Walimu kuchukulia mishahara dirishani mwezi january.

Janualy ni National pay day kwa watumishi wote wa serikali na sio walimu peke yao, naunga mkono kwa 100% zoezi hili. lengo ni kubaini mishahara hewa kwa watumishi wote wa serikali.

Toka wameanza kufanya hivyo wameshawagundua wangapi? Na wamewafanya nini?
Na mbona wameshindwa kulikomesha hadi leo?
Je, kwa akili yako unadhani hyo hela ya wafanyakazi hewa inaliwa na nani siku zote?
Usumbufu tu, wezi wa hzo hela hewa mbona wanajulikana.
Hata wafanye nini, badi wataendelea kuwepo na pengine wataaongezeka.
The whole Tanzania system is corrupt.
 
Baba Ubaya wapo watumishi hewa wengi sana, lakini hiyo haizuii kufanya mambo mengine kama uliyosema mkuu.
Hakuna jipya story za kila siku zisizo na tija!
Waanze kuhakiki mikataba ya madini, mikataba ya makampuni mbalimbali kama IPTL, SONGAS ndo waje kwenye hili!
 
Idea nzuri sana kwa sisi vigogo kupata fursa ya kujichagulia nyumba ndogo
 
Nataka wanaJF mtambue kuwa uhakiki huu unahusu sekta zote za umma. Kwa taarifa nilizo nazo ni kwamba watumishi watapewa HUNDI baada ya mtumishi kuwasilisha (yeye mwenyewe na si kutuma mtu) vitu vifuatavyo:-
I. Kitambulisho cha kazi chenye picha.
II. Salary slip za hivi karibuni.

Kadhalika watumishi waliopo masomoni na wagonjwa wa muda muda mrefu wapewe taarifa ili wawepo siku hiyo. Ambaye hatakuwepo atahesabika kuwa ni mtumishi hewa na hundi yake itarudishwa hazina na yeye kufutwa.

Sasa hiyo ni akili kweli?
Hvi walioko masomoni tanzania hii na waliopo in service ni wangapi ndugu yangu?
Woote wasambaratike vyuoni warudi makazini kuhakikiwa, na huo mtaala huko chuoni inakuwaje ikotokea robo au nusu ya wanachuo ni in service? Waza mtu wa Tabora yuko chuo tanga, arudi kuhakikiwa, gharama hzo zinalipwa na nani?
Kwa nini mtumishi abebeshwe mzigo kwa uzembe wa mwajiri. Alafu eti asipokuwepo atahezabika mfanyakazi hewa. Basi safari hii watafukuza wengi. Na km mkataba utamruhusu mwajiru kufanya hvyo. Na kumbuka alie chuoni ana release letter inayomruhusu kuwa chuoni mda huu kisheria.HUU NI UPUMBAVU USIOMITHILIKA. NONSENS.
Ngoja tuone.
 
Toka wameanza kufanya hivyo wameshawagundua wangapi? Na wamewafanya nini?
Na mbona wameshindwa kulikomesha hadi leo?
Je, kwa akili yako unadhani hyo hela ya wafanyakazi hewa inaliwa na nani siku zote?
Usumbufu tu, wezi wa hzo hela hewa mbona wanajulikana.
Hata wafanye nini, badi wataendelea kuwepo na pengine wataaongezeka.
The whole Tanzania system is corrupt.

Mimi sio kiongozi wa chama cha kisiasa kuchallenge kila kitu, kwangu mimi hili ni zoezi sahihi, na niko pamoja na serikali kwenye hili. Nukta.
 
Mimi sio kiongozi wa chama cha kisiasa kuchallenge kila kitu, kwangu mimi hili ni zoezi sahihi, na niko pamoja na serikali kwenye hili. Nukta.

Ngoja tusubiri, tuone how sahihi will be. I mean efficiency and consistency plus accountability ya hao watakaolisimamia
 
Janualy ni National pay day kwa watumishi wote wa serikali na sio walimu peke yao, naunga mkono kwa 100% zoezi hili. lengo ni kubaini mishahara hewa kwa watumishi wote wa serikali.

ahsante kwa taarifa mkuu, mhhh sipate picha hiyo foleni
 
yani njia ya kuhakiki walimu hewa ni kulipia dirishani??? Kweli akili za kawambwa hazichanganyiki kabisa na akili za dilunga.

Hii ndo njia ya kutafuna mihela sasa. Ukata huu wa january, wazee wa kazi watawaacha wakizibeba hizo hela kwenda nazo halmashauri? Na wilaya zisizo na bank kama makambako inakuaje!

Cash security is very expensive, zoezi hili linaweza kugharim pesa nyingi zaidi
 
Mimi sio kiongozi wa chama cha kisiasa kuchallenge kila kitu, kwangu mimi hili ni zoezi sahihi, na niko pamoja na serikali kwenye hili. Nukta.

kaka zoezi hili limekaa kisanii zaidi. Si ajabu ukasikia hundi zitakazotolewa zitakuwa hazina fedha benki. Serikali ya Kikwete imefilisika!haina fedha. Hizi zote ni mbinu za serikali mufsili kubuy time ili kustage usanii zaidi. Hakuna uhakiki hapo!
 
Nataka wanaJF mtambue kuwa uhakiki huu unahusu sekta zote za umma. Kwa taarifa nilizo nazo ni kwamba watumishi watapewa HUNDI baada ya mtumishi kuwasilisha (yeye mwenyewe na si kutuma mtu) vitu vifuatavyo:-
I. Kitambulisho cha kazi chenye picha.
II. Salary slip za hivi karibuni.

Kadhalika watumishi waliopo masomoni na wagonjwa wa muda muda mrefu wapewe taarifa ili wawepo siku hiyo. Ambaye hatakuwepo atahesabika kuwa ni mtumishi hewa na hundi yake itarudishwa hazina na yeye kufutwa.
ahsante kwa taarifa sahihi mkuu, ngoja nivute vute kidogo hadi tarehe 20 ndio nielekee huko
 
kaka zoezi hili limekaa kisanii zaidi. Si ajabu ukasikia hundi zitakazotolewa zitakuwa hazina fedha benki. Serikali ya Kikwete imefilisika!haina fedha. Hizi zote ni mbinu za serikali mufsili kubuy time ili kustage usanii zaidi. Hakuna uhakiki hapo!

"Mtaka cha uvunguni, ...........", Sirikali ikamwangukie Daudi Kameruni, ili atoe msaada wa kifedha.
 
mi nashindwa kuelewa hawa jamaa wanatupeleka wapi? mkurugenzi anakazi gani? kisa eti wanahakiki waliopo kazini why?? je na wale waliopo masomoni itakueje? tubadilike hii ni 2012 so we have to be care!!!!!
 
Hilo zoezi lilifanyika katika vyuo vya ualimu lakini lilikua la kipuuzi. Wakufunzi hawakupewa check za mishahara yao kama ilivyodaiwa hapo awali.
 
1 Reactions
Reply
Back
Top Bottom