Wakurugenzi wa halmashauri wajiandaa kuchakachua hela za walimu. | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Wakurugenzi wa halmashauri wajiandaa kuchakachua hela za walimu.

Discussion in 'Jukwaa la Elimu (Education Forum)' started by Mpatanishi, Jan 21, 2012.

 1. Mpatanishi

  Mpatanishi JF-Expert Member

  #1
  Jan 21, 2012
  Joined: Jul 1, 2011
  Messages: 1,709
  Likes Received: 42
  Trophy Points: 145
  Wakuu nimepata taarifa zisizo rasmi kwamba huu ndio wakati wa zile hela za walimu za kujikimu ,nauli na hela za mizigo kuchakachuliwa.

  Ushauri wangu kwenu walimu wapya ni kuwa makini na kutafuta waraka wa serikali kwenda kwa wakurugenzi hao unao onyesha malipo mnayostahili kupata kila mwalimu.

  Walimu muache kuwa waoga, taaluma mmesomea na mmefuzu hivyo kamwe msikubali vitisho wa wakurugenzi hao.
   
 2. Laurence

  Laurence JF-Expert Member

  #2
  Jan 21, 2012
  Joined: Jun 11, 2011
  Messages: 3,105
  Likes Received: 35
  Trophy Points: 145
  Asante kwa taarifa,tafadhali mwenye huo waraka atuwekee hapa
   
 3. M

  Mamatau Member

  #3
  Jan 21, 2012
  Joined: Jan 6, 2012
  Messages: 84
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Wakurudengi wasizuliwe, waalimu wafuate taratibu na fehd zao watapewa kama zilivyopangwa na serikali.
   
 4. Laurence

  Laurence JF-Expert Member

  #4
  Jan 21, 2012
  Joined: Jun 11, 2011
  Messages: 3,105
  Likes Received: 35
  Trophy Points: 145
  Wewe mamatau umeelewa kinachosemwa au? Unaweza kufuata taratibu huku aliejuu asifanye taratibu zimpasavyo?
   
 5. Mpatanishi

  Mpatanishi JF-Expert Member

  #5
  Jan 21, 2012
  Joined: Jul 1, 2011
  Messages: 1,709
  Likes Received: 42
  Trophy Points: 145
  wewe mama ni DED nini?! Unataka kukataa kitu gani wakati kila mwaka haya mambo yanakuwepo?!
   
 6. Mpatanishi

  Mpatanishi JF-Expert Member

  #6
  Jan 21, 2012
  Joined: Jul 1, 2011
  Messages: 1,709
  Likes Received: 42
  Trophy Points: 145
  mkuu huyu mama tumsamehe tu mana hajui haya matatizo wanayopata walimu.
   
 7. The secretary

  The secretary JF-Expert Member

  #7
  Jan 21, 2012
  Joined: Jan 14, 2012
  Messages: 4,161
  Likes Received: 42
  Trophy Points: 145
  na sio uzushi ngoja wajifanye mazoba waone.watawalaghai kwa kusema kuwa walimu kutoka vyuoni ni wakorofi wamezoea migomo, wale ni wa kuwaendea kama unatoka boko haramu vile.waraka unapatikana ofisi ya utumishi,cwt, shuleni na kwa afisaelimu.lkn hawa wawili utumishi na afisaelimu ni ngumu kukupa lao moja.kaeni mtambue huo waraka ni haki yenu kuupata huwezi amini hawa watu wanakula mamilioni ya hela za walimu wanaoripoti
   
 8. Laurence

  Laurence JF-Expert Member

  #8
  Jan 21, 2012
  Joined: Jun 11, 2011
  Messages: 3,105
  Likes Received: 35
  Trophy Points: 145
  Mnafiki tu huyu mama,sasa mkuu tuutafute huu waraka kabla hatujaenda vituoni ili tujiridhishe mapema kabla hatujafika huko tuendako
   
 9. Laurence

  Laurence JF-Expert Member

  #9
  Jan 21, 2012
  Joined: Jun 11, 2011
  Messages: 3,105
  Likes Received: 35
  Trophy Points: 145
  Mkuu kama waweza pata huo waraka tusaidie kutuwekee hapa maana tunataka full details wasijeenda kutuibia bure,ok kama unakumbuka je waraka wa mwaka jana ulikuaje? eg ile hela ya siku 14 ilikua bei gani? pia kuhusu umbali wa km walikua wanalipaje? na mengine mengi uyajuayo mkuu
   
 10. Ngadu

  Ngadu Senior Member

  #10
  Jan 21, 2012
  Joined: Oct 10, 2009
  Messages: 123
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Kazeni buti
   
 11. The secretary

  The secretary JF-Expert Member

  #11
  Jan 21, 2012
  Joined: Jan 14, 2012
  Messages: 4,161
  Likes Received: 42
  Trophy Points: 145
  Mwaka jana mwezi wa nne wametoa waraka mpya kwa marekebisho ya waraka uliopita.fedha za kujikimu ni siku saba inategemea na kiwango cha elimu degree kwa jiji ni 85000,manispaa 65000,halmashauri 45000.pesa ya njiani [on transit sh.35000 kwa safari ya masaa zaidi ya 6.kama una mke,mtoto zaidi ya miaka 3 au mume muwe na cheti cha ndoa na mtoto analipwa nusu ya fedha ya kujikimu ya mwajiriwa kwa siku saba.mizigo ni km ulizotoka times tan 3 times 1000 yani kila km 1 ni sh.1000 ni sawa na 3000 times km ulizotoka hakikisha unapata waraka kabla ya kuripoti nenda hlmashauri yoyote uliyopo utapewa
   
 12. The secretary

  The secretary JF-Expert Member

  #12
  Jan 21, 2012
  Joined: Jan 14, 2012
  Messages: 4,161
  Likes Received: 42
  Trophy Points: 145
  kwani siku zote wanapanga nani kama si serikali jamani kuna ufisadi wa kuoza kwenye halmashauri hela tu za likizo mtu anakuzidishia kiwango ulichoomba ili ikifika tu wanachukua kiasi chao. kuhusu hela za kujikimu za walimu hata idara ya afya mpango unasukwa toka huko tamisemi mtashangaa kila ngazi unayoenda kudai wanalindana kwa kupiga danadana offcourse walimu wanafata utaratibu je hao wa juu wanafuata utaratibu watu husema kabla ya kumwagikiwa upupu huwezi jua mwasho wake .yani unaenda tamisemi mtu anakupa laivu kuwa sisi tunatabia ya kulindana
   
 13. Twilumba

  Twilumba JF-Expert Member

  #13
  Jan 21, 2012
  Joined: Dec 5, 2010
  Messages: 5,944
  Likes Received: 536
  Trophy Points: 280
  Ni tabia mbaya sana ku-generalize vitu kama alivyofanya hivi vitu, zaidi ni kutaka kujenga chuki kwa wakurugenzi kitu ambacho kitasababisha hawa walimu wafundishe kwa tension na pengine kusababisha kudorora kwa elimu kwa sababu walimu wapya wataamini wanaonewa kitu ambacho si kwa kweli kwa baadhi yao.

  Nijuanvyo mimi kuna walaka ambao unaeleza kuwa mtumishi anayeanza kazi atalipwa substance allowance ya siku 14 habari ya mizigo ilishafutwa kwa sababu itakuwa ni njia nyingine ya kumdhurumu mtanzania kwani mwalimu anayeanza kazi akitokea chuoni hatutegemea atakuwa na mizigo ya tani 3 ambayo ndio atataka alipwe pesa kama nauli ya kusafirishia mizigo hiyo toka place of domicide. Acha kuwapotosha wenzio standing order ipo kwa ajili ya kuwaongoza inapatikana huko halmashauri mtakapo report!

  Acha kuwapotosha watanzania ndugu.
   
 14. Laurence

  Laurence JF-Expert Member

  #14
  Jan 21, 2012
  Joined: Jun 11, 2011
  Messages: 3,105
  Likes Received: 35
  Trophy Points: 145
  Mkuu asante sana J3 ntaenda cwt makao makuu wanipatie ili nianze kujipigia hesabu mapemaa maana wengne tumesoma vyuo vinavyosemekana migomo imetamalaki,mkuu mie graduate
   
 15. Mpatanishi

  Mpatanishi JF-Expert Member

  #15
  Jan 22, 2012
  Joined: Jul 1, 2011
  Messages: 1,709
  Likes Received: 42
  Trophy Points: 145
  mkuu tutafutane twende pale cwt kupata huo waraka hakuna cha mkoba wala makoba mwaka huu wataelewa tu.
  Kuna mdogo wangu yupo village inabidi tupate huu waraka nae wasije wakamchakachua posho zake.
   
 16. Mpatanishi

  Mpatanishi JF-Expert Member

  #16
  Jan 22, 2012
  Joined: Jul 1, 2011
  Messages: 1,709
  Likes Received: 42
  Trophy Points: 145
  asante sana hapa watu wataelewa tu. Tunachotaka ni walimu kupata haki zao zote bila kuletewa uchakachuaji.
  Najua wabongo wengi wamezoea kucheza na haki za watu hivyo hapa watu wa halmashauri watataka kupata ada za watoto wao na hela ya kula kilaji kupitia posho za walimu hawa.
  Mm tayari ni mwalimu hvyo najua haya mambo yapo na mwaka huu ndugu zangu wawili nao waraka unawahusu.
   
 17. Laurence

  Laurence JF-Expert Member

  #17
  Jan 22, 2012
  Joined: Jun 11, 2011
  Messages: 3,105
  Likes Received: 35
  Trophy Points: 145
  Haina noma mkuu,wewe uko wapi kwa sasa? Mimi ni tbt so niPm ili tujue namna ya kukutana twende cwt huko
   
 18. The secretary

  The secretary JF-Expert Member

  #18
  Jan 22, 2012
  Joined: Jan 14, 2012
  Messages: 4,161
  Likes Received: 42
  Trophy Points: 145
  We ndo mpotoshaji mkubwa humu waraka umeusoma au ndo wale wanaoupata na kuweka mezani anafanya kazi kwa uzoefu .kwanza waraka huo usemao wewe ni upi sababu uliotoka mwaka jana mwezi wa nne umebadilishwa badala ya tani 5 kwa degree wameweka tani 3 na diploma ilikuwa tan 3 wameweka level sawa tani 3 kwa wote na ndio tulivyolipwa sisi na fedha za kujikimu si siku 14 tena ni siku 7.ufinyo wa kufikiri eti hutegemei wanaotoka chuoni hawawezi kuwa na mizigo kumauka kuna watu tayari wanakwenda chuoni na familia zao na wengine walikuwa wanafanya private wamejiendeleza na wengine wameoa na kuolewa wakiwa chuoni kumbuka siku hizi mtu yupo chuoni lakini anafanya kazi nyingine mtaani we ndio bingwa wa kugeneralize. jamani vijana njooni tuchape kazi na tujikomboe msisubiri cwt wale imebaki story tu wazee huku wanatuangusha uwezo tunao ,nia tumeonewa tumechoka hakuna kulishwa unga wa ndere na hawa wakina bi kirembwe.halimashauri zote zimeoza eti mtu unaomba waraka unaambiwa ni siri na huku umeandikwa uwafikie walengwa waajiri na waajiriwa.wanajf kazi kwenu kupima kama nadanganya au huyu ndo anadanganya.
   
 19. Twilumba

  Twilumba JF-Expert Member

  #19
  Jan 22, 2012
  Joined: Dec 5, 2010
  Messages: 5,944
  Likes Received: 536
  Trophy Points: 280
  Mkuu huo waraka ulitenguliwa na waraka mwingine ambao uliongeza posho za vikao mbalimbali vya halmashauri akafika hadi 200,000/- kwa mwenyekiti na hapo ndipo ule waraka wa posho mpya ukatenguliwa hii nadhani ni baada ya kuona hali ya uchumi si nzuri!

  Mkuu cha kuangalia ni namna ambavyo scale za mishahara ya walimu inaweza kubadilishwa na kufikia walau ile ya sekta ya Afya. Kwa gap lilopo wanatofautiana kwa zaidi ya asilimia 50. Hizo posho hazina msaada maana ni kitu cha mara moja, wakati mshahara ndo mapngo mzima!
   
 20. KANCHI

  KANCHI JF-Expert Member

  #20
  Jan 22, 2012
  Joined: Sep 3, 2011
  Messages: 1,547
  Likes Received: 57
  Trophy Points: 145
  Jamani m2 atakaye upata huo waraka aulete hapa jamvini basi.
   
Loading...