Walichosema CUF - Nyaraka

Mzee Mwanakijiji

Platinum Member
Mar 10, 2006
33,539
40,166
Yafuatayo ni majibu ya chama cha CUF kuhusu sakata zima la muafaka kama walivyotoa jana. CCM na nyinyi kama mnayo majibu yenu penyezeni hapa mwanakijijiatklhnews.com ondoa neno "at" na weka alama ya @
 
Attachments

  • MaelezoyaCUF-Muafaka.doc
    114.5 KB · Views: 306
Mwanakijiji,

Kisura wa Kikwere ana kazi kweli mwaka huu. Alifikiri kazi ya Urais ni kazi nyepesi kupanda benzi na mabodigadi!

He is yet to make a tough descision that will define his reign!

EPA, Richmond, Rada, Kiwira, TICTS, Buzwagi na sasa Muafaka. He ought to have blood preasure medication to suppress his blod preasure level to skyrocket.

However, he is Mkwere, always taking things at ease and he possibly have one of the deepest sleep that he can never hear a 3:00 am call mpaka wamwagie maji!

CUF watamtoa kamasi pamoja na ujinga wa kukamata watu kule Pemba!
 
Let it boil baby, i don't feel sad kwa mkwere hata siku moja. Wacha CUF wawasukumize CCM mpaka watokwe kamasi.

Naona CUF wemekubaliana na mimi kwamba kingunge need Alzeimer check. I said once kwamba CUF wangekataa kuingia kwenye makubaliano the day kingunge alipofika, you can't trust the 95 years old guy. Who knows about his mental status?
 
Watanzania wanahitaji kumuona kama anavyojishughulisha na masuala ya Kenya, Comoroes, Zimbabwe na hivi majuzi tu mgogoro wa DRC Congo na Uganda, basi kwa uzito mkubwa zaidi ashughulikie suala hilo la mpasuko wa kisiasa Zanzibar. Wahenga wamesema sadaka huanzia nyumbani.

Hapa Mkuu ndipo kabisa atachekwa, na kupoteza umaharufu wake anaojijengea.
 
Baada ya kusoma hoja nzito za namna hii ndipo sasa huwa namtafuta Kasheshe na kundi kuja kuonyesha busara za Chama chao .Tuwape nafasi .
 
Baada ya kusoma hoja nzito za namna hii ndipo sasa huwa namtafuta Kasheshe na kundi kuja kuonyesha busara za Chama chao .Tuwape nafasi .
Hakuna jipya wala hoja nzito... Ni habari ambazo zimekuwepo kwenye masikio yetu kwa miaka sasa..
 
Njia ya mwongo ni fupi na majuto ni mjukuu.

Katika mazungumzo ya mwafaka Sisiem wamepwaya kweli,Tatizo kubwa la msingi haliko pekee kwa katibu mkuu mgosi na babu wa Kilwa,bali Mwenyekiti wa chama ambaye ameshindwa kuenea ktk kiti hasa mambo yapokuwa out of contol.Kila kitu yupo nyuma ya kamera wala haonekani.Mwishowe mkanda utaisha na aibu kubwa itampata.Alilianzisha mwenyewe dec 30,2005 kwa nini asilimalize kwa gharama yeyote?Kwa kuwa aliamua kuchukua siti hiyo kubwa basi inabidi ailipie ili asafiri kwa raha
 
Haya Yote namlaumu Makamba na Kingunge,Wakati Mwingine unaweza kuwaombea Mabaya utadhani wao ndiyo wazanzibar??

Wazanzibar waachwe waamue watakavyo wao,kuna maana gani kuendele kusigana kusikoisha,huyu anasema hivi na huyu ansema hivi.

Kama ukiona mtu anakushinda kila mara kwanini usiungane naye?
 
Subirini waje na hoja yao wakiongozwa na Makamba na Babu yetu......
Kama unativii yako izime tu la sivyo utajikuta unatamani kuua mtu buree.
 
Ukweli ni kwamba chama tawala kinaendelea kuparaganyika...sasa hivi kila mtu anasema lake hata hatuna hakika tumsikilize nani. Mara Shamuhuna kaibuka na kujibwatukia ghafla wanasema yake hayo! Jana Makamba alikuwa Pemba kenda jieleza kwa Wapemba...kama yaleeee ya mawaziri na bajeti zao, hawakawii kusema ni maoni yake binafsi. M/kiti siti imekuwa moto hajui hata pa kushikia, si walimtosa Butima? Sasa hajui awe upande gani Maji ya shingo!!! Babu nae hekima ndio hamnazo unategemea nini toka kwake? Anataka kufia kwenye hako kakiti anaongea tu na wauzauza ya umri
 
ccm wameendekeza usanii wakafikiri hauna kikomo.
sasa wanaabika vibaya sana, hivi kikwete ataongea nini kuhusu hili!
lakini ana moyo mgumu kweli, wala hakosi usingizi, ndo kwanza anaenda kufungua pantoni!!
 
Nami nimemaliza kuisoma hii dosier, Kwa kweli, kwa mara nyingine tena, CUF wameonyesha umakini wao na wamezidi kuanika udhaifu wa CCM. Nimefurahi zaidi pale walipowashughulikia CCM kuhusu madai yao yasiyokwisha ya u-Hizbu. Kumbe at the end of the day, kama ni u-Hizbu, CCM ni Hizbu kuliko Hizbu wenyewe. Lakini kwa jinsi CUF walivyo makini, wametoa hii historia sio kwa lengo la kuwaumbua CCM bali kwa nia ya kuonyesha jinsi ambavyo Zanzibar ni taifa la watu mchanganyiko na kwa vyovyote vile watu wengi sana kule Zanzibar hawawezi kukwepa damu ya mwarabu. Sasa huu ujinga wa CCM wa kuwalaghai watu kwamba mtu hafai kuwa kiongozi kwa sababu tu ana matone ya damu ya warabu itabidi ukome. Natazamia pia wale wajumbe wenzetu hapa JF ambao wamekuwa wakishindilia sana kwamba Salim hafai kuwa Rais wetu kwa kisingizio cha u-Hizbu itabidi wawe wastaarabu watoke hadharani hapahapa watubu, vinginevyo wanyamaze kimya milele katika hili maana inaonekana ama hawajui wanaloliongea au nao ni sehemu ya propaganda za ovyo za CCM!

Hapa kwa kweli ndugu zetu CCM wameshikwa pabaya. Ambacho hawataki kukielewa watu wa CCM ni ukweli kwamba katika ulimwengu wa leo ni vigumu mno kukalia habari. CCM wanatia huruma na kusikitisha zaidi wanapoendelea kumtumia Kingunge awatetee na kuwasemea kwenye mambo controversial kama haya. Yote hii ni kwa sababu wanafikiri watu watakubali tu kwa kuwa anayeongea ni Kingunge wasijue kwamba Kingunge mwenyewe heshima yake katika jamii ilishashuka kuliko hata ya Makamba! Bora wangewatumia Ze Comedy kuliko kumtumia Kingunge.

Hata hivyo, tusisahau hawa mabwana wa CCM wamezoea kuishi kwa ujanjaujanja wa kuwadanganya watanzania basi na mambo yamekuwa yakienda hivyohivyo. Bila ujanjaujanja, ghiliba, uongo, kujigeuzageuza CCM haiwezi ku-survive. Ndio maana sasa katika ulimwengu huu wa leo ambao huwezi ku-survive bila competence in style and substance wenzetu wa CCM inawawia ugumu.

Ngoja tusubiri watasema nini kwenye hii dosier ya CUF lakini kwa mambo yalivyo hawana hoja zaidi ya kuendeleza ujanjaujanja na ghiliba tu
 
Imefika mahali CCM wamekuwa wanamipasho, hawana hoja za kuweza kutetea kile wanachotaka badala yake wanatafuta namna ya kumpaka matope yeyote anayewagusa "pabaya". Hizi ni dalili za mwisho kabisa za kufilisika kisiasa. Na ikumbukwe hata huyo waliyeenda kumtambikia Butiama alionya kuhusu kutenga watu kwa ukabila na asili zao..."sisi wapemba wao ..." Leo hii wamejikuta juu ya kuti kavu wanayasema mambo ambayo hata historia yake hawajaifanyia kazi. Swala si nani kaanzia wapi bali ni vipi huu mpasuko uzibwe?

Nataka kuamini ikiwa M/kiti atafungua mdomo wake siku za karibuni atafanya upembuzi ya kinifu na kulichukulia swala hili hapo lilipofikia kwa unyeti wake na hatakurupuka ...japo si tabia yao kutokukurupuka
 
Nimeanza kuona mantiki katika msimamo na staili anayoitumia Kikwete katika kukabili mambo mengi mazito yanayoikabili serikali yake na chama chake - kama kweli hii ni mbinu mahsusi anayoitumia kwa maksudi na kwa lengo maalumu.

Natumaini kuwa staili hii mahsusi sio udhaifu; bali ni mbinu. Kama hivyo ndivyo; basi wengi tutafurahi wakati atakapoonyesha makali yake, wakati utakapowadia.

If he does that, many of us will be pleasantly surprised, and obviously thankful!
All the chips are still in place Mr. President, for you to show the way. It is about time now, don't leave it until it is too late!
 
Mimi nashindwa kuelewa kwanini kiongozi mzima kama Mzee makamba na Kingunge wanakaa na waandishi wa habari na kusema uongo ambao wanajua kabisa kesho yake CUF watakuja na vielelezo vya uhakika kuwaelimisha wananchi kitu gani kilitokea.

Hivi wameishiwa vitu vya kusema kiasi kuwa lazima waseme uongo ambao ni dhahiri kabisa ili wapate support ya wananchi? Hivi taharifa yao walimuonyesha mwenyekiti wao au walikimbilia kwenye vyombo vya habari bila mwenyekiti kujua? Hivi mwenyekiti anajiweka nafasi gani kwa kukubali uongo kama hule usomwe mbele ya waandishi wa habari?

Nafikiri umefika wakati wa kuwapima akiri viongozi wote wa CCM kwa kuanza na bwana makamba.

Jamani watetezi wa CCM hapa kijiweni mbona hamuonekani tunataka kusikia kutoka upande wenu.
 
Tatizo la viongozi wetu ni kufanya mzaha kwenye masuala ya msingi na ndio imetufikisha hapa tuliko.

ukisikiliza ufafanuzi uliotolewa na makamba na kingunge, hata mtoto mdogo atakuwa na wasiwasi na kinachoelezwa kwani mzaha ni mwingi kuliko maelezo ya msingi.

Ombi kwa JK anatakiwa kufanya mabadiliko makubwa kwenye safu ya uongozi kwani mzaha kwenye mambo ya msingi ni hatari sana,apate watu wanaoweza kujenga hoja na si jasiba.

Kuhusu muafaka afanye maamuzi kwa masilahi ya taifa na hatasikia mtu akilalamika hata mmoja kwani kila mtu ataona ni nini kimefanyika.kwa sasa jammaa wanamchezea na kumtisha at watarudi ASP na yeye anaogopa huu ni mchezo wa kuigiza.
 
Nakumbuka kauli aliyotoa mzee mkapa akisema alikuwa amezoe kuonga vita na mauaji kwenye nchi nyingine na ni kwenye tv,na ghafla akayaona yanatokea Zanzibar ndio akajua pia hata nchini kwake yanaweza kutokea,

Hapa viongozi wetu wanafikiri hakuna mtu anaweza kuanzisha vurungu lakini wanasahau vurugu zote zina kuwa zikifadhiliwa na mataifa mengine pindi mwanya wa kutoelewana unapoonekana katika nchi yeyote ili waweze kufanya biaashara zao.

JK tunakuomba uzibe huo ufa uliojitokeza kwa manufaa ya nchi yetu yasije yakatokea ambayo hatuyapendi kwasababu ya uzembe wa watu wachache.

Jk Naomba usikilize sauti za wananchi na usizibeze kwani madhara yake yatakuwa mabaya na tusingependa yatokee.
 
Nami nimemaliza kuisoma hii dosier, Kwa kweli, kwa mara nyingine tena, CUF wameonyesha umakini wao na wamezidi kuanika udhaifu wa CCM. Nimefurahi zaidi pale walipowashughulikia CCM kuhusu madai yao yasiyokwisha ya u-Hizbu. Kumbe at the end of the day, kama ni u-Hizbu, CCM ni Hizbu kuliko Hizbu wenyewe. Lakini kwa jinsi CUF walivyo makini, wametoa hii historia sio kwa lengo la kuwaumbua CCM bali kwa nia ya kuonyesha jinsi ambavyo Zanzibar ni taifa la watu mchanganyiko na kwa vyovyote vile watu wengi sana kule Zanzibar hawawezi kukwepa damu ya mwarabu. Sasa huu ujinga wa CCM wa kuwalaghai watu kwamba mtu hafai kuwa kiongozi kwa sababu tu ana matone ya damu ya warabu itabidi ukome. Natazamia pia wale wajumbe wenzetu hapa JF ambao wamekuwa wakishindilia sana kwamba Salim hafai kuwa Rais wetu kwa kisingizio cha u-Hizbu itabidi wawe wastaarabu watoke hadharani hapahapa watubu, vinginevyo wanyamaze kimya milele katika hili maana inaonekana ama hawajui wanaloliongea au nao ni sehemu ya propaganda za ovyo za CCM!

Hapa kwa kweli ndugu zetu CCM wameshikwa pabaya. Ambacho hawataki kukielewa watu wa CCM ni ukweli kwamba katika ulimwengu wa leo ni vigumu mno kukalia habari. CCM wanatia huruma na kusikitisha zaidi wanapoendelea kumtumia Kingunge awatetee na kuwasemea kwenye mambo controversial kama haya. Yote hii ni kwa sababu wanafikiri watu watakubali tu kwa kuwa anayeongea ni Kingunge wasijue kwamba Kingunge mwenyewe heshima yake katika jamii ilishashuka kuliko hata ya Makamba! Bora wangewatumia Ze Comedy kuliko kumtumia Kingunge.

Hata hivyo, tusisahau hawa mabwana wa CCM wamezoea kuishi kwa ujanjaujanja wa kuwadanganya watanzania basi na mambo yamekuwa yakienda hivyohivyo. Bila ujanjaujanja, ghiliba, uongo, kujigeuzageuza CCM haiwezi ku-survive. Ndio maana sasa katika ulimwengu huu wa leo ambao huwezi ku-survive bila competence in style and substance wenzetu wa CCM inawawia ugumu.

Ngoja tusubiri watasema nini kwenye hii dosier ya CUF lakini kwa mambo yalivyo hawana hoja zaidi ya kuendeleza ujanjaujanja na ghiliba tu

Hii taarifa imetoa mwanga kwa mambo mengi lakini Mkuu usiseme kuwa Chama Cha Mafisadi hawatakuwa na hoja - hawa jamaa ni Master Planner utaona watakuja na mpya na utaona hii dossiersi chochote.
 
Nami nimemaliza kuisoma hii dosier, Kwa kweli, kwa mara nyingine tena, CUF wameonyesha umakini wao na wamezidi kuanika udhaifu wa CCM. Nimefurahi zaidi pale walipowashughulikia CCM kuhusu madai yao yasiyokwisha ya u-Hizbu. Kumbe at the end of the day, kama ni u-Hizbu, CCM ni Hizbu kuliko Hizbu wenyewe. Lakini kwa jinsi CUF walivyo makini, wametoa hii historia sio kwa lengo la kuwaumbua CCM bali kwa nia ya kuonyesha jinsi ambavyo Zanzibar ni taifa la watu mchanganyiko na kwa vyovyote vile watu wengi sana kule Zanzibar hawawezi kukwepa damu ya mwarabu. Sasa huu ujinga wa CCM wa kuwalaghai watu kwamba mtu hafai kuwa kiongozi kwa sababu tu ana matone ya damu ya warabu itabidi ukome. Natazamia pia wale wajumbe wenzetu hapa JF ambao wamekuwa wakishindilia sana kwamba Salim hafai kuwa Rais wetu kwa kisingizio cha u-Hizbu itabidi wawe wastaarabu watoke hadharani hapahapa watubu, vinginevyo wanyamaze kimya milele katika hili maana inaonekana ama hawajui wanaloliongea au nao ni sehemu ya propaganda za ovyo za CCM!

Hapa kwa kweli ndugu zetu CCM wameshikwa pabaya. Ambacho hawataki kukielewa watu wa CCM ni ukweli kwamba katika ulimwengu wa leo ni vigumu mno kukalia habari. CCM wanatia huruma na kusikitisha zaidi wanapoendelea kumtumia Kingunge awatetee na kuwasemea kwenye mambo controversial kama haya. Yote hii ni kwa sababu wanafikiri watu watakubali tu kwa kuwa anayeongea ni Kingunge wasijue kwamba Kingunge mwenyewe heshima yake katika jamii ilishashuka kuliko hata ya Makamba! Bora wangewatumia Ze Comedy kuliko kumtumia Kingunge.

Hata hivyo, tusisahau hawa mabwana wa CCM wamezoea kuishi kwa ujanjaujanja wa kuwadanganya watanzania basi na mambo yamekuwa yakienda hivyohivyo. Bila ujanjaujanja, ghiliba, uongo, kujigeuzageuza CCM haiwezi ku-survive. Ndio maana sasa katika ulimwengu huu wa leo ambao huwezi ku-survive bila competence in style and substance wenzetu wa CCM inawawia ugumu.

Ngoja tusubiri watasema nini kwenye hii dosier ya CUF lakini kwa mambo yalivyo hawana hoja zaidi ya kuendeleza ujanjaujanja na ghiliba tuKitila kumbuka JK anaongoza Nchi kwa nguvu za Ukada .Mambo hayo yanatumika China , Burma nk lakini hawachelewi kuchemsha .CUF ni chama makini sana na wote walio kuwa wanabisha wameona .Heko CUF hadi mwisho itajulikana .Wacha tungoje spinning ya CCM sasa .
 
Back
Top Bottom