Wakuu wa Wilaya hawa hapa!

Wakuu wa Wilaya hawa hapa!

Mkuu .. Huyo Ponsiano Nyami ni nani?(profile kwa kifupi) kapewa Tandahimba..

trachomatis, huyu alikuwa mbunge wa Nkasi huku Sumbawanga kwa muda mrefu. Uchaguzi uliopita aliangushwa katika kura za maoni ndani ya chama.
 
Last edited by a moderator:
CCM wameamua kujimaliza? Hii list itazidisha vita vya wenyewe kwa wenyewe. Imejaa wapambe!
 
ltn can lubinga ni jembe wazee km ni huyu aliyetokea etende jkt kwenda mlalakua mmjkt je amesha staafu
.ltn canal edward ole lenga nae ni mchapakazi halazi dam
,huyu huyu wa rombo simwelew kabisa siyo jembe hata kidogo
Enginia Ray mushi alipaswa apewe mkoa sio wilay ilani mchapa kazi karibu ilala
TUWASHUKRU
EVANCE BALAMA
CANAL MJENGWA NA HUYU WA MBOZI KWA KAZI NZURI WALIO IFANYAAAAAAAAAA
 
Itabidi tumtumie Zamaradi Mketema kumshauri Rizi maana naskia amezaa nae ndomana mbwe mbwe kibao na Bongo movie..next time msishangae kumkuta Kingwendu mkuu wa mkoa maana ye si anamshauri babake..mmeimba weee aongee na mshua haya kalonga nae..Mtajuta!!!! nilikuepo!!!


Nimecheka kwenye basi mpaka abiria wakanishangaa
 
Wakuu wa wilaya hawana jukumu lolote la ajabu ambalo wanalifanya. Ona tumekaa miaka miwili bila wao mbona mambo yanaenda kama jana na juzi tu. Acha wapeane ulaji wanamagamba.
 
kwenye blue hapo!! hao baadhi ni wabunge na walio kua wabunge...hivi kuna haja gani ya kurecycle??????

Wana recycle kwa kuwa "mwenzao" anakuwa ameangukia pua na hivyo wanatafuta namna ya kumpoza ili aweze kusonga mbele na maisha.

Kumteua mbunge kuwa Mkuu wa Mkoa/Wilaya, huu ni ubadhirifu. Moja, ataendelea kulipwa posho zote za Mbunge na haswa mafuta, wakati tukijua wazi kwamba anatumia gari la Mkuu wa Mkoa/Wilaya.

Kwa wastani, wabunge wanakuwa ama Dodoma au Dar kwa shughuli za Bunge kwa miezi 6 kwa mwaka [Bunge la Bajeti miezi 3, Vikao vingine 3 vya wiki mbili mbili sawa na mwezi na nusu, ukijumlisha na vikao vya Kamati za Bunge tayari unapata miezi karibu 6].

Kwa kipindi chote hicho, Mkuu wa Mkoa/Wilaya anatumia gari na dereva wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa/Wilaya. Matokeo yake ni kwamba mtu mmoja anajikuta analipwa mara mbili. Kama Rais angeteua mwingine ambaye si mbunge, angeweza kubaki kwenye kituo chake cha kazi kwa miezi 10 na kuwa nje ya kituo kwa miezi labda miwili tu ambapo hela ya mafuta, matengezo ya gari la mkuu wa mkoa na posho za dereva zingeweza kusalimika.

Tumeona mawaziri kibao wanajivinjari na mashangingi ya serikali na madereva wao wakiwa majimboni kwao wakifanya shughuli za kubunge, kitu ambacho ni makosa maana tayari huyo waziri analipwa na Bunge kufanya hizo shughuli za kibunge lakini bado serikali pia inalipia gharama za waziri kwenda jimboni kwake na wapo ambao kila weekend yuko jimboni kwake na hawezi kuulizwa maana ni sehemu ya majukumu yake kama mbunge.

Hapa ndipo kuna umuhimu wa wabunge kutokuwa sehemu ya serikali. Kuna mgongano mkubwa sana mbunge anapoteuliwa kuwa waziri au mkuu wa wilaya/mkoa, kwa kuwa inamnyima fursa ya kuwa huru kuwatumikia wananchi na pia inaongeza gharama kwa mlipa kodi na ni ubadhirifu wa mali ya umma.
 
Duh! Huyo Dogo hata chuo hamaliza teyari kapewa ulaji. Aliyechagua kweli Hamnazo.
 
Huyu James Olemillya Wilaya ya Longido kurudishwa tena Longido wakati alistaafu hii ndo mwisho wa CCM katika jamii ya wafugaji longido. Naona anakuja kuizika chama. Kweli nimeamini ccm haipo tena maana ccm imekuwa ikiota ndoto za kimweri kwamba wafugaji bado wapo ccm huku Lekule Akijitahidi kwa udi na uvumba kumtafuta mrithi.
 
Huyu James Olemillya Wilaya ya Longido kurudishwa tena Longido wakati alistaafu hii ndo mwisho wa CCM katika jamii ya wafugaji longido. Naona anakuja kuizika chama. Kweli nimeamini ccm haipo tena maana ccm imekuwa ikiota ndoto za kimweri kwamba wafugaji bado wapo ccm huku Lekule Akijitahidi kwa udi na uvumba kumtafuta mrithi.
Alishastaafu?
 
Sijamuona Betty jamani!!amelipa fadhila big time du!!haya itafika muda hizi nafasi za fadhila zitapitwa na wakati!!

Yupo kwenye list ya pili ya wale wa zamani. Jina namba 8. Anaitwa Elizabeth Mkwasa.
 
Kwahiyo unataka kusema baada ya tangazo la leo, wengi wataamia CDM?

Ya tanzania ni makubwa, manake nasikia na wabunge wengine wanataka kuamia CDM kisa hawakupewa uwaziri. Mtu anayehama kwa sababu kakosa uwaziri, ukuu wa mkoa, au Udc basi hafai manake huyo ni mwanachama tumbo!

Ukweli mwishowe utadhihiri kuwa; waliopo CCM wanalenga kushibisha matumbo yao tu!
 
Nilisema hapa kwenye post yangu ya page 1 kuwa jk atabeba wahadhir toka udsm,kuna mdau amenambia Dr KADEGHE MZEE WA CL AMEPEWA UKUU WA WILAYA MBOZI(KAMA SIKOSEI)......sasa ndo najiuliza wataalam hawa wakienda hulo,huku kwenye elim atabak nan????
 
Back
Top Bottom