GENTAMYCINE
JF-Expert Member
- Jul 13, 2013
- 56,694
- 109,123
Nakumbuka Wiki iliyopita baada ya hili ‘ Sakata ‘ Kuibuka na Kuanza kusambaa sehemu mbalimbali na hasa hasa humu ‘ Mitandaoni ‘ kuhusu Mbunge Masele ya Spika wa Bunge Ndugai nilichangia katika Uzi wa Mtu hapa na ‘ nikatahadharisha ‘ kuwa Watanzania tuache ‘ Kukurupuka ‘ na kusukumwa na Hisia za ‘ Kianaharakati ‘ kwani Siku ukweli ukija Kutolewa Kwetu wengi Wetu tuliokuwa ‘ tukilaumu ‘ tu tutatafuta wapi tufiche Sura zetu kwa Aibu.
Baada ya Mbunge Masele ‘ Kuwaaminisha ‘ Watanzania wana Mitandao wa ‘ Kukurupuka ‘ kuwa Yeye hakuwa na Kosa huko katika Bunge la PAP ambapo Yeye ni Makamu wake / wao hatimaye jana ukweli kamili umejidhihiri na kuwekwa hadharani juu ya ‘ Mapungufu / Makandokando ‘ yake na kama kawaida wale waliokuwa ‘ wakimtetea ‘ Kutwa wamepotea ghafla wakati mwanzoni ndiyo walikuwa wakifululiza Kumtetea na Kudhania kuwa ameonewa au anaonewa.
Hivi Mbunge Masele Yeye ni nani mpaka alazimishe na hadi Kushinikiza kwa Watu wa Ikulu, Ofisi ya Waziri Mkuu na Taasisi ‘ Nyeti ‘ nchini kuwa ni lazima apatiwe Walinzi kutoka Usalama wa Taifa wa Kumlinda? Yeye ni nani hadi atake Kupewa Nyumba Kubwa ( Mansion ) na Gari za Kifahari na hadi awe na ‘ Msafara ‘ wake? Huu ‘ Ukubwa ‘ aliokuwa akiutaka Mbunge Masele unatokana na nini labda?
Bado nahoji wale wana ‘ Mtandao ‘ mliokuwa mkimtetea mpo wapi sasa? Mbona mmenyamaza?
Nawasilisha.