Walinzi wa getini ofisi ya Mkuu wa Mkoa Dar es Salaam punguzeni njaa, msijifiche kwenye kichaka cha barakoa

mwandende

JF-Expert Member
Feb 16, 2017
10,518
19,885
Nawasalimia kwa jina la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Tangu kufunguliwa kwa shule za secondary na msingi inchini mwaka huu 2022,,,

Ofisi za afisa elimu mikoa mbali mbali zimekuwa busy Sana ktk kuhudumia wanainchi wanaohitaji uhamisho wa shule kwa watoto wao.

Baada ya wingi huo wa wananchi kujazana ofisi za afisa elimu mkoa,
limeibuka wimbi la walinzi kuwazuia watu kuingia ndani ya ofisi na kuwalazimisha watu kununua barakoa zinazouzwa nje ya ofisi hizo za mkuu wa mkoa:

Ni kama ule usemi wa kufa kufaana ndiyo kinachotendeka pale.

Leo nimekwenda ofisi za mkuu wa mkoa ilala - Dar es salaam na kujionea upuuzi unaofanywa na walinzi wa getini wanalazimisha watu kununuwa barakoa wakati wao wenyewe hawana barakoa.

Lilitokea zogo kubwa hata kupelekea kutaka kushikana mashati na walinzi wale, tena huku wakinitisha kuniweka chini ya ulinzi.

Sababu tu nimehoji kwanini wanizuie kuingia ndani wakati wao pia hawana barakoa.

Hivi hili la kujikinga na ugonjwa wa COVID ni kwa watu wengine tu? Au hata watumishi wa umma?
Kwanini walinzi hawavai barakoa? Lakini mgeni avae barakoa?

Niliwapa maswali magumu jamaa waka panic.

Nadhani pia hii ni aina fulani ya kunyanyasa wanainchi kwa kujificha ktk kichaka cha biashara ya barakoa.

Kwanza hata humo ndani wote hawana barakoa,
au kama wanazo basi wameziweka shingoni au mkononi badala ya kuzivaa usoni.

Natamka pasi na Shaka kwamba huenda walinzi wanahusika na biashara za barakoa zinazouzwa getini pale.
Nasema ni biashara zao sababu hakukuwa na ulazima wa kulazimisha watu kununuwa barakoa kwa nguvu na tena wanakwambiya "nunua pale getini"

Kuna kijamaa nje getini kimeshika barakoa anauza,,
Halafu hizo barakoa, zikishanunuliwa hazivaliwi kwa ufasaha bali watu huziweka mkononi na kupita bila usumbufu.

Sasa unanunua za nn na hazivaliwi?

Pia Hata hizo barakoa zenyewe zinazouzwa hapo getini zina usalama gani?
Maana zinaonekana ni locally kabisa.
tena zina dalili zote za kutengenezwa mitaani.

Wataalam wa afya wanashauri tununuwe barakoa zenye usalama tena pharmacy.

Sasa hizi za mikononi zina usalama gani?

Na ni maajabu sana kwakweli. Mlinzi anazuia watu wasiingie bila barakoa ,,
wakati yeye pamoja na waliomzunguka wote hawana barakoa.

Huu upuuzi ukomeshwe!

Naomba muheshimiwa mkuu wa mkoa Daresalam ,,uwaangalie walinzi hawa kwa jicho la tatu.

Hawa ndy watumishi wachache wanaochafua serikali yetu tukufu kwa njaa zao.
Wanaangalia zaidi biashara kuliko usalama wa afya za wanainchi.

Hata kama watu wanakula kwa urefu wa kamba yao.
Lakini hawapaswi kusumbuwa wanainchi, kwa kujificha ktk kichaka cha kuvaa barakoa.

Walinzi punguzeni njaa.
 
Umeandika gazeti refu lakini ni ujinga mtupu umeandika.

Barakoa ni agizo kwa ofisi zote ni lazima uvae barakoa, kama unaona mlangoni unalanguliwa nunuwa hukohuko mtaani kwako nenda na barakoa yako au shonesha ya kitenge kwa fundi utakuwa unafuwa.

Ni kwa nini wao hawavai barakoa si kazi yako, wao kazi yao ni kuhakikisha wageni wote wana barakoa.

Lets assume wao wamechanja chanjo ndio maana hawavai, lakini mgeni lazima.

Magari ya Polisi mengi ni mabovu, polisi wengine kwenye pikipiki hawavai element, sasa wewe waendee na hoja zako za kiboya hizi ndio utaelewa dunia ilivyo.

Yani kusumbuwa watu JF kwa ajili ya barakoa ya jero? Upumbavu huu.
 
Hata ukichanja unatakiwa kuvaa barakoa
 
Tanzania ujinga bado uko sehemu nyingi mkuu.

Ni kama airport, ukifika pale wanakulazimisha uvae barakoa wakati ukiingia ndani watu hawajavaa barakoa wala nini.

Kwa kua sipendi maneno, nina barakoa moja nayoitumia toka mwaka jana mwanzoni, nikifika pale navaa, baada ya kupita zile scanner machines naitupia mfukoni.

Ni ujinga tu kulazimishana kuvaa mibarakoa.
 
Umeamdika upumbavu kuliko huo wa mleta mada. Umeshindwa kuelewa mantiki ya hoja zake na kumjibu unaishia kujiaibisha.

Mlinzi kaa kimya tu
 
Ksma ni jamaa wa sumajkt basi wale no wapuuzi sana huwa hawajui reasoning huwa kama maroboti

Huwa wanapaniki sana ukiwapiga maswali magumu

Nimeshakutana nao sana na kuzinguana nao

Huwa wanajiona wanajeshi wakati alikuwa servicemen tu huko jeshini wakaonewa huruma wakaletwa huko sumajkt
 
Wanapunguza njaa kaa kuuza barakoa? Hivi umejisikia ulichosema? Unafikiri njaa itaishaje asipojiongeza? Ha ha ha ha ha ha ha.

Hata hivyo ofisi zote za umma unatakiwa kuvaa barakoa, tembea nayo mfukoni ukifika vaa, hutalazimishwa kununua mpya. Ukitoka vua na uendelee na hamsini zako.

Gazeti la nini?
 
Nishasema ufisadi haukwepekiiii Samahani halafu nenda kafuatilie tozo za pale stand ya magufuli mbezi utakuja kujua kwamba kweli hasira ni hasara!! uatchukua hatua mkononi ila kama ni kapuku utafichwa tu.. bora halafu kingine juzi Kuna ndugu yangu amepaki gari kwake tarura wanakuja kumdai parking!!! nilicheka saaana

Sent from my TECNO CC7 using JamiiForums mobile app
 
Hata pia ukienda ofisi ya tra mkoa wa Pwani nao ni hivyo hivyo bila barakoa huingii ndani na cha ajabu pia barakoa hizo wanauza wenyewe walinzi wa Suma JKT na ukiingia ndani hakuna mfanyakazi hata mmoja aliye vaa barakoa
 
Tanzania ujinga bado uko sehemu nyingi mkuu.

Ni kama airport, ukifika pale wanakulazimisha uvae barakoa wakati ukiingia ndani watu hawajavaa barakoa wala nini.

Kwa kua sipendi maneno, nina barakoa moja nayoitumia toka mwaka jana mwanzoni, nikifika pale navaa, baada ya kupita zile scanner machines naitupia mfukoni.

Ni ujinga tu kulazimishana kuvaa mibarakoa.
Msijali sana,soon na barakoa nazo zitapotea na kusahaulika kama sanitizer pamoja na maji tililika naona siku hizi hawaweki tena unakuta matenki matupu hakuna maji!,ni swala la muda tu,yetu macho tu!
 
Back
Top Bottom