Wale Mlio Kibaha, Mnisaidie Contacts za Kiwanda cha Honey King!

ChamaDola

JF-Expert Member
Dec 23, 2016
3,431
2,804
Wakuu,
Nina asali mbichi na ningependa kuiuza hapo kiwandani!
kwa walio kibaha au katika viunga vyake,naomba mnisaidie:mawasiliano(emails,phone numbers) za kiwanda na bei ya lita moja!
Thanks in advance!
 
Unauzaage,, wekaa bei kwa paackage zake.
ni asali mbichi ya nyuki wakubwa:
lita moja 10,000/=
lita tano 50,000/=
lita kumi 100,000/=
lita 20 ni 200,000/
niko meatu ambako nimefuata mzigo!
 
Mkuu Itabidi Ufanyie Utaratibu Wa Kuuweka Kwenye Vifungashio Maana Najua
Kiwanda Cha Kibaha Kipo Barabarani Kabisa
Ukienda Na Mzigo Wakizingua Unakwenda Na Dar Kule Utauza Kwenye Super Markets Nyingi Sana
 
Mkuu Itabidi Ufanyie Utaratibu Wa Kuuweka Kwenye Vifungashio Maana Najua
Kiwanda Cha Kibaha Kipo Barabarani Kabisa
Ukienda Na Mzigo Wakizingua Unakwenda Na Dar Kule Utauza Kwenye Super Markets Nyingi Sana
nikiuweka kwenye vifungashio vya lita tano tano watachukua?na bei kwa lita ni tsh ngapi?
 
Mkuu Mimi Ukweli Sijui Bei Ila Ninaona Sana Dar Biashara Ya Asali Original Huwa Kwenye Super Market Hutakosa Kuuza
 
Wakuu,
Nina asali mbichi na ningependa kuiuza hapo kiwandani!
kwa walio kibaha au katika viunga vyake,naomba mnisaidie:mawasiliano(emails,phone numbers) za kiwanda na bei ya lita moja!
Thanks in advance!
Mkuu ndio hiki??

Honey king LTD

Basic Information Top
  • Business Type:
    Export & Inport
  • Main Markets:
    world wide
  • Company Categories:
    Dairy products; bird's eggs; natural honey; edible products of animal origin, not elsewhere specified or included
Contact Information
  • Company:
    Honey king LTD
  • Address:
    Visiga Dar es Salaam Dar es Salaam(72593)
  • Number of Employees:
    0
  • Company Tel:
    +255-773-299888
  • Company Fax:
    +255-22-2450790
 
ni asali mbichi ya nyuki wakubwa:
lita moja 10,000/=
lita tano 50,000/=
lita kumi 100,000/=
lita 20 ni 200,000/
niko meatu ambako nimefuata mzigo!
Meatu jangwani kwa asali wapi na wapi? Ama pale kwa wanakikundi njia ya kuelekea Bariadi?
 
Meatu jangwani kwa asali wapi na wapi? Ama pale kwa wanakikundi njia ya kuelekea Bariadi?
hapana,upande wa kaskazn kuelekea ndio hakuna asali kwa wingi!upande huo wote upo tarafa ya kisesa!
upande wa kusini ndiko asali iliko kwa wingi!kwani kuna mapori mengi ya akiba!kuna pori la akiba la makao,hili linaunganika na ngoro2 na serengeti upande wa arusha!na pia kuna pori la itaba!
na ukanda huu unapatikana tarafa ya nyalanja na kimali
 
bei ya jumla iko vipi huko vijijini
lita moja ni kati ya 2000-5000!
lita 5 ni 20.000 constant!
Lita 20 ni 80,000-100,000!
Hapo ni nje ya usafiri,vifaa,ushuru(japo ufuatiliaji hauko kivile),t.b.s,tfda,na mazaga mazaga mengineyo!
 
lita moja ni kati ya 2000-5000!
lita 5 ni 20.000 constant!
Lita 20 ni 80,000-100,000!
Hapo ni nje ya usafiri,vifaa,ushuru(japo ufuatiliaji hauko kivile),t.b.s,tfda,na mazaga mazaga mengineyo!
ok shukrani mkuu
 
Kesho kutwa jipange kupokea njemba sio chini ya 40 wakisaka mali huko nikiwemo mimi sababu information ni kamili.
lita moja ni kati ya 2000-5000!
lita 5 ni 20.000 constant!
Lita 20 ni 80,000-100,000!
Hapo ni nje ya usafiri,vifaa,ushuru(japo ufuatiliaji hauko kivile),t.b.s,tfda,na mazaga mazaga mengineyo!
 
ni asali mbichi ya nyuki wakubwa:
lita moja 10,000/=
lita tano 50,000/=
lita kumi 100,000/=
lita 20 ni 200,000/
niko meatu ambako nimefuata mzigo!
Hapo Honey King huwezi kupata Soko kwa bei hizo unazotaka. Kile ni kiwanda na kina utaratibu wake wa kupata raw materials moja kwa moja kutoka Shambani na siyo kwa rejareja kama unavyodhani. Isitoshe, na wao wanafanya Processing hivyo huhitaji raw materials at cheap price ili ku-minimize production costs...

Any way; Kwa nini umeamua kuji - involve kwenye Biashara bila kufahamu uhakika wako wa Soko.? Kwa nini kufanya biashara locally kiasi hicho, au haupo serious sana na biashara hiyo?

Nakushauri haya yafuatayo;
1)Tulia utafute network ya Soko kupitia kwa wadau mbalimbali, Biashara ya Asali kwa sasa bado ina changamoto kidogo kwa maana ya Soko la Uhakika. Lakini kuna wadau wakubwa ambao huchukuwa Asali kwa ajili ya kuzalisha bidhaa mbalimbali na kutumia Asali kama ingredients moja wapo. Wadau hao ni pamoja na Bakhresa, ASAS DAIRIES LTD.

2)Kama umeamua kufanya Biashara ya asali serious, tembelea TBS, TFDA, SIDO na TFS ili kufata taratibu za kufanya Biashara hii. SIDO utapata mafunzo mafupi jinsi ya kufanya packaging, na kupitia kwako unaweza kuleta mzigo wako na kufanya packaging kwa kupatiwa material and skills support. TBS kwa ajili ya ubora wa bidhaa yako, TFDA ni mamlaka ya chakula na dawa, TFS ni Taasisi inayosimamia na kuratibu biashara zitokanazo na mazao ya Misitu ikiwemo Asali.

3)Fungua Duka lako la Asali katika moja ya Miji mikubwa hapa Tanzania kama vile Mwanza, Dar, Morogoro, Arusha, Zanzibar,Tanga na Mbeya au Mkoa wowote unaodhani Biashara itakulipa. Ukiwa na Duka lako la asali ni rahisi kupata Network ya wadau wa Asali ndani na nje ya Nchi.

4)Hudhuria maonesho ya Siku ya Wakulima na nyinginezo; kupitia maonesho hayo tafuta Banda la wadau wa Asali kisha weka bidhaa yako hapo na utakuwa umejitangaza.
5)Tembelea BODI ya Asali Tanzania ili kupata network zaidi kuhusu Biashara ya Asali.
6)Mtembelee Former PM , Mizengo Pinda, yeye ni mdau Mkubwa sana, kisha omba ushauri kutoka kwake na mwambie akupe somo kubwa zaidi kuhusu upatikanaji wa Soko la Asali ndani na nje ya Nchi.

7)Ukifanikiwa kupitia njia zote hizo, usisahau kurudi hapa JF na kutoa shukrani kwa Wanajukwaa kutokana na ushauri mbalimbali ukiwemo huu wangu.
8)Fanya kazi kwa bidii bila kuwa na hofu na kukatishwa tamaa na Wanadamu.
9)Fanya biashara kwa njia halali, Mche Mungu, mwombe Mungu sana akusaidie katika shughuli zako za kujipatia riziki hapa Duniani, usitegemee akili zako pekee, mshirikishe zaidi Mungu naye atakufanikishia.
10)Kila lakheri katika yote.
 
Back
Top Bottom