huyo jamaa amenena kabisa...maana hiyo kwanza watu wataacha kumegana na ata wakimegana watakuwa makini hasa hawa wanawake....itasaidia sana maana hamna mambo ya kubambikiana na watoto kulelewa na single parent. mwana alitoa point na namsupport
Sijui anawaza nini tu alietoa hayo maoni.
Yew! Hizi avatar hizi, baada ya kupima na kujua kabisa migulu yako mizuri ndio ukaweka kama avatar! Mi nataka katiba mpya wanawake wavae "Baibui"
Hahahahaaa sasa pamoja na kuwa mang'ana ndio usepe jamani. We hujui kama jini akipanda anapungwa ili atulie?
Hahahahaaaa wala hakupandi, mtakuwa "Partners"
Nyani Ngabu, Watz wengi ni wajinga kwenye maswala ya Katiba. Wanaropoka tu na wala hawajui tofauti ya Katiba na Sheria zingine. Mmoja alishawahi kusema Katiba Mpya izuie safari za Rais nje ya Nchi! Sasa sijui kama alishawahi kuiona hata Katiba ya sasa ajue kama imetoa ukomo wa safari za viongozi nje ya nchi. Mwingine akadai anataka Katiba mpya izuie wanawake kuvaa vimini/nguo fupi la sivyo wafungwe miaka 10! Hivi kama haya ndio maoni ya Watz wa karne hii, kuna umuhimu kweli wa kuendelea na huu mchakato ilhali wananchi wengi hawajui wanachokifanya? Poor Tanzanians! Ama kweli ukistajaabu ya Firauni utaona ya Mtumishi wa Mungu Musa!Kwenye huu mchakato wa kukusanya maoni ya katiba mpya nimesikia kila aina ya viroja.
Hitimisho nililofikia ni kwamba watu wengi somo la uraia linawapiga chenga.
Kuna mmoja nilimsikia anataka katiba mpya ikataze uzinzi. Kuna mwingine anataka lotion zipigwe marufuku na hiyo katiba mpya. Na kuna mmoja anataka sare za vyama vya siasa nazo zipigwe marufuku.
Kuna wanaotaka pia ndoa za mkataba ziruhusiwe na katiba mpya lol.
Ndiyo Watanzania hao.
Partner una kimeo nini?
Hili sio la kitaifa tu partner ni la kimataifa