Keen
JF-Expert Member
- Sep 27, 2007
- 617
- 172
nimekuwa mwana ccm maisha yangu yote. Nimeipigia serikali ya ccm kura siku zote, lakini baada ya hii patashika, inanibidi nijitafakari.
Baada ya kufika nyumbani mithili ya saa mbili usiku jana 16/07/2013, mwanangu anayesoma darasa 5 hapa jijini dar, alikuwa na shauku kubwa sana ya kuongea na mimi. Kitu ambacho hakikuwa kawaida yake. Baada ya kuvua nguo za kazi, aliniita sebuleni na kuniuliza, baba huko tayari kuongea na mimi? Nikamuuliza kuna nini, alinijibu namaongezi na wewe. Kwa wasiwasi wasi mkubwa nilitii ombi la binti huyu.
Mwanangu aliniuliza maswali mengi yaliyonitoa machozi. Maswali yake yalikuwa kama yafuatayo
huku akiwa na daftari lake na kalamu mkononi, akiyasubiria majibu yangu? Nilishikwa na ghanzi. Nilishindwa kumjibu. Nilimuuliza kwa upole, haya mambo umejifunza wapi?
- baba, kwanini hatupati chakula cha kutosha?
- kwa nini hauna gari wakati unaowapigia kura wana magari ya kifahari?
- kwa nini kaka issa alifeli form four na sasa hana kazi, wakati watoto wa mafisadi waliofeli wanafanya kazi benki kuu?
- kwa nini hospitalini lazima uonge ndio tutibiwe?
- kwa nini unapewa fulana na sahani ya pilau kisha kuuza kura yako?
- tanzania haijawahi kuwa na udini, iweje leo tugawanywe kwa udini?
- baba, duka lililokuwa la mama kariakoo amepewa mchina, je wachina watachua hadi nyumba tunayokaa?
- kwa nini serikali haitaki kuwalipa walimu wetu vizuri?
- kwa nini polisi wanawaua raia badala ya kuwalinda?
- baba serikali ya ccm imekusaidia nini?
- kwa nini hauwazomei mafisadi?
- wamefundishwa kwamba ccm ni chama cha magaidi wakiongozwa na mwigulu nchemba
Bila woga alinijibu, kwamba wamefundishwa shuleni jinsi ya kulikomboa tanzania kutoka mikononi mwa mafisadi. Wamefundishwa kuwazomea mafisadi wanaopita mabarabarani na kesho lazima warudi na majibu shuleni
anasoma shule gani mwanao?