Walinzi wa Museveni & Gaddafi watwangana vikali- Karume Asukumwa!!!

Kawaida ya waarabu ni ufedhuli na ujeuri hiyo ni silka yao, sidhani kama Gadaffi kajenga huo msikiti kwa nia ya kuuendeleza uislamu bali ni katika kuonesha fahari kama ilivyo kawaida ya jamaa zetu hao. kwa sababu kutoa katika misingi ya kiislamu ni kwamba utowe kwa siri na sio kuutangazia umma au ulimwengu wote ukajua kama alivyofanya yeye.

kitu chengine ambacho kinanishangaza kwa hawa watu misaada ambayo wao naona ni bigdeal ni kujenga misikiti tu, wakati kuna mambo mengi wanaweza kusaidia kama kweli wao ni watu wa msaada. kuna waislamu wengi tu masikini hawana uwezo wa hata kusomesha watoto wao, kuna mayatima lakini sijaona misaada katika channel hiyo.
Ni kweli..lakini this time wao waarabu wanaamini kuwa this is the new crusade..na wanataka waumini wao na raia wote wa dunia waliangalie hilo suala kimtizamo huo!Kwamba Bush na marekani wanapigana vita dhidi ya uislam!N kwa Gadhafi..kutokana na kibri aliyonayo yeye sasa anapigania uislam kanda hii ya Afrika na anachukizwa na ukumbatiwaji wa Bush na westinism?Swali ni moja hapa.."where are we going to stand?"
 
Huyu Gadafi hata kama ana urafiki na sisi ni wa kinafiki tu...wakati wa vita na Idi Amin si alituma majeshi yake kumsaidia Amin,sasa sijui kama alishatuomba msamaha au vipi.
Hawa mabodigadi nao kupigana ni poa tu,maana wanafanya mazoezi sana.Sasa kama wanakosa mtu wa kutishia maisha ya kiongozi wao,si ni bora wafuane wenyewe tu.Maana wengi huwa wanakaa na viongozi wao,mpaka wanastaafu bila ya kasheshe lolote,hata mlipuko wa tyre burst wa kuwashtua kidogo hakuna!
Huku kwetu kuna mabodigadi ukiona wana vitambi wengine,sasa kama issue ndio ya kusukumana,duh!
 
nashauri ghadaffi asikanyage tanzania...hivi alikuja kumzika mwalimu??..nakumbuka ali,pa pesa mwlimu ya kujenga msikiti wa butiama...akitaka anaweza kujenga misikiti yote hapa ..lakini hawezi kuja kuifungua kwenye ziara ya kiserekali..kwa kuwa nchi yetu haina dini..na hatuataki vurugu...

Hivi wakati viongozi wetu wakiwemo mafisadi waliotukuka wanapanga msururu wa kufungua na kuchangia ujenzi wa makanisa na shughuli zengine za kidini huwa hawatumii kodi za wananchi? Anyway huu ni msikiti tu ambao wengi wenu mnaona hauna thamani kwani mafundisho na imani ya baadhi yenu inawafunza kuwa ninyi tu ndio mnaoamini mungu wa kweli na wale wanaotumi msikiti ni wajinga.....

Cha pili, ieleweke kuwa ufunguzi wa msikiti huu una ishara kubwa si tu kwa mahusiano ya kijamii ndani ya uganda bali hata katika nchi jirani. Huu ni msikiti ulianza kujengwa na Iddi Amin Muislam ambaye alikuwa na wafuasi wake wengi wakiwemo waislamu wa kabila lake na wabaganda ambao wamekuwa wakiamini kuwa loyalty yao kwa amini ndio iliyowafanya wapate vikwazo vya kielimu, kiuchumi na hata kisiasa kwa miaka mingi baada ya mkristo Museveni wa kutoka magharibi achukue utawala wa nchi yao. Hivyo basi ingawa ufunguzi ulikuwa wa "msikiti tu" kama muonavyo wengi hapa lakini shughuli hiyo ilikuwa na umuhimu wa kipekee katika kujenga umoja na maridhiano ndani ya jamii ya waganda lakini pia hata katika mataifa mengine jirani.

Tanzanianjema
 


Walinzi wa George W waliwakwida wenyeji wao? Walinzi wake wamemkamata nani nchini mwetu?

George W kwa Afrika amekuwa rafiki mzuri. Ni yeye aliyeongeza bajeti ya msaada kwa kontinenti letu kuliko hata huyo kipenzi chetu Bill. George W alipokuwa kwetu lichanganyikana na watu bila matatizo. George W anatusaidia katika vita vyetu dhidi ya Malaria, ugonjwa unaoua kuliko ukimwi. Kwa nini basi tusimkaribishe? Hauwezi kukubaliana na hata rafiki yako katika kila jambo.

FONT]



Kazi kwelikweli........

Hivi ndugu yangu hujui kuwa sio tu watanzania tisa walikamatwa kwa amri ya hawa jamaa lakini hata mfumo mzima wa usalama wa nchi tuliwakabidhi na watu wetu wakaenda likizo....

Tanzanianjema
 
Huyu Gadafi hata kama ana urafiki na sisi ni wa kinafiki tu...wakati wa vita na Idi Amin si alituma majeshi yake kumsaidia Amin,sasa sijui kama alishatuomba msamaha au vipi.
Hawa mabodigadi nao kupigana ni poa tu,maana wanafanya mazoezi sana.Sasa kama wanakosa mtu wa kutishia maisha ya kiongozi wao,si ni bora wafuane wenyewe tu.Maana wengi huwa wanakaa na viongozi wao,mpaka wanastaafu bila ya kasheshe lolote,hata mlipuko wa tyre burst wa kuwashtua kidogo hakuna!
Huku kwetu kuna mabodigadi ukiona wana vitambi wengine,sasa kama issue ndio ya kusukumana,duh!
Kutuma majeshi hakumaanishi zaidi ya utamaduni wa kiafrika,Tz walituma majeshi sehemu nyingi tu na mpaka leo wanatuma,ufahamu kua uswahiba tu ndio unaosababisha,kwani kuvunjika kwa East Africa si kuna fedha hazikurudishwa na magari kibao yalitaifishwa,mbona nchi zilizochukua feza hiyo hazijaombana samahani na urafiki umirudi. Pili tukubali kuwa mabodi gadi na wapambe wa Gadafi wako makini ukilinganisha na wakwetu ambao Raisi anakabidhiwa Cheki feki na kupigwa picha na kufikia hadi picha kuchapishwa hakuna aliezinduka mpaka jamaa wa JF walipositua ndio ukasikia na wao wanapiga makelele.
 
Kawaida ya waarabu ni ufedhuli na ujeuri hiyo ni silka yao, sidhani kama Gadaffi kajenga huo msikiti kwa nia ya kuuendeleza uislamu bali ni katika kuonesha fahari kama ilivyo kawaida ya jamaa zetu hao. kwa sababu kutoa katika misingi ya kiislamu ni kwamba utowe kwa siri na sio kuutangazia umma au ulimwengu wote ukajua kama alivyofanya yeye.

kitu chengine ambacho kinanishangaza kwa hawa watu misaada ambayo wao naona ni bigdeal ni kujenga misikiti tu, wakati kuna mambo mengi wanaweza kusaidia kama kweli wao ni watu wa msaada. kuna waislamu wengi tu masikini hawana uwezo wa hata kusomesha watoto wao, kuna mayatima lakini sijaona misaada katika channel hiyo.
Bora wakijenga misikiti kuliko wakileta kitita cha feza wagaiwe mayatima na masikini ,eti wabongo si tunajuana maana hata wazungu siku hizi wametusitukia ,wanaleta matofali badala ya feza ,kule zenji nasikia Kajima walipojenga bara bara na madaraja simenti walioyoileta ilikuwa spesho yaani ukiiba ukifika nayo nyumbani inageuka jiwe ,jamaa walishindwa kuiiba baada ya kuona kuna kemiko inabidi ziwepo ili uweze kuitumia.
 
Hivi Bush anapokuja tembelea nchi zetu naye ma body guard wake hunyang'anywa silaha na kubakia na hizo pistol 8?..
Nauliza tu nipate kufahamu kama kuna sheria maalum ya kimataifa na Marekani hukiuka.

Bora ungeuliza yule jibwa alieingia na kunusa gari ya Mkapa alipokuja Clinton,naona wengi walikuwa kama wametumbukizwa kwenye gunia lililoloweshwa maji.Na wanastyle ya kuzima mawasiliano ya mji mzima na kufunga bara bara zote hakuna kurudi wala kwenda aliekuwemo hatoki na alieko nje haingii ndani ,si waulizeni wakazi wa Daresalamu pale juzi walipotembelewa na Joji kichaka halafu na kashikashi zake za kukamata watu wa alkaeda , yaani jamaa funga funga tu alafu kamba ile mbaya ,mi hata siamini kama kuna watu walikamatwa kuhusiana na alkaeda zaidi ya madoido ambayo Joji Kichaka ndio dau lake la kusafiria.
 
Kazi kwelikweli........

Hivi ndugu yangu hujui kuwa sio tu watanzania tisa walikamatwa kwa amri ya hawa jamaa lakini hata mfumo mzima wa usalama wa nchi tuliwakabidhi na watu wetu wakaenda likizo....

Tanzanianjema

Najua! Lakini kwani walikamatwa na askari wa George W.? Unataka kutuambia kuwa wakati wa ziara ya George W askari wake na walinzi wake walikuwa wanazunguka kuwakamata watu huko Ifakara? Au ni sisi katika kujipendekeza? Kuna sehemu gani ambako imeonyesha kuwa walinzi wa George W. walikiuka makubaliano ambayo sisi wenyewe tuliingia nao hata kama kwa wengi wetu tuliona ni ukoloni mamboleo? Lakini ndiyo makubaliano tuliyoyafanya, tukayatekeleza na wao hivyo hivyo.

Gaddafi hakufanya hivyo. Amefanya jeuri na kiburi kwa kuangalia wakati walinzi wake wakitwangana mbele ya mwenyeji wake. Kama pangekuwa na makubaliano ya awali haya yote yasingetokea. Kama waganda wangekubali kumwachia usalama wote basi wasingekuwa na sababu ya kuwatilia ngumu. Alionyesha kiburi na hili ndilo ninalolilaani.

 
Libyan leader Colonel Muammar Gaddafi has been involved in a diplomatic incident as he arrived in the Nigerian capital, Abuja, for a summit.

Nigerian officials say Col Gaddafi was accompanied by more than 200 heavily armed Libyan bodyguards.

When security officers refused to allow them to keep their weapons, an argument ensued and Col Gaddafi stormed off.

Only when Nigerian President Olusegun Obasanjo intervened did the bodyguards agree to hand in their weapons.

Foreign ministers from Africa and Latin America have been preparing for the summit which gets under way on Thursday.

The size of Libya's delegation was not a problem, it seems, just the sheer amount of weapons and ammunition they carried.

So Nigerian security refused to let them proceed to the capital.

As arguments raged, the Libyan leader angrily set off on foot, intending to walk some 40km (25 miles) to the capital, before he was persuaded to return to the airport lounge.

Intervention

By sheer coincidence, President Obasanjo was passing through the airport at the same time.

He intervened in person and proposed that the weapons could be allowed through if they were registered first.

But the Nigerians say that was rejected and the Libyan delegation threatened to fly home.

Incensed, the Nigerians said that was fine with them and told the delegation that instead of the original compromise, they could now only carry eight pistols if they wanted to enter Nigeria, like any other diplomatic security detail.

They ordered that the rest of the weaponry had to be put back on the Libyan official jet.

After a stand-off lasting several hours, the Libyans backed down and finally made their way to Nigeria's capital.
 
Hivi Bush anapokuja tembelea nchi zetu naye ma body guard wake hunyang'anywa silaha na kubakia na hizo pistol 8?..
Nauliza tu nipate kufahamu kama kuna sheria maalum ya kimataifa na Marekani hukiuka.
Ona askari wa kimarekani wakiwa juu ya paa la ikulu ya magogoni
765ythgfgy0.jpg
 
.....hivi huyo Shein alikuwa kabeba mkasi wake wa kukatia utepe?? au?
......isije ikawa wamemsukuma baada ya kujisahau na kutaka kukata utepe wakati yeye si mgeni rasmi( maana nasikia imekuwa kama reflex action ya knee jerk of some sort kati yake na tepe...)


.......kukosa kazi za kufanya, ya msikiti tu, tena uloanza kujengwa na dikteta, una draw viongozi wa nchi 11 kati ufunguzi wake?? mie pia ni muislam, lakini hii ni ridiculous!! aibu kwa afrika na aibu kwa tanzania, yaani ile kuthubutu kumtuma makamo wake wa raisi ktk ufunguzi wa msikiti ktk nchi jirani. yaani wataka kusema haya ni matumizi halali ya fweza za walipa kodi!!??? ama kweli gademu, na hivi ndivyo tulivyo...GD Tanzania!.
.
Hahahaaa. Shein mzee wa kutembea na mkasi kwenye koti kwa ajili ya kukata utepe!
 
Back
Top Bottom