Me nadhani huyu mdogo wetu hakueleweka vizuri, alichosema ni kwamba walio wengi wanasomea ualimu Kutokana na mambo matatu aliyoyataja,
Hivyo, Yawezekana kabisa mtu akawa na div I. 3 ya form six lakini akasomea ualimu si kwa sababu anapenda hiyo kazi bali anataka apate mkopo au ili apate ajira baada ya kuhitimu kwani anatoka kwenye familia ambayo hana watu wa kumshika mkono ili apate kazi BoT nk,
So me sijui kwanini mnapoteza muda na nguvu nyingi kulumbana!!
Hivi Kuna mtu mwenye div one, nyumbani pesa zipo za kumsomesha hata akikosa mkopo, ukoo wao mambo Safi kila idara Wapo na hivyo issue ya ajira kwake sio tatizo lakini akasomea ualimu?? Kama Wapo basi ni wachache mno na hao ni wazalendo wa dhati zaidi ya mwl Nyerere!
Heshima kwenu walimu wote, nyie ni watu muhimu sana, anaewadharau na alaaniwe!!!!!