Wadau,
Ahsanteni kwa kuupitia Uzi huu, na shukran za pekee kwa wote walioweza ku-apply kupitia email nliyowatumia.
Kifupi, tumepata applicants 14, tulipanga kuwafanyia 6 interview Leo hii, wengine wanne kesho na wanne wa mwisho Alhamis.
Leo tumefanikiwa kuwafanyia watatu, mmoja tumekosa mawasiliano nae kwa sababu zilizo nje ya uwezo wetu na wawili walikuwa hawapatikani hewani. Bahati mbaya ndio wameshakosa usaili, labda kama tutapata muda ijumaa tunaweza watafuta.
Wale wote waliotuma maombi nawasihi wawe wanapatikana hewani muda wote.
Muda wa kutuma maombi umekwisha na nawashkuru sana wadau.
Ahsanteni,
Relief Mirzska.