwekeza pia bongo katika maeneo ambayo hayaguswi na wakuu vinginevyo watakugeuzia kibao na kukunyang'anya kwa visingizio mbalimbali ikiwa na pamoja kukubambikizia mambo yatakayokushangaza na kuamua bora kuachia uliyo nayo ili ubaki na amani yako.

  Hata hivyo usikate tamaa, unaweza kurudi huku na ukabaki na wazo lako zuri la kutengeneza mazingira mazuri ya bustahi za kupumzikia na maburudisho mbalimbali ya michezo, wakati ukiwadia tukishawaondoa hawa vinara wa kutuzuga kila kukicha basi tutawaiteni mje, maana kwa sasa tunajua mnafanya jitihada huko kuandaa mitaji ya kuwekeza ili kujenga uchumi wa nchi yetu.
   
 10. Candid Scope

  Candid Scope JF-Expert Member

  #10
  Aug 20, 2012
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 11,896
  Likes Received: 119
  Trophy Points: 160
  Umefunua kitu ambacho huenda wengi hawakijui kuhusu Public Procurement Act ya Mwaka 2004, ungajaribu kutufafanulia kwani kuna wengi wanaotaka kuijua zaidi ya huyu Njele.
   
 11. Kijakazi

  Kijakazi JF-Expert Member

  #11
  Aug 20, 2012
  Joined: Jun 26, 2007
  Messages: 3,546
  Likes Received: 44
  Trophy Points: 135

  Na hapo ndio mnapokosea kwa maana mko out of touch na ndio maana nikakutolea mfano wa wazungu au wageni wengine kabla hawajaamua kuja Tanzania wanafanya kwanza utafiti na wanajifunza nakusoma kwanza watu wakoje na wanautamaduni gani kwa hiyo hawezi kuja hapa na kuanza kuongelea mambo ya kujenga bustani ya kupumzikia wakati huyo unaemjengea wala haelewi maana ya hicho kitu, ana matatizo mengine kabisa, ukimwambia mtanzania wa kawaida kwamba watoto hawana mahali pa kuchezea eti unataka kuwajengea hawezi kukuelewa, na ndio maana hata ukiaangalia makampuni makubwa kwa mfano Samsung wanauza bidhaa ambao ziko tofauti na bidhaa za wanazouza sehemu nyingine unafikiri kwa nini? si wanajua mazingira ni tofauti, TV inayotengezwa for African market sio sawa na for European market huo ni mfano tu!

  Kwa hiyo wazo lako labda sio baya lkn kwa kwetu hapa halitaeleweka, ni bora hata ungeanzisha tuition kwa watoto ya kujitolea bure hapo ungeeleweka! kuna kina kitabu kinaitwa "what makes people tick"
  ukikisoma kinaelezea jinsi ya kuweza kutambua tabia na tamaduni za watu ili uweze kuishi na kuendana nao vinginevyo utakuwa unaonekana kichekesho kwa sababu hutaeleweka!
   
 12. Candid Scope

  Candid Scope JF-Expert Member

  #12
  Aug 20, 2012
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 11,896
  Likes Received: 119
  Trophy Points: 160
  Wamisionari walipokuwa walikuja kutalii kuangalia kama waafrika tunahitaji dini?
  Wakoloni walipokuja kututawala tulishakuwa na watawala wetu na waliingia kwa nguvu ya magobole, kwani waafrika tulihitaji hawa wazungu waje kututawala au vipi?

  Hitaji lipo, utakuwa watu wanavyofurahia bustani za Mnazimmoja, pale St. Joseph, kule kwenye mchezo wa golf nk.
  • Ni hakika bustani zinahitajika
  • Ni hakika vijana wanahitaji viwanja vizuri vya kuchezea michezo
  • Ni hakika watoto wanataka maeneo mazuri ya kuchezea, leo Idd tazama walivyojazana ufukwe wa Bahari au kile kitega uchumi Mbagala, ila wakuu wetu hawafunguki.

  Inawezekana huyu Njele alishaona wazo lake linapokeleka, na hajalalamika kwamba wananchi walimkatisha tamaa, bali anasema viongozi wa serikali ndo waliomtisha na kumkatisha tamaa. Tutetee mambo kwa misingi ya ukweli katika mazingira ya leo.
   
 13. Kijakazi

  Kijakazi JF-Expert Member

  #13
  Aug 20, 2012
  Joined: Jun 26, 2007
  Messages: 3,546
  Likes Received: 44
  Trophy Points: 135
  Mzawa unatakiwa kuangalia kipana kwa vile si mtu wa kupita, ni nyumbani. Maeneo yaliyotengwa kuwa wazi yanatia huruma kuwa vichaka vya vibaka, timu za mitaani ambazo ni chumbuko la vipaji kukosa viwanja vyenye hadhi vya kuchezea. Watoto kukosa social life ya michezo ya kiwango ambayo humsaidia kukua vizuri kimwili na kiakili, na mengineyo tusiwe wachoyo, kwani niliyojifunza huko nilipokuwa chuo na kupiga box yaliyo mazuri napenda kuyaendeleza, ila viongozi hawako tayari kuruhusu maendeleo haya..[/QUOTE]

  Wewe nafikiri labda uliondoka Tz mtoto na huelewi maisha ya mtanzania wa kawaida ni kama yule anaesema treni zianze kubeba watu halafu watu watanunua tiketi ya mwezi kisa kaona Ulaya wanafanya hivyo anataka Tz hivyo hivyo!
  Hayo unayoongea sijui ya mtoto kukua kimwili na kiakili kwa kucheza kwenye bustani nzuri yako irrellevant hapa nyumbani kwa maana unapaswa kufahamu ili mtoto aweze kukua kimwili na kiakili kwanza anahitaji lishe bora kabla ya hayo mambo ya viwanja vya kuchezea, na sehemu kubwa ya watz kula x3 kwa siku achilia mbali kula chakula bora tabu leo hii ukawaambie unataka kujenga sijui bustani ili wapate sehemu ya kuchezea? kwanza sehemu ya kucheza kwa watoto wengi sio shida karibu shule zote msingi zina viwanja watoto wanacheza huko, mawazo yako mazuri lakini hayako relevant hapa nyumbani labda ulaya!

   
 14. Candid Scope

  Candid Scope JF-Expert Member

  #14
  Aug 20, 2012
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 11,896
  Likes Received: 119
  Trophy Points: 160

  Wewe nafikiri labda uliondoka Tz mtoto na huelewi maisha ya mtanzania wa kawaida ni kama yule anaesema treni zianze kubeba watu halafu watu watanunua tiketi ya mwezi kisa kaona Ulaya wanafanya hivyo anataka Tz hivyo hivyo!
  Hayo unayoongea sijui ya mtoto kukua kimwili na kiakili kwa kucheza kwenye bustani nzuri yako irrellevant hapa nyumbani kwa maana unapaswa kufahamu ili mtoto aweze kukua kimwili na kiakili kwanza anahitaji lishe bora kabla ya hayo mambo ya viwanja vya kuchezea, na sehemu kubwa ya watz kula x3 kwa siku achilia mbali kula chakula bora tabu leo hii ukawaambie unataka kujenga sijui bustani ili wapate sehemu ya kuchezea? kwanza sehemu ya kucheza kwa watoto wengi sio shida karibu shule zote msingi zina viwanja watoto wanacheza huko, mawazo yako mazuri lakini hayako relevant hapa nyumbani labda ulaya!

  [/QUOTE]

  Tusijenge utetezi usikuwa wa kweli. Umeona Kikwete alivyotoa kauli kule Maputo kuhusu kuwatuhumu akina Lowasa na Membe kwamba ni wapinzani wake kisiasa kwa kutishia Malawi walipodai Tanzania tunataka kulinda mipaka ya nchi yetu. Hapo unaweza kuona mfano wa huhu Njele tatizo si wananchi, tatizo aliloliainisha wazi ni viongozi wetu. Hakuna mwananchi asiyependa maendeleo, ukiweka sehemu ya namna hiyo utaona kesho wamejazana kwenye mapumziko, angalia maeneo mengine wazi yaliyotunzwa vizuri yanavyojaza watu.

  Tukubali tatizo ni viongozi wetu, wala si wananchi au mazingira ya leo, tujue kwamba ulimwengu wa leo ni global village, kila kona ya dunia inaonekana kipa pande ya dunia na ni mwalimu tosha, hakuna haja kubwa ya kukalishana madrasat kuelimishana hayo.
   
 15. Z

  ZeMarcopolo JF-Expert Member

  #15
  Aug 20, 2012
  Joined: May 11, 2008
  Messages: 13,589
  Likes Received: 480
  Trophy Points: 180
  hii hapa...
  View attachment 62455
   
 16. Kijakazi

  Kijakazi JF-Expert Member

  #16
  Aug 20, 2012
  Joined: Jun 26, 2007
  Messages: 3,546
  Likes Received: 44
  Trophy Points: 135
  Shida ni kwamba huyu kama ukisoma origin post yake analalamika kwamba ameshindwa na sasa anarudi alikotoka, na mimi ndio nikamwambia hiyo ni kawaida ya watz wanaoishi nje (sio wote) wakija hapa wanataka wote tubadilike tuwe kama wao wanasahau kwamba sisi tumelelewa vingine na tuna priorities tofauti, kwa hiyo japokuwa kuwa na bustani sio jambo baya lkn haliwezi kuwa priority kwa mtz wa kawaida na hawezi kukuelewa, kwa hiyo leo hii ukienda ofisini kwa mtu halafu unaanza kumwambia unataka kujenga sijui bustani atakupuuza tu!

  Tanzania sasa hivi tuna matatizo mengi sana wadogo zetu hawasomi hawana vitabu, wengine hawawezi hata kwenda shule kisa njaa, wengi wanashindwa kulipa sh 2000 kwa mwaka kwenda shule huwezi amini lkn ndio ukweli sasa mambo ya bustani ya kupumzika yana nafasi kweli?

   
 17. Z

  ZeMarcopolo JF-Expert Member

  #17
  Aug 20, 2012
  Joined: May 11, 2008
  Messages: 13,589
  Likes Received: 480
  Trophy Points: 180
  Mkuu sana, unaweza kuwa sahihi, lakini nilichoona mimi huyu ndugu yetu kilichomshinda siyo tamaduni bali ni taaluma ya business and marketing pamoja na ujuzi kidogo wa sheria za manunuzi ya umma. Katima marketing unaweza kumuuzia mtu kitu hata kama hakihitaji au siyo kipaumbele chake kutokana na jinsi utakavyokitangaza. Huyu mwenzetu hilo limemshinda. Vilevile ndugu yetu huyu ameamua kuuza biashara yake kwa serikali, hivyi basi alipaswa kujua sheria inayosimamia manunuzi ya serikali.
  Halafu, amejifunga kwa serikali tu. Huduma ya gardening inahitajika na watu wengi, siyo serikalini tu.
   
 18. Kijakazi

  Kijakazi JF-Expert Member

  #18
  Aug 20, 2012
  Joined: Jun 26, 2007
  Messages: 3,546
  Likes Received: 44
  Trophy Points: 135
  Hakuna mwananchi asiyependa maendeleo, ukiweka sehemu ya namna hiyo utaona kesho wamejazana kwenye mapumziko, angalia maeneo mengine wazi yaliyotunzwa vizuri yanavyojaza watu.

  Tukubali tatizo ni viongozi wetu, wala si wananchi au mazingira ya leo, tujue kwamba ulimwengu wa leo ni global village, kila kona ya dunia inaonekana kipa pande ya dunia na ni mwalimu tosha, hakuna haja kubwa ya kukalishana madrasat kuelimishana hayo.[/QUOTE]

  Sasa na hiyo ndio point yangu wewe mwenyewe umesema mbona kuna maeneo na watu wanakwenda sasa yeye ameshindwa nini?
  kwani hayo yalalishushwa kutoka Mars si kuna watu walijenga chini ya viongozi hao hao unaowaita ni tatizo?

  Kwa hiyo kumbe kuna watu ambao wanakomaa na wanaweza kufanye vitu regardles ya uongozi huo unaouita mbaya, sasa yeye ameshindwa nini?
  Ni lazima mtu upambane kama unataka kufanikisha kitu!

  Jamani tunalalamika sana! Wenzetu wanachukua nchi yetu, sisi kulalamika tu, mbona wengine wanafanikiwa? Wahindi hawafiki 200 000 Tanzania nzima lakini wanamilki > 80% ya uchumi wote pamoja na kuwa na hao hao viongozi unaowaita wabaya, kwa nini sisi tushindwe!

  Miaka zamani tulisingizia ukoloni, haya wazungu wakaenda, tukaja mara ujamaa haya ukaja ukaenda, sasa hivi tumepata kisingizio kingine CCM, na kuhakikishia CCM nayo itaenda na bado tutatafuta sababu za kulalamika huku wenzetu wahindi wakipiga kazi na kuendelea kumiliki uchumi na kuendelea!
  TUNALALAMIKA SANA!
   
 19. Z

  ZeMarcopolo JF-Expert Member

  #19
  Aug 20, 2012
  Joined: May 11, 2008
  Messages: 13,589
  Likes Received: 480
  Trophy Points: 180
  Asilimia kumi tu ya watanzania wakianza kufikiria hivi, nchi itachukua less than ten years kuwa kama Dubai.
   
 20. m

  mkwegi Member

  #20
  Aug 20, 2012
  Joined: Feb 9, 2008
  Messages: 20
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 5
  Kijakazi una mtazamo mzuri kwa maana kuwa una sisistiza kwamba ungekuwa wewe ungejua kuwa hilo wazo haliwezekani hapa tz. lakini napenda kutofautiana na wewe kwa mambo mengi lkn hapa nitazungumza kifupi tu. kiukweli kabisa, ni wajibu wetu kuleta new ideas ambazo zinaongeza tija na zenye less competition kwa sababu zinaongeza diversification badala ya kubaki na idea za kuuza juice au kufuga kuku wa nyama na mayai kama ilivyozoeleka kwa kila mkasiriamali. Wengi wetu humu tumeishi ng'ambo na tungetamani kuona vitu vizuri vyenye kuonyesha ubunifu ktk mazingira ya Afrika ukileta manufaa kwetu na faraja. Tatizo ninaloona mimi and correct me if Im wrong, ni kwamba kuna long term target ya watu fulani (wakubwa) kuvichukua hivyo viwanja na hivyo kuifanya idea nzima kushindikana maana itakuwa vigumu wahusika kuviomba kiujanja wakati tayari vimeshagawiwa kwa mtu mwingine. kama alivyoeleza hapo juu Njele, ni kweli wazungu na wahindi wanafanya kile tunachoita "ukila na kipofu usimguse mkono" wanahakikisha wanajifanya wako ktk level sawa na sisi na kutimiza "business as usual" lkn kimsingi wanakuwa na malengo yao yaliyojificha. Endapo tutashindwa kuona point ndani ya hii observation ya Njele basi tutakuwa kama vipofu na huenda kwa miaka hii watanzania wataungana na wale wa west Africa ambao wakifika ulaya hawataki kusikia jina la nchi yao tena kwa kisingizio kuwa hakuna social security na uonevu ni mkubwa maana bado serikali ziko barbaric. TUFUNGUE MACHO TUSISUBIRI WACHINA, WAHINDI NA WAZUNGU KUANZISHA VITU VYOTE VIPYA NA KUTUFANYA SISI TUWE WATU WA KUFUATA TU BILA HATA KUULIZA.
   
Loading...