Wale tuliotoka familia masikini na tukatusua kimaisha tukutane hapa

Mkulungwa01

JF-Expert Member
Jul 14, 2021
1,551
2,000
Wanajamvi nawasalimu!

Nilipokuwa chuo niliishi maisha magumu mno, mlo nilikuwa nakula mmoja tu napo ni jioni. Home hakukuwa na hela na hawakuweza kunilipia ada. Hela yote ya boom nilikuwa naigawa kulipa madeni, ada na pango, na kubakiwa na kiasi kidogo mno ambacho hunisogeza kwa siku chache tu.

Wasichana wazuri nilikaa nao mbali kwani sikuwa na cha kuwapa. Wanasema ni bora kujifanya unazo ili uwanase, ila kwangu uongo ulikuwa ni mwiko kwani aibu ya kuumbuka ni kubwa mno. Nimeshakosa tests kadhaa chuo kwa kukosa hela ya ada ila kwa uwezo tu wa Mungu nilifanikiwa.

Home hakuna hata mmoja aliyefika advance, ni mimi tu. Dada zangu karibia wote wanne walipata mimba na hawakuweza kusoma. Mmoja ameishia form four na akafeli.

Kaka zangi wawili wameishia la saba na kufeli kuingia form one.
Pata picha hapo maisha yalivyokuwa magumu. Ilifika wakati mtaani tulikuwa tunachekwa kwani tulijazana watu wengi ndani ya nyumba moja ndogo ya vyumba vitatu, na vyote uliishi humo kuanzia baba, mama, ndugu na watoto wote.

Narudi maisha ya chuo...Chuo sikuwahi kutembelea kumbi za starehe kwani sikuwa na pesa za kutosha, na ukizingatia DSM kila weekend wanachuo hufurika kumbi zote za starehe kula bata.

Nilivaa mavazi ya kimasikini japo si sana. Nilijitahidi kusoma kwa bidii na kwa uchungu mkubwa. Hakuna 'demu' yeyote aliyenipenda katika kipindi hiki, wote walinikwepa kama kinyesi. Ila sikuwa na kawaida ya kukopa kopa hela kwa watu au kulia lia shida hovyo. Kifupi nilikuwa ni masikini jeuri.

Namshukuru Mungu kwa kunifuta machozi ya muda mrefu, na hayo ndiyo maisha niliyopitia chuo.

'Mungu na awaone wengj wanaopitia kipindi kigumu kwa muda huu'

Nawasilisha, karibuni tufarijiane na tukumbushane maisha haya ya uchungu.

Kwa sasa nashukuru Mungu wanangu wanaitwa WA KISHUA. Thanks lord!
 

Malcom Sr

JF-Expert Member
Apr 17, 2021
991
1,000
Maisha ya jamii forum yanachanganya sana
Wewe juzi tu hapa sii ulisema uko second year au nimekuchanganya
Leo umeshakuwa manager tena kwenye kampuni mbili
Hii inaweza kuwa kweli katoboa na hela ya mboga anayo..

Lkn ishu ya kuwa manager kwny makampuni mawili ya serikali imenibdi nione Kama chai ya Buza..labda atuambie chuo amemaliza mwaka gani
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom