Wakuu hii ipoje, Ushirikina au ndio dini?

Wakuu hii ipoje, Ushirikina au ndio dini?

Haihusiani.Alipombariki Petro kuvua samaki kwa nini alienda wanakovua samaki kabisa?Si angeagiza aletewe maji ayaombee kisha ayarudishe yalikotolewa?
Yesu alitemea mate udongo na kutengeneza tope na kumpaka kipofu na akapona

Je huo pia ni ushirikina?
Haya ni mambo ya kiroho , ukiyachambua physical hauto ambulia kitu
 
Haihusiani.Alipombariki Petro kuvua samaki kwa nini alienda wanakovua samaki kabisa?Si angeagiza aletewe maji ayaombee kisha ayarudishe yalikotolewa?
Kabla sijakujibu,
Niufanishe mfano wako wakipuuzi na huu,

Kwa nini hakujiokoa msalabani kama alikua ana miujiza?

Kila tendo kibiblia lina funzo hadi likaruhusiwa kuandikwa ,
 
Mambo yote ya Mungu ukiyatafuri kwa upande wa kishetani yanaendenda na ushirikina,shetani hakuumba kitu chochote isipokuwa anatumia vitu vilevile vilivyoumbwa na Mungu kwa kuvibadilisha.

Kipindi cha Musa, Musa alibadilisha fimbo kuwa nyoka, wachawi nao wakatengeneza nyoka, Mungu anasema usizini,shetani anasema zini.
CHANZO CHA YOTE HAYO NI HIKI [emoji116]

HOSEA 4:6.

Watu wangu wanaangamizwa kwa kukosa maarifa; kwa kuwa wewe umeyakataa maarifa, mimi nami nitakukataa wewe, usiwe kuhani kwangu mimi; kwa kuwa umeisahau sheria ya Mungu wako, mimi nami nitawasahau watoto wako.

Inamaana akihamia Ulaya pia akafatwe na Nabii uchwara huko huko anapoishi kuchukua udongo anapofanyia biashara ili uombewe ndipo biashara ifanikiwe [emoji848]

Kwani akipaombea mahali hapo pa biashara kwa imani thabiti tu haiwezekani kusikilizwa na kujibiwa na Mungu [emoji848]
 
Maandiko yako wazi kabisa kuhusu kuibuka kwa manabii wa uongo siku za mwisho, lakini watu bado wamekomaa kuwafuata kama nyumbu....
 
Maandiko yako wazi kabisa kuhusu kuibuka kwa manabii wa uongo siku za mwisho, lakini watu bado wamekomaa kuwafuata kama nyumbu....
kwa hakika siku za mwisho zimewadia
 
Manabii wa uongo wameshika akili zao
Mkuu usiombe kuchapika na maisha utaamini kila unaloambiwa....husikii sikuhizi vijana wako tayari kuwa wake za watu mradi tu wawe na maisha mazuri.....hakuna wakati tunahitaji ulinzi wa Mungu kama nyakati hizi
 
umeongea point mkuu!
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom