Wale tuliotoka familia masikini na tukatusua kimaisha tukutane hapa

Haya maisha muacheni mungu aitwe mungu.

Miaka 3 tu ilibadilisha kabisa upepo wa maisha, nilitengeneza zaidi ya 600m.

Katika utafutaji naamini kabisa na bahati inachangia, sikutumia nguvu kubwa sana katika utafutaji wangu na wala simjui mganga.

watu mpaka leo hawaamini mimi kuishi kwenye nyumba ya zaidi ya 200m.
Woooow! Hongera kaka.

"Hakuna uganga wala uchawi kwenye nyumba ya Israel".
 
Hujamaliza hata nusu mwaka tangu ujiunge JF lakini unataka kuanza uongo na utapeli. Hii thread yako unataka watu wakuombe connection maana unasema wewe ni meneja at the same time ni Mkurugenzi tena wa bodi.

Acha ushamba dogo, jiandae na September Conference. Ulidhani huku ni facebook?
Duh! Usilolijua... Malizia. Ningetaka kuwa tapeli mbona ningetapeli wengi mno tena watu wazito?

Pia ningekuwa na tamaa ningepiga madili mengi mno, hebu imagine nimeshawahi kukacha dili la 80M!

Sihitaji ku-prove kwa yeyote, nawa-inspire wahusika wasikate tamaa kupitia hii historia yangu.
 
Perspection uliyotumia kujenga hoja ku justify umaskin ulikuwa nao back in days haina uhalisia kwa mfano unasema ulishindwa kutembelea kumbi za starehe siku za mwisho wa juma sababu hukuwa na pesa kwenda club sio hitaji muhim kukosa kwenda club haimaniishi ww maskin kuna watu wana pesa and they had never visit huko inshu ya madem pia haina uhalisia kupiga pass ndefu ndo maisha ya wanachuo walio wengi pia dhana ya kutusua ni pana zaidi hapo unaposema ww umetusua kwa mwenzio ni umaskin wa kutupwa
Ila nilichojifunza maskin wengi huzaa watoto wengi some body to test the null of this hypothical idea
 
Wanajamvi nawasalimu!

Nilipokuwa chuo niliishi maisha magumu mno, mlo nilikuwa nakula mmoja tu napo ni jioni. Home hakukuwa na hela na hawakuweza kunilipia ada. Hela yote ya boom nilikuwa naigawa kulipa madeni, ada na pango, na kubakiwa na kiasi kidogo mno ambacho hunisogeza kwa siku chache tu.

Wasichana wazuri nilikaa nao mbali kwani sikuwa na cha kuwapa. Wanasema ni bora kujifanya unazo ili uwanase, ila kwangu uongo ulikuwa ni mwiko kwani aibu ya kuumbuka ni kubwa mno. Nimeshakosa tests kadhaa chuo kwa kukosa hela ya ada ila kwa uwezo tu wa Mungu nilifanikiwa.

Home hakuna hata mmoja aliyefika advance, ni mimi tu. Dada zangu karibia wote wanne walipata mimba na hawakuweza kusoma. Mmoja ameishia form four na akafeli.

Kaka zangi wawili wameishia la saba na kufeli kuingia form one.
Pata picha hapo maisha yalivyokuwa magumu. Ilifika wakati mtaani tulikuwa tunachekwa kwani tulijazana watu wengi ndani ya nyumba moja ndogo ya vyumba vitatu, na vyote uliishi humo kuanzia baba, mama, ndugu na watoto wote.

Narudi maisha ya chuo...Chuo sikuwahi kutembelea kumbi za starehe kwani sikuwa na pesa za kutosha, na ukizingatia DSM kila weekend wanachuo hufurika kumbi zote za starehe kula bata.

Nilivaa mavazi ya kimasikini japo si sana. Nilijitahidi kusoma kwa bidii na kwa uchungu mkubwa. Hakuna 'demu' yeyote aliyenipenda katika kipindi hiki, wote walinikwepa kama kinyesi. Ila sikuwa na kawaida ya kukopa kopa hela kwa watu au kulia lia shida hovyo. Kifupi nilikuwa ni masikini jeuri.

Sijui kilitokea nini ila kwa sasa ni manager katika shirika X la serikali hapa DSM, pia ni mkurugenzi wa body X ya shirika la serikali hapa DSM. Mishahara yangu yote miwili ni 8M plus marupu rupu, kwa mwezi.

Namshukuru Mungu kwa kunifuta machozi ya muda mrefu, na hayo ndiyo maisha niliyopitia chuo.

'Mungu na awaone wengj wanaopitia kipindi kigumu kwa muda huu'

Nawasilisha, karibuni tufarijiane na tukumbushane maisha haya ya uchungu.

Kwa sasa nashukuru Mungu wanangu wanaitwa WA KISHUA. Thanks lord!
Inspiration.
 
Sijali sana ukakasi uliopo kuhusu story zako lakini achana na kitu kinaitwa umaskini, kisikie hivyo hivyo tu kaka.Huwezi kuelewa kwa kuigiza,umasikini mbaya sana na hakuna hisia mbaya kama kukosa kula kwa sababu hauna chakula.hata hivyo tupambane tu.Mungu yupo na anajua kila kitu
 
Perspection uliyotumia kujenga hoja ku justify umaskin ulikuwa nao back in days haina uhalisia kwa mfano unasema ulishindwa kutembelea kumbi za starehe siku za mwisho wa juma sababu hukuwa na pesa kwenda club sio hitaji muhim kukosa kwenda club haimaniishi ww maskin kuna watu wana pesa and they had never visit huko inshu ya madem pia haina uhalisia kupiga pass ndefu ndo maisha ya wanachuo walio wengi pia dhana ya kutusua ni pana zaidi hapo unaposema ww umetusua kwa mwenzio ni umaskin wa kutupwa
Ila nilichojifunza maskin wengi huzaa watoto wengi some body to test the null of this hypothical idea
Ni kweli masikini huzaa watoto wengi mno!
 
Nika zani uta elezea ume ikwamua vipi familia yako pia.ila nme ishia kuona tu mshahara jeh kama una utumia wote kufanya vile ulivyo vikosa chuoni
Kitu cha kwanza katika msisha ni kujikwamua binafsi then the next of kin and others.
 
Back
Top Bottom