Sabri-bachani
Member
- Apr 3, 2008
- 96
- 3
Mimi nashukuru kwamba wewe mwenyewe sasa umeanza kufahamu mambo. Punguza jazba utazidi kufahamu zaidi. Tokea lini Zanzibar mtu akakosa cheo kwa sababu ya kuwa na damu ya Kiarabu. ,Nani kakueleza hivyo aliyekuwa Bingwa wa histotoria. Hebu angalia utawalam wa hivi sasa. Katika Baraza la Mawaziri la Mheshimiwa Karume. Wamo wenye damu ya Uarabu, Wamo wenye damu ya Uhindi (Ukumbaro), Wamo wenye damu ya Unyamwezi, Wamo wenye damu ya Ushirazi, Wamo wenye damu ya Uhadimu,wamo wenye damu ya Upemba. wamo wenye damu ya Utumbatu- ni mchanganyiko maalum. Ukitaka data zaidi wenyewe wakiruhusu nitakupa na majina. Please jifunze historia. Na acha jazba.Sasa huu ujinga wa CCM wa kuwalaghai watu kwamba mtu hafai kuwa kiongozi kwa sababu tu ana matone ya damu ya warabu itabidi ukome. Natazamia pia wale wajumbe wenzetu hapa JF ambao wamekuwa wakishindilia sana kwamba Salim hafai kuwa Rais wetu kwa kisingizio cha u-Hizbu itabidi wawe wastaarabu watoke hadharani hapahapa watubu, vinginevyo wanyamaze kimya milele katika hili maana inaonekana ama hawajui wanaloliongea au nao ni sehemu ya propaganda za ovyo za CCM!