Kwanini thamani ya baba katika familia nyingi haitambuliki?

Song of Solomon

JF-Expert Member
Aug 5, 2021
2,733
5,490
Huyu apewe maua yake , ya lazima kuisoma natafsiri kwa kifupi tu.

Mkutano wa Familia

Mama yetu alifanya kitu cha kustaajibisha na kusichotegemewa. Alitutumia ujumbe wa mkutano wa dharura wa familia nyumbani. Sote wanne tulifika, lakini mama hakutupokea kwa furaha tuliozoweya. Kulikuwa na ubaridi fulani katika sauti yake.

Hata baba alishangaa kutuona wote watoto wake wa kiume pamoja na akamuuliza Mama kulikoni, akajibiwa subiri utajua sababu.

Mama akatushukuru kwa kuacha shughuli zetu na kufika lakini tumemuudhi. Na yeyote anayemuudhi yeye anakuwa amemuudhi Mume wake.

Baba alijaribu kusema lakini mama alivyomtazama akanyamaza na kutabasamu tu. Sijui kwa ndugu zangu wengine lakini mimi sijamkosea yeye na baba kwa njia yoyote. Kaka mkubwa alisema. Nina uhakika Mama.

Akatuuliza siku ya kuzaliwa ya baba yenu ilikuwa lini? Tukaangaliana kwa nyuso za hatia. Ilikuwa ni jana nikajibu.

Mama akasema kama nakumbuka vizuri hakuna hata mmoja wenu aliyepiga simu wala kutuma ujumbe kwenda kwa baba yenu. Kama ingekuwa ni yangu nyote pamoja na wake zenu msingeisahau na mngeirusha mitandaoni.

Na mgenipigia simu na kunitumia na kunijazia hela kwenye akaunti yangu. Nimewaangalia kwa miaka kadhaa lakini siwezi nikaachia hali hii iendelee. Baba alishangazwa sana na sababu ya mama kuitisha mkutano ule.

Kila mwezi mnanitumia hela bila kuwaomba. Lakini hamfanyi hivyo kwa Mume wangu kama vile siyo Baba yenu. Kwa ukweli acheni kunitumia Mimi tu. Namba ya Baba yenu mnayo lakini hamumpigii bali mnaniambia mpe salamu Baba.

Tukajisikia vibaya kwa sababu ya ukweli aliyotuambia. Nikakumbuka kwenye sherehe yake mama niliagiza hadi matarumbeta.

Mnafikiria ni nani alilipa ada zenu wote nyie Hadi mkahitimu vyuo vikuu. Nani alilipa kodi, alileta chakula tulichokula, aliyelipa kodi mpaka tukahamia kwenye nyumba yetu. Yeye ndiye alitafuta hela za kila kitu na Mimi nilimsaidia tu. Mnafikiria Baba yenu hapendi mapenzi na ukaribu na watoto wake. Mnadhani ni mama tu anayestahili. Mama alijifuta machozi.

Kwa hiyo mlipanga tu kusherehekea msiba wa mume wangu, kwa kununua ng'ombe kuwafanya watu wafikirie mlikuwa mnamjali sana? Mshukuru Mungu na nyie mna watoto na mtavuna mnachopanda. Msifikiri mume wangu halii na kusononeka. Au hasikii uchungu. Hamuwezi kujua.

Mama alituangalia kwa makini kabla hajajifuta tena machozi.

Sintokuwa miongoni mwa kundi la wanawake wanao watenganisha watoto na baba zao kwa kuwaambia ungo kuwa baba yao hakuwajali na hakuwafanyia lolote. Wapo Wapo wanaume wachache wasiojali lolote, lakini siongelei hao. Huyu baba yenu ni Simba wangu na katika miaka yake 75 bado anaustua moyo wangu. Sintoruhusu nyie mumdharau baba yenu.

Wakati tunatafakari mama aliondoka ghafla kwenda chumbani kwao na kurudi na funguo za gari la baba na pochi yake na kumshika baba mkono.

Twende alisema mama, na baba hakukataa na kumfuata. Mnaenda wapi? Wote tulisema kwa pamoja. Tunaenda na mume wangu kusherehekea siku yake ya kuzaliwa.

Lakini na mama.... Hakutujibu wala kutupa nafasi ya kusema lolote. Fungeni milango na geti, alimwambia Kaka mkubwa, ninao ufunguo wa akiba.

Waliingia kwenye gari na kuondoka. Watoto tukabaki na mkutano wetu. Tuliafikiana kuwa tumekosea na tukatambua kuwa hatuwezi kurudi makwetu mpaka tufikie muafaka wa suala hili. Tukawaambia Wake zetu kuwa hatutorudi kwa sababu hatujui wazazi watarudi saa ngapi. Tutalala huku.

Mama akiendesha walirudi saa 1:30 usiku. Mama hakushangaa kutukuta, ila baba alishangaa. Sote tuliomba msamaha wazazi wetu, na kuahidi kubadilika. Mama alirudi toka chumbani na Bibilia. Akafungua kitabu cha Waephesi na akasoma sura ya 6:2 inayosema "waheshimu baba na mama yako" ambayo ni amri ya pekee yenye ahadi.

"Bibilia haisemi mtukuze mama na umsahau baba yako. Uzuri wa amri hii inakuja na ahadi. Kwenye aya ya 3, inasema itakuwa vyema kwako na utaishi miaka mingi duniani.

Mama alichukua muda kufafanua aya hii katika Bibilia, na kutufumbua macho kwa ambacho hatukukifahamu. Mwisho alimtaka baba kutuombea. Alifurahi na kutusalia sala kutoka moyoni.

Hatukurudi makwetu na kuongea hadi usiku sana. Sina Budi kusema mama alitupikia chakula kitamu sana.

Mpendwa msomaji, usingojee mpaka sikukuu ya Baba au ya kuzaliwa baba ndiyo umuenzi baba yako. Nyayua simu yako na umpigie. Usimsahau katika maisha yako.

Wake waenzini Waume zenu. Msijiunge na wanawake wanaowachochea watoto wao kuwachukia na kuwatenga baba zao. Usiwageuze watoto wako kuwachukia baba zao.

Mahusiano ya familia ni ya thamani na hayana budi kuenziwa na kutunza siku zote kiendelevu. Usingoje siku maalumu kuonesha mapenzi na fadhila kwa wazazi wako. Fanya hivyo kila siku Mungu wabariki wababa wote popote walipo wakinge na vifo vya ghafla vinavyosababishwa na msongo wa mawazo .
 
Baba ni zaidi ya kulipa Ada shuleni na kulisha familia.

Wanawake wanatupiga gap kwenye ishu ndogo ambayo ni nyeti Sana., Ukaribu
Huo ukaribu halafu utalisha SAA ngapi familia?

Angalia familia ya Simba, wawindaji ni majike lakini wa kwanza kula ni mfalme ambayo kazi yake kuu ni kulinda himaya na kuzalisha majike tu lakini ukaribu na Watoto ni swala la majike.

Nature iko hivyo hata kwa binadamu, mama lazima awe na ukaribu zaidi, lakini kama una Watoto hawajui baba ni nini umekula hasara.

Baba ni sauti ya mamlaka wachezewe wote ukuongea wote wanapaswa kutii mamlaka.

Mimi Nina kalast born by list kakilizwq tu lazima aje kushitaki kwangu anajuwa Mimi ndio mamlaka ya mwisho naweza kumuadhibu yeyote akiwemo yeye.

Sasa jiulize ni kwa nini Watoto wa kike ni wanawake lakini ndio wanaowajali zaidi baba zao baadaye?
 
Unaweza ukawa mtafutaji na ukawa karibu na mtoto Mkuu.
 
Wakina baba wengi huwa wanapenda kuvuna wasichopanda, kulipa ada na kuhudumia familia huwa ni wajibu wa baba anaopaswa kuufanya bila kutegemea malipo yoyote....!

Ukitaka wanao waje kukutunza na kukupenda uzeeni unapaswa uwekeze upendo na ukaribu na wanao tokea wakiwa wadogo....! Sio utegemee miujiza kisa uliwasomesha na kuwalisha wakati ulikua ni wajibu wako
 
Baba ni zaidi ya kulipa Ada shuleni na kulisha familia.

Wanawake wanatupiga gap kwenye ishu ndogo ambayo ni nyeti Sana., Ukaribu
Mwanamke na kila alichonacho ni cha Baba! Mwanamke katika dunia hii hakuna anachomiliki! Ni kujitutumua tu na sisi wababa kwa busara tunawanyamazia na kuwafanya wavimbe bichwa! Wee mwanamke wakati unaolewa ulikuja na nini zaidi ya 'k'? Tunawanyamazia tu!
 
Wakina baba wengi huwa wanapenda kuvuna wasichopanda, kulipa ada na kuhudumia familia huwa ni wajibu wa baba anaopaswa kuufanya bila kutegemea malipo yoyote....!

Ukitaka wanao waje kukutunza na kukupenda uzeeni unapaswa uwekeze upendo na ukaribu na wanao tokea wakiwa wadogo....! Sio utegemee miujiza kisa uliwasomesha na kuwalisha wakati ulikua ni wajibu wako
Vyovyote utakavyoandika! Upendo wa mama mnaoupigia chapeo unatoka wapi kama si kutokana na gharama za baba? Baba asipogharamika mama yenu hali na mali ya kuwatunza angeitoa wapi? Hata hivyo baba kwa vile ni asili ya mali na vitu vyote vizuri hapa duniani hana haja ya kushindana na kiumbe dhaifu mwanamke! Mwanamke anayejitambua anaelewa hivyo! Wanaharakati na wanawake mabedhuri ndo haoooooh!
 
Huo ukaribu halafu utalisha SAA ngapi familia?

Angalia familia ya Simba, wawindaji ni majike lakini wa kwanza kula ni mfalme ambayo kazi yake kuu ni kulinda himaya na kuzalisha majike tu lakini ukaribu na Watoto ni swala la majike.

Nature iko hivyo hata kwa binadamu, mama lazima awe na ukaribu zaidi, lakini kama una Watoto hawajui baba ni nini umekula hasara.

Baba ni sauti ya mamlaka wachezewe wote ukuongea wote wanapaswa kutii mamlaka.

Mimi Nina kalast born by list kakilizwq tu lazima aje kushitaki kwangu anajuwa Mimi ndio mamlaka ya mwisho naweza kumuadhibu yeyote akiwemo yeye.

Sasa jiulize ni kwa nini Watoto wa kike ni wanawake lakini ndio wanaowajali zaidi baba zao baadaye?

Mabinti kuwa karibu na baba zao ni kwa sababu huwa wanaoneshwa care na ile emotional assistance ambayo kwa wazee wengi hawaioneshi kwa watoto wa kiume,

Inshort, baba anakuwa mkatili kiasi kwa watoto wa kiume "tough love" Ili kuwaandaa kupambana na dunia

Mama anakuwa hivyo kwa watoto wa kike ili kuwaandaa na ugumu wa kuwa home makers and mothers

Ndio maana mara nyingi, mtoto wa kiume anamuelewa baba yake akiyaanza maisha na mtoto wa kike atamuelewa mama yake baada ya kuzaa. Hivyo tu
 
Vyovyote utakavyoandika! Upendo wa mama mnaoupigia chapeo unatoka wapi kama si kutokana na gharama za baba? Baba asipogharamika mama yenu hali na mali ya kuwatunza angeitoa wapi? Hata hivyo baba kwa vile ni asili ya mali na vitu vyote vizuri hapa duniani hana haja ya kushindana na kiumbe dhaifu mwanamke! Mwanamke anayejitambua anaelewa hivyo! Wanaharakati na wanawake mabedhuri ndo haoooooh!
Mkuu tuliza munkari 😁😁

Asee mama ni mama tu, chukulia mfano

Baba anaweza agiza kuku choma na bear na hata akatoa offer kwa marafiki na michepuko bar ila watoto wanakula dagaa home

Ila mama ni mtu akienda hata kwenye sherehe si ajabu kurudi na juice au vyuku kwa ajili ya watoto wake

Kiufupi wanaume wengi tunagawanya attention kwenye mambo mengi ila mwanamke anapozaa, attention yake yote ipo kwa mwanae TU. Nothing comes first kuliko watoto na hili lipo hata kwa wale wanaofanya kazi.
 
Akina baba unaowatolea mfano ni akina baba wa ovyo kama walivyoakina mama wa ovyo wengi makatili na wauaji na kutoa mimba! Tunaongelea kwa ujumla! Familia nyingi zilizoimara (angalia hata hapo mtaani kwako), hesabu nyumba/familia zilizovizuri nani kiini cha uimara wa hiyo familia kama si baba? Ni familia chache (kama Baba yupo) kukuta kuimarika kwa hiyo familia kunatokana na mama!! Hata ukiona hivyo ujue nyuma yake kuna Baba! Mama hawezi kuleta ustawi endelevu bila supporti ya Baba! Baba kama Baba huna haja ya kujionyesha kwasababu wewe ni Baba. Fullstop! Akina mama ndo wanapiga Chalambe ili waonekane!
 
Asilimia tisini na tano (95%) ya Watoto wadogo nilio wauliza kati ya
"Baba na mama" wanampenda sana yupi?

Walijibu Mama.
 
Huyu apewe maua yake , ya lazima kuisoma natafsiri kwa kifupi tu.

Mkutano wa Familia

Mama yetu alifanya kitu cha kustaajibisha na kusichotegemewa. Alitutumia ujumbe wa mkutano wa dharura wa familia nyumbani. Sote wanne tulifika, lakini mama hakutupokea kwa furaha tuliozoweya. Kulikuwa na ubaridi fulani katika sauti yake.

Hata baba alishangaa kutuona wote watoto wake wa kiume pamoja na akamuuliza Mama kulikoni, akajibiwa subiri utajua sababu.

Mama akatushukuru kwa kuacha shughuli zetu na kufika lakini tumemuudhi. Na yeyote anayemuudhi yeye anakuwa amemuudhi Mume wake.

Baba alijaribu kusema lakini mama alivyomtazama akanyamaza na kutabasamu tu. Sijui kwa ndugu zangu wengine lakini mimi sijamkosea yeye na baba kwa njia yoyote. Kaka mkubwa alisema. Nina uhakika Mama.

Akatuuliza siku ya kuzaliwa ya baba yenu ilikuwa lini? Tukaangaliana kwa nyuso za hatia. Ilikuwa ni jana nikajibu.

Mama akasema kama nakumbuka vizuri hakuna hata mmoja wenu aliyepiga simu wala kutuma ujumbe kwenda kwa baba yenu. Kama ingekuwa ni yangu nyote pamoja na wake zenu msingeisahau na mngeirusha mitandaoni.

Na mgenipigia simu na kunitumia na kunijazia hela kwenye akaunti yangu. Nimewaangalia kwa miaka kadhaa lakini siwezi nikaachia hali hii iendelee. Baba alishangazwa sana na sababu ya mama kuitisha mkutano ule.

Kila mwezi mnanitumia hela bila kuwaomba. Lakini hamfanyi hivyo kwa Mume wangu kama vile siyo Baba yenu. Kwa ukweli acheni kunitumia Mimi tu. Namba ya Baba yenu mnayo lakini hamumpigii bali mnaniambia mpe salamu Baba.

Tukajisikia vibaya kwa sababu ya ukweli aliyotuambia. Nikakumbuka kwenye sherehe yake mama niliagiza hadi matarumbeta.

Mnafikiria ni nani alilipa ada zenu wote nyie Hadi mkahitimu vyuo vikuu. Nani alilipa kodi, alileta chakula tulichokula, aliyelipa kodi mpaka tukahamia kwenye nyumba yetu. Yeye ndiye alitafuta hela za kila kitu na Mimi nilimsaidia tu. Mnafikiria Baba yenu hapendi mapenzi na ukaribu na watoto wake. Mnadhani ni mama tu anayestahili. Mama alijifuta machozi.

Kwa hiyo mlipanga tu kusherehekea msiba wa mume wangu, kwa kununua ng'ombe kuwafanya watu wafikirie mlikuwa mnamjali sana? Mshukuru Mungu na nyie mna watoto na mtavuna mnachopanda. Msifikiri mume wangu halii na kusononeka. Au hasikii uchungu. Hamuwezi kujua.

Mama alituangalia kwa makini kabla hajajifuta tena machozi.

Sintokuwa miongoni mwa kundi la wanawake wanao watenganisha watoto na baba zao kwa kuwaambia ungo kuwa baba yao hakuwajali na hakuwafanyia lolote. Wapo Wapo wanaume wachache wasiojali lolote, lakini siongelei hao. Huyu baba yenu ni Simba wangu na katika miaka yake 75 bado anaustua moyo wangu. Sintoruhusu nyie mumdharau baba yenu.

Wakati tunatafakari mama aliondoka ghafla kwenda chumbani kwao na kurudi na funguo za gari la baba na pochi yake na kumshika baba mkono.

Twende alisema mama, na baba hakukataa na kumfuata. Mnaenda wapi? Wote tulisema kwa pamoja. Tunaenda na mume wangu kusherehekea siku yake ya kuzaliwa.

Lakini na mama.... Hakutujibu wala kutupa nafasi ya kusema lolote. Fungeni milango na geti, alimwambia Kaka mkubwa, ninao ufunguo wa akiba.

Waliingia kwenye gari na kuondoka. Watoto tukabaki na mkutano wetu. Tuliafikiana kuwa tumekosea na tukatambua kuwa hatuwezi kurudi makwetu mpaka tufikie muafaka wa suala hili. Tukawaambia Wake zetu kuwa hatutorudi kwa sababu hatujui wazazi watarudi saa ngapi. Tutalala huku.

Mama akiendesha walirudi saa 1:30 usiku. Mama hakushangaa kutukuta, ila baba alishangaa. Sote tuliomba msamaha wazazi wetu, na kuahidi kubadilika. Mama alirudi toka chumbani na Bibilia. Akafungua kitabu cha Waephesi na akasoma sura ya 6:2 inayosema "waheshimu baba na mama yako" ambayo ni amri ya pekee yenye ahadi.

"Bibilia haisemi mtukuze mama na umsahau baba yako. Uzuri wa amri hii inakuja na ahadi. Kwenye aya ya 3, inasema itakuwa vyema kwako na utaishi miaka mingi duniani.

Mama alichukua muda kufafanua aya hii katika Bibilia, na kutufumbua macho kwa ambacho hatukukifahamu. Mwisho alimtaka baba kutuombea. Alifurahi na kutusalia sala kutoka moyoni.

Hatukurudi makwetu na kuongea hadi usiku sana. Sina Budi kusema mama alitupikia chakula kitamu sana.

Mpendwa msomaji, usingojee mpaka sikukuu ya Baba au ya kuzaliwa baba ndiyo umuenzi baba yako. Nyayua simu yako na umpigie. Usimsahau katika maisha yako.

Wake waenzini Waume zenu. Msijiunge na wanawake wanaowachochea watoto wao kuwachukia na kuwatenga baba zao. Usiwageuze watoto wako kuwachukia baba zao.

Mahusiano ya familia ni ya thamani na hayana budi kuenziwa na kutunza siku zote kiendelevu. Usingoje siku maalumu kuonesha mapenzi na fadhila kwa wazazi wako. Fanya hivyo kila siku Mungu wabariki wababa wote popote walipo wakinge na vifo vya ghafla vinavyosababishwa na msongo wa mawazo .
By nature, bond ya mama kwa mtoto/watoto ni kubwa sana na hii ni kabla hajazaliwa, sababu 99.9%ya mtoto akiwa tumboni anategemea mam yake kwa kila kitu. na hata anapokuja kuzaliwa bado mama anakuwa karibu sana na mtoto kuanzia kunyonya hadi kuoga kwako.

kwaio kibinaadamu hii inajijenga akili katika maisha yake yote. ndo mana sisi wababa inatubidi tujenge strong joint zetu kwa watoto hata kama itafikia hakuna maelewano na mama zao,
 
Akina baba unaowatolea mfano ni akina baba wa ovyo kama walivyoakina mama wa ovyo wengi makatili na wauaji na kutoa mimba! Tunaongelea kwa ujumla! Familia nyingi zilizoimara (angalia hata hapo mtaani kwako), hesabu nyumba/familia zilizovizuri nani kiini cha uimara wa hiyo familia kama si baba? Ni familia chache (kama Baba yupo) kukuta kuimarika kwa hiyo familia kunatokana na mama!! Hata ukiona hivyo ujue nyuma yake kuna Baba! Mama hawezi kuleta ustawi endelevu bila supporti ya Baba! Baba kama Baba huna haja ya kujionyesha kwasababu wewe ni Baba. Fullstop! Akina mama ndo wanapiga Chalambe ili waonekane!

Mbona unafanya ionekane kama wanawake ni kama pretenders!!..

Ulishawahi kuishi na mama, dada, mashangazi etc. Maana kama umeshawahi kuishi nao bhasi ni wazi ulikuwa una bad experience. Japo haiondoi fact kuwa wanawake huwa selfless kwa watu wanaowapenda ndio maana wengi husema mtoto wa kike kamwe hasau kwao. Unadhani kwa nini

Wanawake Mungu amewajalia emotional level kubwa na huruma. Hapo ni sawa na mama, hafanyi ili aonekane ila ni ile love toka ndani yake,
 
Back
Top Bottom