Wale tuliotoka familia masikini na tukatusua kimaisha tukutane hapa

Yes bro, si uongo. Ni mkurugenzi wa bodi fulani, inawezekana.
We jamaa hata mimi nahisi kuna chai kwenye huu uzi. Hebu tuwekane sawa kwanza. Unamaanisha wewe ni mwenyekiti wa bodi ya taasisi fulani ya serikali au mkurugenzi?. Hivi vyeo vyako hebu viweke vizuri, ni meneja wa nini hasa na ni mkurugenzi wa bodi au mwenyekiti wa bodi?
 
I meant nilipokuwa mwaka wa 2 chuoni kaka. Now nina-approach 31 years.
31 uko meneja na mkurugenzi at the same time tena serikalini huo UONGO

Miaka hii ya sasa kukuta wa umri huo kuwa katika hizo senior ni nadra sana

Tena serikalini unahold two positions tena executive position aisee

Labda ungekuwa mjumbe wa bodi

Yaani uwe meneja huku halafu mkurugenzi kule tena serikalini hio haiwezekani

Walioko serikalini watakubalina na mimi labda kama babu yako alikuwa MzilanKENDE muyago kwa yule mtu kila kitu kilifanyika
 
I meant nilipokuwa mwaka wa 2 chuoni kaka. Now nina-approach 31 years.
Umewezaje kufikia umeneja na ukurugenzi katika shirika na bodi ya serikali katika umri ambao wengi ndio huwa wako katika hatua za mwanzo ajira za serikali?
 
Maisha ya jamii forum yanachanganya sana
Wewe juzi tu hapa sii ulisema uko second year au nimekuchanganya
Leo umeshakuwa manager tena kwenye kampuni mbili
nimesoma comment chache tu hapa ila nilichogundua jf wana wivu sana adi thread imeharibika maana na lengo lake
 
Mishahara yote miwili ni 8M+

Well, hajatusua as such. Salary is time bound. Sio “asset”. Most importantly - unachopata sio issue ila kinachobaki baada ya kufanya expenses zako zote ndio muhimu zaidi
Mkuu Kwa maskin ninaoujua mm acha ale maisha tu
 
Wanajamvi nawasalimu!

Nilipokuwa chuo niliishi maisha magumu mno, mlo nilikuwa nakula mmoja tu napo ni jioni. Home hakukuwa na hela na hawakuweza kunilipia ada. Hela yote ya boom nilikuwa naigawa kulipa madeni, ada na pango, na kubakiwa na kiasi kidogo mno ambacho hunisogeza kwa siku chache tu.

Wasichana wazuri nilikaa nao mbali kwani sikuwa na cha kuwapa. Wanasema ni bora kujifanya unazo ili uwanase, ila kwangu uongo ulikuwa ni mwiko kwani aibu ya kuumbuka ni kubwa mno. Nimeshakosa tests kadhaa chuo kwa kukosa hela ya ada ila kwa uwezo tu wa Mungu nilifanikiwa.

Home hakuna hata mmoja aliyefika advance, ni mimi tu. Dada zangu karibia wote wanne walipata mimba na hawakuweza kusoma. Mmoja ameishia form four na akafeli.

Kaka zangi wawili wameishia la saba na kufeli kuingia form one.
Pata picha hapo maisha yalivyokuwa magumu. Ilifika wakati mtaani tulikuwa tunachekwa kwani tulijazana watu wengi ndani ya nyumba moja ndogo ya vyumba vitatu, na vyote uliishi humo kuanzia baba, mama, ndugu na watoto wote.

Narudi maisha ya chuo...Chuo sikuwahi kutembelea kumbi za starehe kwani sikuwa na pesa za kutosha, na ukizingatia DSM kila weekend wanachuo hufurika kumbi zote za starehe kula bata.

Nilivaa mavazi ya kimasikini japo si sana. Nilijitahidi kusoma kwa bidii na kwa uchungu mkubwa. Hakuna 'demu' yeyote aliyenipenda katika kipindi hiki, wote walinikwepa kama kinyesi. Ila sikuwa na kawaida ya kukopa kopa hela kwa watu au kulia lia shida hovyo. Kifupi nilikuwa ni masikini jeuri.

Namshukuru Mungu kwa kunifuta machozi ya muda mrefu, na hayo ndiyo maisha niliyopitia chuo.

'Mungu na awaone wengj wanaopitia kipindi kigumu kwa muda huu'

Nawasilisha, karibuni tufarijiane na tukumbushane maisha haya ya uchungu.

Kwa sasa nashukuru Mungu wanangu wanaitwa WA KISHUA. Thanks lord!
Elimu yako haijakukomboa. Kwa uandishi huu naamini umesoma kile Chuo Kikuu pale Msamvu
 
nimesoma comment chache tu hapa ila nilichogundua jf wana wivu sana adi thread imeharibika maana na lengo lake
No sina maana hiyo, Ila siku moja before hajaleta hii thread tulikuwa tunabishana kwenye jukwaa la elimu kuhusu maswala ya chuo.
 
Maisha ya jamii forum yanachanganya sana
Wewe juzi tu hapa sii ulisema uko second year au nimekuchanganya
Leo umeshakuwa manager tena kwenye kampuni mbili
Kuna kausemi ka wahenga ' ukiongopa sharti uwe na kumbukumbu" labda hakajui
 
Ni fikra zako tu kuwa ulikuwa Maskini bana!!...tena mna nyumba kabisaa siyo padogo hapo......na ajabu mzee wako anaweza gharamia watoto shule hapo si ndo penyewe??? penye utajiri??

Kuna maskini huko hata hawajui kuna neno elimu...uende usiende ni sawa tu hata ukifaulu hawajui km mtoto amefaulu ni mpaka mwalimu aje awastue

mie ni tajiri niliye kuwa na fikra za kimaskini!....sikujua km nina maisha mazuri kuliko wengi niliosoma nao bali walipojua Maisha ya familia yangu walinishangaa sana kwa nini nasoma shule ile wkt Baba yangu ana pesa na majumba mengi!

wengi walipenda kushinda home kwetuu!! daaaa!!
 
61 Reactions
Reply
Back
Top Bottom