Wakuu nimeibiwa laptop 2 kwenye gari

Habari zenu, jioni hii nilipaki gari maeneo ya africana mbezi beach, wamevunja na kuiba laptop mbili lenovo, na vitu vingine na pesa, nimekuja kwenu kwa yeyote atakaefuatwa kuuziwa naomba kwa msaada wako u nitaarifu

Na pia nauliza hivi naweza pata mganga wa jadi atakaeweza kunisaidia kumpata huyu mwizi? Maana wamenirudisha nyuma sana na kuna vitu na documents.muhimu sana.

Nawasilisha
Wajameni wewe umesoma madarasa mangapi bado unafikiri in terms ya waganga wa jadi?

Sad, inaelekea ndo umetoka kwenu ushirombo. Do not leave valuables in unattended car .ndo message unayopewa ukipack sehemu kama uliyopaki ukalitelekeza gari. Sorry ndo umekaribishwa mjini.
Unaishi kwenye gari mpaka uweke laptop mbili na pesa?
 
Watu wanajifanya hawajawahi kusikia ushirikina, huu ni ulimbukeni. mimi nina ndugu yangu walipora duka usiku tena kukiwa na mlinzi wa kampuni. Kesi kwenda mahakamani ikawa hailelweki inavyoendeshwa.

Basi akatafutwa mganga kutoka Mkoa mwingine, Akasema tumfanye nini, wakamwambia unavyoweza ila arudishe mali, kumbe ilikuwa timu kubwa iliyoiba.

Yule mganga aliwajaza upepo, wakawa wanatuma ndugu zao kuomba msamaha.
Adabu walishikishwa na sidhani kama wanaendelea kufanya ushirikina.

Mwisho wa siku walisamehewa kwa sababu vitu wameshauza, kwa yale mateso waliyopitia ilibidi tu kuwaachia.

Sio hatuamini hizo nguvu zipo .zipo sana tu lakini ni wachache sana wenye power hizo..mtu mwingine hela yake ni safi kaipata kwa uchungu ukiiba lazima ikutese..
 
Hapo kweny kutumia Ndumba / Utapigwa kuzidi hadi hizo laptop baada uwaze njia zakitaalamu zakuwanasa awo wezi .

Sahv hakuna waganga wakweli labda kama unataka kujaza maji mtoni.


Semeni nyie msio wajuvi..lol!
Kigamboni kuna mganga alikua anamwelezea mshikaji jinsi anavyoagua yaan ni kituko...! Unaambiwa amejaza tu matunguri .anasema hata lugha anayoongeaga na wateja huwa haiwez hadi apige nyagi!yeye na nyag na mabomba kuunganisha mtu from point a to b
 
Hapo mie chakukushauri ni kuwa tangaza dau hata kwa uyo aliyeiba,mfano jamani mimi nimepoteza laptop lakini inadocoment zangu ambazo nazihitaji sana nipo tayari kutoa kiasi fulani cha pesa mfano Milioni Moja ili docoment zangu nizipate,nitashukuru kwa atakayenipatia,hapo kidogo unaweza ukazipata,Nakumbuka kuna mtu aliibiwaga vifaa vya gari usiku,Akamtumia mtu asubuhi yake kuulizia gerezani akajibiwa vifaa ivyo vipo ila sharti lake inakubidi utoe laki sita basi yule bro ilimbidi tu kutoa iyo hela mida ya mchana wakaja kumrudishia vifaa vyake kama mwanzo,Hapo bro jifanye tu mjinga kama kweli unataka kuvipata ivyo vifaa
 
Habari zenu, jioni hii nilipaki gari maeneo ya africana mbezi beach, wamevunja na kuiba laptop mbili lenovo, na vitu vingine na pesa, nimekuja kwenu kwa yeyote atakaefuatwa kuuziwa naomba kwa msaada wako u nitaarifu

Na pia nauliza hivi naweza pata mganga wa jadi atakaeweza kunisaidia kumpata huyu mwizi? Maana wamenirudisha nyuma sana na kuna vitu na documents.muhimu sana.

Nawasilisha
Kwa nin hukuziweka kwenye buti ya gari??

Sent using Jamii Forums mobile app
 
weee dogo angalia kauli zako.... baadae utakuja humu kujiliza.... Ooooh.... Mimi..... JF. ..... Sijui Slim5 ....


Hahhaa ni imani tu mzee baba...kila mtu kalelewa kwa imani yake sina imani hiyo kali sana ila amini nna imani yangu tu!najua ww mambo haya uko vyema sana!...mie nna damu kali sana ndugu yabgu km majanga yangenipataga way back...!
 
Pole Sana rafiki.Gari ulii-pack Africans sehemu gani mkuu.Nje ya bar au eneo gani? Maana miye nakaa eneo Hilo na ni mwenyeji.ili kesho nianze kuwapanga vijana wa eneo ulikoibiwa waanze kunusanusa na kudodosa kwa vibaka wa eneo ulikopack gari kwa ahadi KWAMBA walioiba wakirudisha,Tutawakatia kitu reasonable,na kwa ahadi pia KWAMBA hakutakuwa na mkono wa Sheria.Sema specifically ulipack eneo gani Africans na ILOKUWA around muda upi.

Sent using Jamii Forums mobile app
Barabara inayoelekea whitesand, mbele kuna mtaa unaitwa Manyara drive, kwenye hiyo manyara drive nilipark kama nusu saa kuna mahali gari haipiti nikavuka kwa mguu nikarudi baada ya dk 45 hv nikakuta wamevunja

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Yaani mimi huwa namshangaa sana mtu anayesema nimeibiwa laptop au simu iliyokuwa na documents za muhimu sana. Kweli kwenye dunia ya sasa, ambapo kuna aina nyingi tu za kuback up documents zako tena nyingine zipo automatic ukiweka tu document kwenye simu inajiback up automatic.
Tumieni technology acheni ushamba wa kulia lia
Asante

Sent using Jamii Forums mobile app
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom