Serikali imelala kwa vile viongozi wanafikiria zaidi maisha binafsi kuliko uwajibikaji kwa jamii. Maeneo hayo yamesahauliwa na hata hayapangiwi bajeti, na hata kama bajeti yanayo inaishia kununulia soda wakubwa maofisini na kufanyia semina elekezi zisizoleta mabadiliko katika utumishi. Bajeti inayoidhinishwa na bunge badala ya kutumika kama ilivyokusudiwa kwa maendeleo, inatumika kufanya makongamano na semina elekezi na pesa inaishia huko pamoja na posho zake. Mtu binafsi hana nafasi ya kufanya kongamano au semina elekezi ya kutengeneza au kuyaendeleza maeneo wazi, ni kazi tu basi kadiri ya plan ambayo imeidhinishwa na idara husika za serikali.
Malengo ni kutoa mfano mmoja kwanza ambao unaweza kuwavutia wengi na kisha baada ya miezi au mwaka kuona eneo lilivyo kivutio itahamasisha maeneo mengine hata wewe ukaingia mkataba kuyaendeleza kwa utaratibu ambao mimi nilipanga kufanya. Serikali ikishakaa sawa na kuwa na uwezo wa kuyahudumia maeneo hayo, muda wa mkataba ukiisha basi, huduma hiyo inaweza kuhamishiwa kwenye halmashauri ya jiji au mji ili kuendelea kuistawisha. Huu ndio utaratibu ambao hata mataifa yaliyoendelea yamepitia na sasa maeneo hayo ni kivutio na hata wakuu wetu wanaposafiri wanaenda kubembea huko, hayakuja yenyewe, kuna watu waliojituma kubuni, kuyatengeneza na kuyaendeleza.