Wakwe wamekataa kuzika binti yao

Statistics

JF-Expert Member
Sep 22, 2013
3,594
7,587
Amani iwe nanyi!


Kuna rafiki yangu likuwa ameoa, toka June 2016.( mwaka mmoja) na mke wake amefariki leo. Wakati anaoa hakuweza kutoa mahali hata senti.


Tatizo1. Wazazi wa marehemu wamekataa kuzika hadi mahali itolewe. Na mwili upo hospitali, mortuary.



Tatizo2: jamaa hana chochote, ndugu zake hawana uwezo na hajui cha kufanya ili apate ng'ombe 20 wanazotaka wakwe zake.


Jamaa: msukuma
Mke & wakwe: ni wasukuma.


Je, nini kifanyike ili kumzika huyo marehemu pasipo kutoa mahali?



NB: kutaja kabila la kisukuma isiwe maada, lengo la kuandika ili kuwapa watu mwanga wa kujadili kwa kutumia utamaduni wao na katiba ya Tanzania, hasa sheria ya ndoa.
 
kweli kufa kufaana kwahiyo wameamua kumfanya maiti ya binti yao mtaji? kama hana akaushe wataenda kuchukua maiti yao na kuzika!
 
Poleni, kuwa mwanaume ni kazi kwelikweli.
Akazikie kwao, death certificate au tangazo la kifo litamtetea mahakamani siku za machoni wazazi wa mke wakishtaki.
 
Jamaa akae kimya, aendelee na maisha yake kama kawaida, maiti hiyo itakaa Mortuary kama hao ndugu za huyo mwanamke hawatakuja kuichukua, baada ya muda fulani, serikali waitazika kama mzoga.

Hakuna kucheka na Kima.
 
Hili ni tatizo pia ni fundisho kwa vijana wanaopenda shoti kati, ni vyema ukatambua kuwa binti ana wazazi waliomlea, kitendo cha kuoana kiholeala sio vema kwani huyo ni binadamu lolote linaweza kutokea.
Hapo wazee wa pande zote lazima wakae chini waridhiane, vinginevyo ni pagumu
 
Akachukue kibali cha kuzika polisi... Mengine watamalizana baada ya mazishi... Mahari ingekuwa imebakia kidogo sawa...

Ila hiyo ni nyingi sana...



Cc: mahondaw
 
Manispaa si wanazika aachane na hao wakwe...
Imeandikwa mwanamke atamwacha baba na mama yake na kumfuata mumewe.
Sasa hao wasukuma wanataka wamgeuze marehemu binti Yao kitega uchumi.
Hili kabila ovyo sana!
 
akachukue maiti aizike afungue kesi mahakamani under certificate of urgence apewe kibali imetoka hiyo
 
Jamani hasa vijana msichukuwe mabinti za watu kinyemela bila mawasiliano ni hatari. Vijana wengine hufanya dharau na hasara mijini

Unaweza usiwe na kitu lakini mawasiliano ni muhimu tena ya kirafiki na ukweni kwako. Si busara kujichukulia mke bure tu.
 
Back
Top Bottom