WALE TULIOWAHI CHONGEWA TUKAKIONA CHA MOTO

WALE TULIOWAHI CHONGEWA TUKAKIONA CHA MOTO

AbuuMaryam

JF-Expert Member
Joined
Dec 26, 2015
Posts
2,651
Reaction score
4,758
KICHWA CHA HABARI CHA HUSIKA...

WALE tuliowahi kuchongewa either na mdogo wako au kaka yako au mama au shangazi au yeyote katika familia ukala kipondo au kazini au shuleni mwisho wa siku kupata matatizo si cha nchi hii hebu tukutane hapa tueleze ilikuaje na yupo wapi snitch wako iwe kweli alikuchongea au uongo...aliyekubonda au kukupa shida yupo wapi...anakuangaliaje usoni...

Nianze na mimi..

Nakumbuka nilipokuwa kinda kijijini, Bibi alisafiri akaniachia maagizo kwamba kuna mama fulani jirani akija nimchotee unga nimpe...sasa kuna binamu yangu fulani wote tulikuwa tunaishi kwa bibi...na bamdogo angu fulani mkali huyo...Sasa binamu yule akaja kunichongea kwa bamdogo kwamba nimechukua kitu ndani bila ruhusa nikampa mtu...

Bamdogo alikuwa mfuta sigara zile za vijijini za kusokota kwa tumbaku, sasa akiwa ameiwasha sigara yake, akanambia weka miguu ukutani mikono chini yaani hivyo hivyo mpaka sigara yangu iishe...huku akinitia mafimbo makubwa makubwa hayo mpaka damu ikatoka puani yaani nyie acheni nililia eti...

Wala sikuwa mtukutu alafu nilikuwa nasifika kijijini kwa nidhamu na upole na tabia nzuri, wanakijiji walimmind, MIMI NIKASEMA HAPA NITAKUFA...NIKAFANYA MCHAKATO WA KUTOROKA KUJA TOWN DSM KWA BABA MZAZI...NILIAGA SHULENI WANAFUNZI WENZANGU, MAJIRANI NA KIJIJI KIZIMA KUWA MIMI NAONDOKA KASORO HOME TU HAKUNA ALIYEJUA KUANZIA BIBI, BAMDOGO NA WENGINE WOTE...NA HATA SIKU NATOROKA BIBI NDIO ALINIAMSHA NIENDE SHULE DARASA LA 4 ENZI HIZO, NINA MIA 9 TU NIMECHANGIWA NA MAJIRANI NILIOWAAGA NATOKA MIKOA YA KASKAZINI MPAKA DAR, YAANI KUTOKA BUSH MPAKA TOWN STAND KUU KUPATA MABUS YA KWENDA ARUSHA ILI KUJA DAR...ILIKUWA KUNA COSTA 3 ZINAPITA KWA KWA MASAA...NIKASEMA NKISEMA NIZISUBIRI NITASHTUKIWA...NIKAANZA KUUMA PORI KWA PORI MPAKA NIMEFIKA KATIKATI HIVI PORI LINA WANYAMA KAMA SIMBA FISI, ASUBUHI KALI ILE...NI ALLAH TU ALIYENILINDA...NIISHIE TU HAPA KWA SASA BUNDLE LIMEKATA...ISITOSHE WINO WANGU UMEFIKA MWISHO...

Hebu shusha mkasa wako hapo chini...kushare changamoto hizo...
 
Back
Top Bottom