Walimu Watakapoanzisha Kampeni Rasmi Madarasani Kuing'oa CCM | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Walimu Watakapoanzisha Kampeni Rasmi Madarasani Kuing'oa CCM

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by eedoh05, Aug 29, 2012.

 1. e

  eedoh05 JF-Expert Member

  #1
  Aug 29, 2012
  Joined: Apr 20, 2011
  Messages: 633
  Likes Received: 39
  Trophy Points: 45
  Nakumbuka wakati wa wiki ile ya mgomo wa walimu mwezi uliopita; kuna mwalimu aliwaambia viongozi wa serikali aliokuwanao studio za Star TV -Dar es Salaam wakijadili mgomo wa walimu. Mwalimu huyo alisema, kama walimu wangeanzisha kampeni za kuwang'oa CCM madarakani basi hata viongozi wa serikali aliokuwanao pale studio wasingekuwa madarakani. Kwangu mimi nadhani si walimu tu ambao wanaweza kuwa na athari mbaya kwa utawala kama watafanya kampeni hizo bali hata madaktari wanaweza kuchomeka siasa katika taaluma yao.

  Kwa mwendo wa serikali ya CCM wa kulichukulia kila jambo kisiasa limeanza kuchukua sura mbaya. Kwa taratibu siasa zimekuwa sehemu ya maisha ya kila mtu. Kwa sasa si walimu tu wanaoingiza siasa kazini hadi madarasani bali hata kada nyingine pia mathalan, wauguzi, madaktari, wakulima wa pamba, wachimba migodi, wafugaji, viongozi wa dini wanamichezo na wengine wengi.

  Ili kuiondoa serikali iliyopo madarakani na chama chake wafanyakazi wa kada mbalimbali wakiamua kwa kauli moja kwamba wasigome wala kulalamikia mazingira magumu ya kazi na mishahara duni; wanaweza kuanzisha kampeni kabambe kuwatumbukizia au kupaka sumu dhidi ya watawala na serikali yao kwa kila mteja wao. Sumu hiyo inweza kusambaa vibaya na ikaleta athari na tija ya haraka kuondoa matatizo yaliyopo sasa. Walimu wakiongeza kasi ya kampeni hizo kwa wanafunzi kutoka wanavyofanya sasa, matokeo ya kung'oa viongozi wabovu itachukua muda mfupi sana. Nadhani kwa watu waliowahi kuangalia filamu ya "SARAFINA" watakubaliana nami..

  Hivyo, nashauri ili hayo yasitokee ni heri watawala na vyombo vya dola wafike mahala wajue kutenganisha siasa na taaluma. Wakiacha hali iliyopo iendelee kwa kila jambo kuchukuliwa kisiasa basi nchi nzima na watu wa kada zote watakuwa wanasiasa. Na ndio maana sensa inahusishwa na siasa.

  =======
  July 2013:

  SMS hii inasambaa kwa kasi

   
 2. Escobar

  Escobar JF-Expert Member

  #2
  Aug 29, 2012
  Joined: Sep 16, 2011
  Messages: 576
  Likes Received: 217
  Trophy Points: 60
  Smahani mkuu, unaongelea walimu wapi wenye kuweza kusema NO na wakamanisha hivyo? Kama ni hawa wa division 4 ya point 28 na wale wa voda faster hiyo kitu sahau! Hawana option B ndio maana hawawezi kutunisha misuli.
   
 3. Mpatanishi

  Mpatanishi JF-Expert Member

  #3
  Aug 30, 2012
  Joined: Jul 1, 2011
  Messages: 1,709
  Likes Received: 43
  Trophy Points: 145
  Mbona M4C ipo madarasani tayari! Kwa sasa nimewekeza kwa 4m3 na 4m4 mana hawa 2015 wanapiga kura watakua na 18yrs.
  Tunachofanya walimu ni kuwaeleza watoto adui yao ni nani hasa.
  Hata kwenye mgomo walituunga mkono.
  2015 ccm must go.
  Count my words.
   
 4. Bilionea Asigwa

  Bilionea Asigwa JF-Expert Member

  #4
  Aug 30, 2012
  Joined: Sep 21, 2011
  Messages: 12,627
  Likes Received: 9,840
  Trophy Points: 280
  kwa hapa bongo sahau hii kitu......tatizo walimu wengi porojo nyingi mno action NIL
   
 5. MARCKO

  MARCKO JF-Expert Member

  #5
  Aug 30, 2012
  Joined: Jun 10, 2011
  Messages: 2,265
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  Sisi walimu >CCM Out, tunafanyia CDM arakati za kuingia madarakani, maana mkuu wa wilaya na mkoa pinda alisema hamna shida wakifanya kazi ya chama ili CCM itawale milele. wakimwaga mboga, walimu ugali twautia mchanga.
   
 6. t

  thatha JF-Expert Member

  #6
  Aug 30, 2012
  Joined: Apr 29, 2011
  Messages: 15,234
  Likes Received: 179
  Trophy Points: 160
  escobar acha dharau kwa walimu wetu, hao ndiyo wamekufikisha hapo!
   
 7. babalao 2

  babalao 2 JF-Expert Member

  #7
  Aug 30, 2012
  Joined: Apr 6, 2012
  Messages: 4,218
  Likes Received: 1,270
  Trophy Points: 280
  Kwa elimu hii watatoka tu[​IMG]
   
 8. m

  mnduoeye Senior Member

  #8
  Aug 30, 2012
  Joined: Jun 30, 2012
  Messages: 166
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  eedoh05 Hilo usemalo sasa si linangojewa lilishaanza laini watawala watasema ni siasa hizo .Ukweli ccm wamekuwa kama comic Ali wa libya imeziba masikio yake na pamba za wapi sijui.Hawataamini yatakayotokea 2015 kwa ajili ya kudharau kila kitu .Lakini hata hivyo ni vyema tupate mabadiliko ya kweli tusimamaie raslimali zetu zinazoporwa na wachache ndani ya ccm.Wameleeshwa na madaraka na raslimali zetu hawatusikilizi tena wala kuwajali wanyonge waliowapa hayo MAMLAKA
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 9. Muke Ya Muzungu

  Muke Ya Muzungu JF-Expert Member

  #9
  Jul 17, 2013
  Joined: Jun 17, 2009
  Messages: 3,451
  Likes Received: 30
  Trophy Points: 0
  Nimekuwa mwana CCM maisha yangu yote. Nimeipigia serikali ya CCM kura siku zote, lakini baada ya hii patashika, inanibidi nijitafakari.

  Baada ya kufika nyumbani mithili ya saa mbili usiku jana 16/07/2013, mwanangu anayesoma darasa 5 hapa jijini Dar, alikuwa na shauku kubwa sana ya kuongea na mimi. Kitu ambacho hakikuwa kawaida yake. Baada ya kuvua nguo za kazi, aliniita sebuleni na kuniuliza, baba huko tayari kuongea na mimi? Nikamuuliza kuna nini, alinijibu namaongezi na wewe. Kwa wasiwasi wasi mkubwa nilitii ombi la binti huyu.
  Mwanangu aliniuliza maswali mengi yaliyonitoa machozi. Maswali yake yalikuwa kama yafuatayo

  1. Baba, kwanini hatupati chakula cha kutosha?
  2. Kwa nini hauna gari wakati unaowapigia kura wana magari ya kifahari?
  3. Kwa nini kaka Issa alifeli form four na sasa hana kazi, wakati watoto wa mafisadi waliofeli wanafanya kazi benki kuu?
  4. Kwa nini hospitalini lazima uonge ndio tutibiwe?
  5. Kwa nini unapewa fulana na sahani ya pilau kisha kuuza kura yako?
  6. Tanzania haijawahi kuwa na udini, iweje leo tugawanywe kwa udini?
  7. Baba, duka lililokuwa la mama kariakoo amepewa mchina, je wachina watachua hadi nyumba tunayokaa?
  8. Kwa nini serikali haitaki kuwalipa walimu wetu vizuri?
  9. Kwa nini polisi wanawaua raia badala ya kuwalinda?
  10. Baba serikali ya CCM imekusaidia nini?
  11. Kwa nini hauwazomei mafisadi?
  12. Wamefundishwa kwamba CCM ni Chama Cha Magaidi wakiongozwa na Mwigulu Nchemba
  Huku akiwa na daftari lake na kalamu mkononi, akiyasubiria majibu yangu? Nilishikwa na ghanzi. Nilishindwa kumjibu. Nilimuuliza kwa upole, haya mambo umejifunza wapi?

  Bila woga alinijibu, kwamba wamefundishwa shuleni jinsi ya kulikomboa Tanzania kutoka mikononi mwa mafisadi. Wamefundishwa kuwazomea mafisadi wanaopita mabarabarani na kesho lazima warudi na majibu shuleni
   
 10. palalisote

  palalisote JF-Expert Member

  #10
  Jul 17, 2013
  Joined: Aug 4, 2010
  Messages: 8,352
  Likes Received: 37
  Trophy Points: 0
  Asante sana walimu
   
 11. Gefu

  Gefu JF-Expert Member

  #11
  Jul 17, 2013
  Joined: Nov 30, 2010
  Messages: 6,962
  Likes Received: 257
  Trophy Points: 180
  ...na bado,mpaka wazazi watafundishwa,ngoja tupeleke intake kama tatu za kutoka vyuoni huko vijijini....
   
 12. Muke Ya Muzungu

  Muke Ya Muzungu JF-Expert Member

  #12
  Jul 17, 2013
  Joined: Jun 17, 2009
  Messages: 3,451
  Likes Received: 30
  Trophy Points: 0
  CCM mwaka huu watakoma
   
 13. d

  duchi JF-Expert Member

  #13
  Jul 17, 2013
  Joined: Oct 22, 2012
  Messages: 1,766
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  we unashangaa mashuleni ? hao wamepenya mpaka kwenye nyumba za ibada sumu inamwagwa
   
 14. Mahesabu

  Mahesabu JF-Expert Member

  #14
  Jul 17, 2013
  Joined: Jan 27, 2008
  Messages: 5,043
  Likes Received: 666
  Trophy Points: 280
  misri....egypt....hosni....mosni .....AND NOW?
   
 15. Lukolo

  Lukolo JF-Expert Member

  #15
  Jul 17, 2013
  Joined: Dec 2, 2009
  Messages: 5,137
  Likes Received: 76
  Trophy Points: 145
  Kwa walimu hawa ambao wanaomba nyongeza ya mshahara mnawapeleka polisi, kwa hakika mtaisoma namba. Ni bahati tu kwamba hawa watoto hawapigi kura. Lakini hii spirit wanayokua nayo itakuwa chachu kubwa ya mabadiliko huko mbeleni.
   
 16. F

  Fitinamwiko JF-Expert Member

  #16
  Jul 17, 2013
  Joined: Aug 13, 2012
  Messages: 4,810
  Likes Received: 255
  Trophy Points: 180
  Arusha, watoto walisema wamepigwa risasa na Police, Viongozi wanasema CDM. Je unategemea hawa watoto kuwaheshimu viongozi waongo? Viongozi wanajidhalalisha wenyewe kwa kauli zao kama ile kauli ya Pinda
   
 17. Lunyungu

  Lunyungu JF-Expert Member

  #17
  Jul 17, 2013
  Joined: Aug 7, 2006
  Messages: 8,836
  Likes Received: 75
  Trophy Points: 145
  Wawapige tu na muda wote na hasa ikifika nyakati za uchaguzi then waone yale ya Arusha kwa mara nyingine
   
 18. Nyasirori

  Nyasirori Senior Member

  #18
  Jul 17, 2013
  Joined: May 3, 2009
  Messages: 183
  Likes Received: 80
  Trophy Points: 45
  Niliwahi kuhudhuria mafunzo ya kikazi kwenye Chuo kimoja huko Nyanda za juu kusini, ambapo mafunzo hayo yalikuwa yanatolewa na wakufunzi wachuo hicho. Wakufunzi hawa kila anayeingia, anafundisha na baadae kuna sehemu ya story kama kawaida. Wanayoongea,kuponda na kulalamika juu ya serkali, binafsi yalikuwa mpaka yananifanya nisipende story zile kwa machungu. Sasa nikawa najiuliza hawa kama haya wanayaongea hata kwa wanafunzi wao madarasani, nini hatima ya ya taifa hili.
   
 19. Ndibalema

  Ndibalema JF-Expert Member

  #19
  Jul 17, 2013
  Joined: Apr 26, 2008
  Messages: 10,916
  Likes Received: 131
  Trophy Points: 160
  shukuru Mungu mtoto wako hawajamjua maana ungepewa taarifa ukamfate mabwepande.
   
 20. Lizaboni

  Lizaboni JF-Expert Member

  #20
  Jul 17, 2013
  Joined: Feb 21, 2013
  Messages: 33,692
  Likes Received: 13,632
  Trophy Points: 280
  kwa hiyo elimu wanayotoa walimu, wanafunzi wakipata zero chadema msiandamane maana leo thread hii mnaifurahia sana. pia mfute zile kauli zenu za kuwataka watendaji wa wizara ya elimu wajiuzuru
   
Loading...