Equation x
JF-Expert Member
- Sep 3, 2017
- 29,420
- 40,398
Binadamu wanachangamoto nyingi katika maisha, mtu anaweza kupambana katika maisha yake mwanzo mwisho bila kupata ushirikiano kutoka kwa ndugu zake au ukoo anaotoka. Wanaweza kuwepo waliofanikiwa, lakini wanakuwa hawako tayari kuwasaidia ndugu wengine waweze kufanikiwa.
Kwa waliopo mijini, unaweza kuona mtu anamafanikio makubwa na inapotokea yeye kufariki na kurejeshwa kwao kwa maziko, unakuta yeye alivyokuwa akiishi ni tofauti na ndugu zake wengine. Unakuta ndugu zake wamechokachoka wana afya dhaifu kutokana na umasikini.
Kuthibitisha hili fanya utafiti mdogo, nenda kwenye misiba ya watu waliofanikiwa......ukiona walioshiba na afya njema jua hao ni marafiki, na ukiona watu waliochokachoka jua hao ni ndugu.
Wakuu tupunguze ubinafsi.