Walimu karibu wote uwezo mdogo

Walimu karibu wote uwezo mdogo

Sio kweli naongea jambo kwa fact udsm education watu wenye three wapo wengi sana na rafiki zangu waliofeli kipindi hicho walisoma pale...ili uweze kuingia DUCE au chuo chochote ualimu kwa vyuo vikubwa kama UDSM, DUCE, MUCE n.k unatakiwa uwe na point kuanzia 5 sasa point tano ni divion ngapi??? Kama S=0.5, E=1, D=2, C=3, B=4, A=5 hivyo point tano maana yake ni D D E ambazo ni point 5 ila ni divion Three point 13...mpaka hapo kuna swali ndugu?!
Wewe ndio kilaza kweli sasa mtu aliyefeli atachagiliwaje kujiunga chuo
 
Nyie kaeni hivyo hivyo mnadis uwalimu ila kaeni mkijua watu wengi wanaomiliki vitega uchumi vidogo vidogo mjini vyeye faida kubwa ambavyo mnavizarau kwa hapa mijini ni walimu

Mabosi takriban asilimia 70 hapa tz ambao ni wakuu wavitengo mbali mbali hapa mjini ni watoto wa walimu

Shule kubwa kubwa nzuri zenye elimu Bora na walimu bora asilimia kubwa watoto wanosoma hapo ni watoto wa walimu acha zile shule zenye mbwebwe za ada mnazopeleka watoto wenu kwa sifa unalipia mwanao ada nyingi wakati ubora hakuna zaidi ya kuwafundisha watoto englishi kozi

Sasa utapima je mwalimu ni Bora ama nini maana Nyie si mnamini kazi nzuri ni ile itakufanya ukae bar kila week end
 
kuna mazingira mengi yanachangia mtu kufeli mtihani hasa ktk elimu ya tanzania,na kwa kufeli huko hakumanishi mtu ana uwezo mdogo.
na kwa upande wa nchi za afrika uwezo wa watu walio wengi hulingana ndo maana toka miaka na miaka hutujagundua chochote chini ya jua
 
Nimeweka hapo awali ukifundishwa kupika haimainishi aliyekufundisha ataendelea kuwa zaidi yako, juhudi zako ndizo humfanya mtu ampite...mwalimu aliyenifundisha uwezo wake ndio uliishia pale ila kwa juhudi zangu nikampita...kwahiyo kama alimaliza form four akapiga four akapelekwa ualimu kisha akaja kufundisha shule ya msingi, mie mwanafunzi wake nikasonga mpaka chuo kikuu bado utasema mwalimu ni bright?! Asilimia kubwa ya waalimu uwezo upstairs ni mdogo
Na kingine mie sikusoma ualimu Bali nilisoma PSPA (Political Science and Public Administration)
Ulisoma kombi gani?
 
Mgaya yupo wapi?, Mwantumu mahiza nakumbuka amewahi kutumia pointi yako ya kwanza mwaka juzi kama sijakosea akiwa Tanga. Kauli ikaleta mtafaruko sana kila kona ya nchi, ha ha haaa! Chamsingi Uzima tu!
 
Habari wanajamvi?

Ashakum sio matusi ila leo nimeamua kuleta mada hii baada ya kufanyia utafiti binafsi kwa muda hivi.Kwanza nilianza kuambiwa na rafiki yangu enzi hizo 2012 pale UDBS kwamba asilimia kubwa kama sio wote waalimu uwezo wao ni mdogo upstairs nikakataa akanitaka nifanye utafiti binafsi.

- Walimu wengi kama sio wote hawakupenda kuwa waalimu ila ufaulu wao ndio ulipelekea wakose option na kujikuta kwa shingo upande wanadumbukia kwenye fani ya ualimu bila kupenda.

-Asilimia kubwa ya walimu hawakupenda kwenda ualimu ila ukiachilia mbali ufaulu kuwa hafifu pia urahisi wa kuajiriwa, hii inatokana na ajira kuwa ngumu hivyo wengi kukimbilia ualimu ili kutatua matatizo yao ya ajira.

-Uchumi mbovu umepelekea wengi kuishia kuwa waalimu, hapa nina maana zile familia ambazo hazina uwezo wa kumlipia mwanafunzi kusoma kitu anachokipenda hivyo kujikuta akisoma ualimu ili apate ufadhili wa serikali.

Naomba nisieleweke vibaya ila jaribu kufuatilia kwa umakini uje unaimbie mwanafunzi aliyepata division one nzuri kabisa akawa mwalimu, asilimia kubwa ya waalimu ni waliosoma arts au biashara kwakuwa wengi matokeo yao hayakuridhisha hatimaye option pekee ikawa ualimu.

Waalimu wengi wa science walifeli hapa naomba uniletee mwalimu ambaye ama alisoma PCM, PCB, PGM n.k akapata divion one au two akaenda kusoma ualimu? Wanaokuwa waalimu wengi huangukia kwenye point ya ufaulu mbovu darasani na ni wachache sana huangukia kuwa waalimu sababu ya uchumi wa familia ila wengi saaana walifeli.

Hata kama walijiendeleza na kuwa na masters still ukirudi nyuma utakuwa wengi walifeli, ndio maana nikasema asilimia kubwa kama sio wote uwezo wao ni mdogo.
Mara ulikuwa UDBS mara PSPA niliwahi kubishana na mtu humu mimi nikiwa na Masters kumbe yeye ni Form five,una chuki na walimu wewe
 
Maelezo ya mtoa mada yanaonyesha hajielewi na anachuki na walimu
064cf541789ae2ddb846b863808c7aaa.jpg
8f29930c92cc9ce6d7673379045d7ce1.jpg
 
Mara ulikuwa UDBS mara PSPA niliwahi kubishana na mtu humu mimi nikiwa na Masters kumbe yeye ni Form five,una chuki na walimu wewe
Siamini kama ulisoma masters ukashindwa kuelewa mada ndogo tu hapo Ndugu, rejea kusoma upya nimesema "Niliwahi kuambiwa na rafiki yangu wa UDBS mwaka 2012" ila Mimi nimesoma PSPA.... Kweli Elimu ya Tanzania ipo kwenye makaratasi, unadai ulikuwa wasoma masters ila ukashindwa kung'amua kitu kidogo hivyo???
 
Wewe ndio kilaza kweli sasa mtu aliyefeli atachagiliwaje kujiunga chuo
Inategemea ufaulu kwako unautambua vipi, kwangu kwa O'level aliyepiga four kafeli na A'level aliyepiga three kafeli...hivyo Nadhani nimekujibu....
 
Hahahahaaa unajipooza bure Ndugu...sijaanza Leo, nimemaliza 2013 na ninachokiongea nina ushahidi nacho asilimia kubwa ya waalimu wanaangukia vipengele vitatu ila kikubwa ikiwa ni matokeo mabovu
Idara gani ina watu wenye ufaulu mzuri kama umebeza walimu.
 
Habari wanajamvi?

Ashakum sio matusi ila leo nimeamua kuleta mada hii baada ya kufanyia utafiti binafsi kwa muda hivi.Kwanza nilianza kuambiwa na rafiki yangu enzi hizo 2012 pale UDBS kwamba asilimia kubwa kama sio wote waalimu uwezo wao ni mdogo upstairs nikakataa akanitaka nifanye utafiti binafsi.

- Walimu wengi kama sio wote hawakupenda kuwa waalimu ila ufaulu wao ndio ulipelekea wakose option na kujikuta kwa shingo upande wanadumbukia kwenye fani ya ualimu bila kupenda.

-Asilimia kubwa ya walimu hawakupenda kwenda ualimu ila ukiachilia mbali ufaulu kuwa hafifu pia urahisi wa kuajiriwa, hii inatokana na ajira kuwa ngumu hivyo wengi kukimbilia ualimu ili kutatua matatizo yao ya ajira.

-Uchumi mbovu umepelekea wengi kuishia kuwa waalimu, hapa nina maana zile familia ambazo hazina uwezo wa kumlipia mwanafunzi kusoma kitu anachokipenda hivyo kujikuta akisoma ualimu ili apate ufadhili wa serikali.

Naomba nisieleweke vibaya ila jaribu kufuatilia kwa umakini uje unaimbie mwanafunzi aliyepata division one nzuri kabisa akawa mwalimu, asilimia kubwa ya waalimu ni waliosoma arts au biashara kwakuwa wengi matokeo yao hayakuridhisha hatimaye option pekee ikawa ualimu.

Waalimu wengi wa science walifeli hapa naomba uniletee mwalimu ambaye ama alisoma PCM, PCB, PGM n.k akapata divion one au two akaenda kusoma ualimu? Wanaokuwa waalimu wengi huangukia kwenye point ya ufaulu mbovu darasani na ni wachache sana huangukia kuwa waalimu sababu ya uchumi wa familia ila wengi saaana walifeli.

Hata kama walijiendeleza na kuwa na masters still ukirudi nyuma utakuwa wengi walifeli, ndio maana nikasema asilimia kubwa kama sio wote uwezo wao ni mdogo.
Wewe hata sijui kama umemaliza darasa la 7, kuna mtu ambaye anaenda chuo kikuu bila kufaulu majabu ya musa haya.
 
Wewe hata sijui kama umemaliza darasa la 7, kuna mtu ambaye anaenda chuo kikuu bila kufaulu majabu ya musa haya.
Hahahaha wewe kweli mbulula wa mwisho, ningekuwa sijamaliza la saba ningebeza walionizidi??? Daima mtu hubeza aliyempita na sio aliyepitwa nae... rudia kusoma mada utaelewa hivyo Nadhani wewe ndio hujagusa kabisa na kukurupuka kwako kijinga....
 
Mkuu wewe ndo nikuulize umesoma kweli..??? Nikuulize tena umesoma kweli??? Kwa taarifa yako hata division 3 wanasoma law na nina my friend alipata division 3 kasoma law pale tena chuo kikubwa mzumbe na nime screenshot min.entry qualification kwa law pale mzumbe ili uone.........alafu tunajua kutokana na vigezo serikali yetu iliyoviweka mtu inatakiwa awe na elimu ngazi ya cheti ili akafundishe level ya primary sasa wewe ndo uniambie katika ngazi ya cheti ni kada gani inayochukua ufaulu mkubwa kuliko kada nyingine zote???? And nimesema kuna mtu amesoma pcb ana division 2 anasoma science education udsm na kuna mtu ana 3 pcb anasoma udaktari or course nyingine ya afya kampala university or st john or imtu or hubert kairuki..sasa wewe ndo uniambie hapo nani mwenye uwezo na ufaulu mdogo and ukija mtaani kwa watu wasiojua ni nani kati ya huyo daktari na mwalimu ataonekana mwenye ufaulu mkubwa.......and niambie sasa wewe ni kada gani ambayo wewe unadhani inachukua ufaulu mkubwa ngazi ya degree na hiyo kada mtu mwenye 3 hawezi soma na kuigusa kabisa...nijibu hayo maswali yangu kwanza.

Mzee Msasambegu, kama utakua umenielewa mimi naongelea vyuo vikuu ambavyo hata wewe nina uhakika unavijua. Sasa ukinitajia hivyo Kampala University, St john, IMTU, Hubert Kairuki sijui St Joseph na vingine vya namna hiyo hapo nadhani utakua hujanielewa.

Mimi nimesoma kipindi vyuo vikuu viko 2 tu, University of Dar es salaam na Sokoine University of Agriculture, hata Muhimbili ilikua ni Faculty tu iliyokua chini ya UDSM, hiyo Mzumbe ilikua ni Institute hakikua chuo kikuu, sasa hivi vingine ukiona vinachukua hata wa Division 3 usifikiri hilo liko kwa vyuo vyote. Hata shule za secondary tu huwezi kuniambia mwanafunzi anayeingia kidato cha kwanza shule kama St. Francis au Marian girls/boys atakua na uwezo kama yule wa shule ya Anna Mkapa secondary school au Frederick Sumaye secondary school na shule za aina hiyo.

Mfano kama hicho St Joseph ni juzi tu tumesikia mambo yake ya kufutwa baadhi ya campus zake. Entry point zinazoonyeshwa kwenye makaratasi huwa si kigezo cha kuchukuliwa, kikubwa hapo huwa ni competition iliyopo.

Hayo mambo ya at least two principals na vitu kama hivyo si kwamba watu 20,000 wakipata hivyo vi-principals wote watachuliwa tu. Hivi mtu wa Division 3 anaweza kuchukuliwa Computor Science au Computor Engineering au any Engineering? ukiachana na hizo unazoziita min entry, hizo ni kukuonesha tu kwamba angalau mtu wa points hizo anaweza hata akajaza hiyo kozi lakini si lazima achaguliwe. Mkuu kama kweli umepita katika vyuo vikuu vya uhakika mbona hili lipo wazi kabisa? Usibaki kuangalia hizo entry points.

Mwisho kabisa, hizo "or or or" na "and and and" unazozitumia zinakuonesha level yako na hata hilo jina lako la Mzee nani sijui linakua halina maana tena.
 
Habari wanajamvi,
Narudi tena kwa ajili ya mada hii ya Elimu kwani niliweka mada ihusuyo waalimu kuwa na uelewa mdogo watu wakanishambulia ila ukweli unabaki pale pale.

Niende kwenye mada, binafsi nimesoma miaka ya nyuma kidogo ingawa sio mbali sana ila kama miaka kumi iliyopita ila miaka inavyozidi kusonga ndio Tanzania inazidi kuzalisha wasomi vilaza. Nikiangalia miaka ya nyuma nikisoma hakukuwa na shule za kata hivyo shule za serikali zilikuwa chache na za kugombania ninashukuru Mungu nilikuwa miongoni mwa wachache waliogombania shule za serikali na kufaulu na kusonga mbele mpaka chuo. Lengo langu sio kukashifu wale waliofeli la hasha msininukuu vibaya ila ninajikita kwenye mfumo mbovu wa elimu yetu ya Tanzania.

Miaka ya nyuma mwanafunzi alikuwa akipata four hata yenye credit mbili basi alikuwa akirudia mitihani na kuitafuta credit ya kumuwezesha kusonga mbele..sikuwahi kusikia ambaye alikimbilia kusoma certificate, hapa naongea kwakuwa wote niliowajua walirudia mitihani na kulikuwa na centers nyingi za watu wanaorisit tofaut na sasa wanaorisit ni wale waliopiga sifuri kabisa au four mbaya kabisa.

Elimu imerahisishwa kiasi kwamba mwanafunzi aliyepiga hata four ya 32 na D zake 3 anakimbilia kusoma certificate na sio kurisit. Kuna ujuzi mzuri sana kwa waliofika form six tofauti na failures waliokimbilia certificate, Elimu haina dhamani sababu ya vilaza hawa (mtanisamehe kwa kauli hii).

Nadhani kuna haja ya kufuta certificate katika vyuo vyote na kufanya wanafunzi wapate wasaha wa kujituma kama zamani, siku hizi imekuwa kawaida mtoto kapiga four yupo mtaani hana hata wasiwasi wala hajutii kufeli kwake kwa kigezo anaenda kusoma chuo certificate. Ingeondolewa certificate na kubaki na diploma tu ambapo wale wanaomaliza form six ambao hawajafikia viwango vya degree ndio wakasome diploma na kwa namna hiyo Elimu yetu ingeleta tija.

Failure hawa ndio baada ya kumaliza chuo hawana lolote kichwani wanaishia kumwaga lawama serikalini kwa kukosa ajira ila ingekuwa kama zamani basi mwanafunzi anayemaliza chuo degree kwanza anaheshimika na ubongo unafanya kazi vilivyo.

Vilaza wengi tulio nao mitaani wengi waliunga unga na kufikia degree na kwakuwa kwao Elimu ni rahisi na inanunulika tu ndio wameishia lawamani kwa serikali.

Hivyo binafsi sioni umuhimu wa Elimu bure mpaka kidato cha nne iwapo bado tunazidi kuzalisha vilaza wasio na mission wala vision... Rejea Elimu ya zamani utakubaliana na Mimi nikisemacho.

Nakumbuka kuna Ndugu mmoja miaka ile alirisit mara tano kutafuta credit tatu ili asonge mbele lakini matokeo yake ya awali hayakuwa mabaya alipata four ya 30 jambo ambalo ingekuwa leo asingejisumbua kurisit bali angeingia certificate moja kwa moja.

Tunaweza kujihesabia kwamba wasomi Tanzania wamekuwa wengi kwa kigezo cha walio na degree ila uhalisia wengi wao ni vilaza kabisa. Kuna haja ya mtaala wetu wa Elimu kufanyiwa marekebisho upya la sivyo kelele hizi hazitaisha kamwe. Wizara ya Elimu kwa kushirikiana na mashirika ya Elimu yana haja ya kufanyia marekebisho ama kupandisha points za certificate na kuwabana wanaoingia huko au kuondoa kabisa certificate, haiwezekani kilaza mwenye D mbili akaenda chuo kisha baadae anasimama na kusema nina degree ilihali hamna kitu chochote kichwani.

Ni maoni yangu kama mtanzania ambaye sipendezwi na mtaala mbovu wa Elimu yetu ya Tanzania..
Asanteni kwa kusoma.

Kama bado kuna mtu atakua hajakuelewa hata hapa, basi huyo ana lake. Mimi binafsi naipata hoja yako. Samahani kwa kui-quote post yote.
 
Mzee Msasambegu, kama utakua umenielewa mimi naongelea vyuo vikuu ambavyo hata wewe nina uhakika unavijua. Sasa ukinitajia hivyo Kampala University, St john, IMTU, Hubert Kairuki sijui St Joseph na vingine vya namna hiyo hapo nadhani utakua hujanielewa.

Mimi nimesoma kipindi vyuo vikuu viko 2 tu, University of Dar es salaam na Sokoine University of Agriculture, hata Muhimbili ilikua ni Faculty tu iliyokua chini ya UDSM, hiyo Mzumbe ilikua ni Institute hakikua chuo kikuu, sasa hivi vingine ukiona vinachukua hata wa Division 3 usifikiri hilo liko kwa vyuo vyote. Hata shule za secondary tu huwezi kuniambia mwanafunzi anayeingia kidato cha kwanza shule kama St. Francis au Marian girls/boys atakua na uwezo kama yule wa shule ya Anna Mkapa secondary school au Frederick Sumaye secondary school na shule za aina hiyo.

Mfano kama hicho St Joseph ni juzi tu tumesikia mambo yake ya kufutwa baadhi ya campus zake. Entry point zinazoonyeshwa kwenye makaratasi huwa si kigezo cha kuchukuliwa, kikubwa hapo huwa ni competition iliyopo.

Hayo mambo ya at least two principals na vitu kama hivyo si kwamba watu 20,000 wakipata hivyo vi-principals wote watachuliwa tu. Hivi mtu wa Division 3 anaweza kuchukuliwa Computor Science au Computor Engineering au any Engineering? ukiachana na hizo unazoziita min entry, hizo ni kukuonesha tu kwamba angalau mtu wa points hizo anaweza hata akajaza hiyo kozi lakini si lazima achaguliwe. Mkuu kama kweli umepita katika vyuo vikuu vya uhakika mbona hili lipo wazi kabisa? Usibaki kuangalia hizo entry points.

Mwisho kabisa, hizo "or or or" na "and and and" unazozitumia zinakuonesha level yako na hata hilo jina lako la Mzee nani sijui linakua halina maana tena.
Wewe ulikuwa unashangaa eti division 3 hawezi kusoma law na kuniuliza kama mimi nimesoma kweli?? Na mimi ikabidi nikushangae je na wewe umesoma kweli???ndo nikakupa mfano na my friend alikuwa na 3 kasoma mzumbe law na msisitizo nimekuonesha hata min entry qualification za law ni ndogo sana hazina utofauti mkubwa na education..na nyinyi mnavyodai kuwa walimu wanaufaulu mdogo hamja specify ni walimu waliosoma chuo gani ndo wanaufaulu mdogo ndo nikakuomba unipe uhalali wa mwalimu aliyesoma ud kuonekana anauwezo mdogo kuliko mtu aliyesomea udaktari kampala wakati aliyesomea ualimu ufaulu wake ulikuwa mkubwa kuliko huyo daktari and umetoa maelezo mengi but umekwepa kujibu maswali yangu ya msingi coz nimekuuliza tunajua nchi yetu ili ufundishe level ya primary inatakiwa uwe mwalimu mwenye elimu ngazi ya cheti nikakuuliza katika kada zote ngazi ya cheti ni kada gani inayochukua ufaulu mkubwa kuliko zote umeruka kunijibu ukaja na conclusion kuwa hizo"or...and" nazotumia zinaonesha level yangu....yeap its true level yangu ya elimu ni darasa la saba but naweza kuwa nauwezo wa kudadavua mambo kuliko hata wewe mwenye phd
 
Shida sababu zako zimekosa kusema selection pia hutegemea mapenzi ya mtu. Mfano, mimi mzee alikua mhasibu na alipenda nisome b.com ila tulikosana kwa hilo. Engineering nilikua sitaki hata kuisikia.Nilikua napiga zangu mapindi kabla hata sijachukua form UD nikaona nikafie huko.
Hata hivyo mleta mada amesema "walimu wengi kama sio wote". Kwa maneno mengine kuna baadhi yao kama wewe hawaangukii katika hayo maelezo. Mkuu usije kujikuta unathibitisha maneno ya mleta mada bila kujua!
 
Nimekukubali, umeandika vizuri sana mkuu. Kama ni baadhi maana yake si wote, sasa yule ambaye anaona hayuko kwenye category ya ufaulu hafifu maana yake haangukii kwenye mada hii.
 
Back
Top Bottom