Bams
JF-Expert Member
- Oct 19, 2010
- 19,768
- 49,949
Hivi ndivyo kila mzalendo anavyotakiwa kufanya. Walimu ni muhimu sana kuleta mabadiliko nchini na hasa kwa vijana. Hongera sana kwa kazi nzuri mnayoifanya. Na wengine tuliopo maeneo mengine tuna wajibu pia. Nami huku niliko kwa kuwa ni mkuu wa taasisi kila inapowezekana naweka mambo sawa ili watu wajue kuwa hatua ya kwanza ya Tanzanaia kupiga hatua ya maendeleo, ni lazima CCM ikae pembeni. Kila mmoja anajua hilo, kama kuna yeyote anayeipenda CCM hapa, anafanya hivyo kwa kificho. Lakini katika uwazi hatuna hata mmoja wa kuiunga mkono CCM. Wote wamebadilika.
Na ukifika wakati wa uchaguzi lazima nisimamie ukusanyaji wa michango ili kuchangia nguvu zaidi za kuilaza CCM sehemu salama. Suala la kuleta mabadiliko ni jukumu la kila mmoja, siyo Mbowe au Slaa pekee yake. Kila mmoja ajiwekee malengo ya kufikia idadi fulani ya kuwaokoa kifikra wale ambao bado hawajajitambua, ambao macho yao hayaoni, akili hazifanyi kazi, mioyo yao inapiga kwa mapigo ya CCM, hata kama wao ndiyo wapo hoe hae.
Nimefanikiwa kumshawishi mfadhili mkubwa wa CCM, tajiri hasa (Analazimika kuchangia CCM kila wakati ili asiwekewe mizengwe kwenye biashara zake). Amesema atachangia kwa kificho lakini lazima atachangia.