Equation x
JF-Expert Member
- Sep 3, 2017
- 29,420
- 40,401
- Thread starter
- #41
Kwa nini inakuwa hivyo,wanakuwa hawana uchungu na unachowapatia au ni kutaka kurudishana nyuma tu?Mzee wangu aliniambia kwamba "huwezi kumfanya mtu aendelee (kumtoa mtu) mtu anajiendeleza mwenyewe"
Hii kauli sasa hivi naiona ya ukweli 100%. Wewe unaweza kuwa na uweza na ukawa hadi unatuma pesa kijijini ili watu wajenge na waanzishe miradi lakini siku ukirudi unakuta yule uliyemtumia ameongeza mke wa pili na hakuna mradi wowote..
Au unamlipia mtu ada likizo anarudi na 0 kitu pekee alichoweza ku-achieve ni kunyoa kiduku kichwani.
Sasa watu wa hivyo utawapa msaada gani?? Ndugu wa hivyo usipoangalia wanaweza kukurudisha kwenye circle of poverty tu. Kwahio kitu bora cha kufanya ni kutembea na wale wanaoweza kupokea msaada wako na kuufanyia kazi wawe rafiki , au hata ndugu wa mbalii.
NB. Cha muhimu wazazi usiwasahau tu. Lakini ndugu wengine kama hawana akili ya kujiendeleza wenyewe hata ukiwa unawapa mil 10 kwa mwezi utakuwa wameongeza wake na kulewa tu.