Walimu acheni kuuliza watoto "Mmeelewa?"

Walimu acheni kuuliza watoto "Mmeelewa?"

Chrysanthemum

JF-Expert Member
Joined
Oct 28, 2016
Posts
1,936
Reaction score
7,026
Walimu wazuri wazuri , wanafunzi wazuri wazuri 🎵
Umeingia darasani, ukaeleza somo kwa nguvu zote. 😅 ukatumia mbinu zako shirikishi , mara onesho mbinu n.k
Then unawaangalia wanafunzi wako unaasema:

👉🏽 “Mmeelewa?”
Darasa zima:
“NDIYOOO MWALIMUUU!” 😂😂
Lakini baada ya dakika tano tu unauliza swali…
😶😶Mmoja anaangalia dari, mwingine dirishani, mwingine anaanza kugeuza daftari kana kwamba jibu limejificha ukurasa wa mwisho. 😂 Wanakwepesha macho ukiwaangalia

Tatizo ni kwamba “Mmeelewa?” mara nyingi hakupimi uelewa—kinachopima ni ujasiri wa kusema YES!
Mtoto anaweza kusema “ndiyo” kwa sababu kwanza anaogopa kuonekana hajui, pili anaogopa kuuliza swali ( maana wengine wenu ni wakali kinoma acheni hizo) mwingine anaona wenzake wote wameelewa, hivyo naye aseme tu “ndiyo.” 😂 au anaamini kabisa ameelewa… mpaka umpe zoezi aone mashikoro 😂
Me napendekeza badala ya kuuliza “Mmeelewa?”, jaribu haya maswali

Niambie kwa maneno yako au nielezee kwa ufupi, mwenyewe tulichojifunza.”
Hapa unaangalia kama mtoto ameielewa concept kweli, siyo amekariri tu.

“Ulipataje hilo jibu?”
Hili ni zuri sana kwenye Hisabati, Sayansi itakupa mwanga mzuri zaidi kujua wapi amekwama.

Pia kitu muhimu kujifunza usiangalie jibu pekee angalia namna alivyofikiri.
Mtoto anaweza kupata jibu sahihi kwa bahati. 😂 hasa hivi vichei chei vya la kwanza na la pili.
Lakini akieleza hatua alizofuata, hapo ndipo unaona kama kweli ameelewa.

Mbinu nyingine unaweza kumwambia “Nipe mfano wako mwenyewe.”
Kama anaweza kutengeneza mfano wake, kuna uwezekano mkubwa ameielewa concept na siyo kukariri definition tu.
Mwalimu uliza pia “Ni sehemu gani imekuwa ngumu kwako?” Hili linampa mtoto nafasi ya kusema wapi anakwama , walimu wa hesabu angalieni hii mambo asee
Usione ugumu yaan si lazima urudie somoyote. Huenda ni kipande kidogo tu ambacho hakijaeleweka.

Yaan hii sentensi iogopeni sana
“Ndiyo mwalimu!” si guarantee kwamba wameelewa. 😂😂

“Mwalimu endelea tu, tutaonana kwenye mtihani.” 😂😂

Kazi yetu kama walimu siyo kumaliza tu mada kwenye mpango wa somo.
Kazi yetu ni kujua kama mtoto kweli AMEJIFUNZA.
 
Hiyo approach yako ya kumuuliza swali mmoja mmoja itafanyaje kazi kwa darasa lenye wanafunzi zaidi ya 80?
 
Watoto wa kisasa walio zakiwa kipindi cha vidonge na sindano, inabidi walimu wafanye tu hivyo maana ukiwatandika viboka tu... tayari mada🫤
 
Back
Top Bottom