Uhamisho wa uonevu TRA, Kamishna Mkuu tafadhali ingilia kati

Dec 6, 2022
8
8
Mheshimiwa Kamishna Mkuu wa TRA, nachukua fursa hii kukuomba uingilie kati uonevu unaofanywa na wasaidizi wako kwenye uhamisho unaoendelea sasa.

Nimefanya kazi TRA miaka mingi lakini hali iliyojitokeza sasa si ya kufumbia macho.

Uhamisho si jambo baya kwenye utumishi, ni kawaida mfanyakazi kuhamishwa kutoka kituo kimoja Kwenda kingine ili kuimarisha utendaji na kuleta ufanisi. Tatizo kubwa ni kuwa wafanyakazi tunahamishwa bila kulipwa stahiki zetu.

Mkuu wa Rasilimali aliyepo hapo anatulazimisha Kwenda kwenye vituo vipya bila kulipwa anasema kama huna hela za kuhama nenda kakope Benki au mahali popote ili mradi uende unakotakiwa Kwenda. Na anatishia kuwa usipokwenda utaona kitakachokukuta ikiwa ni Pamoja na kuhamishiwa TAMISEMI.

Inaonekana kuw TAMISEMI ndio sehemu ya kupeleka watu wasiotakiwa.

Nina uhakika wewe Kamishna Mkuu hulijui hili kwa kuwa tunakufahamu kuwa wewe ni mtu wa haki na hupendi wafanyakazi wateseke.

Kwa mujibu wa utumishi, mfanyakazi anapohamishwa Kwenda kituo kipya cha kazi anatakiwa alipwe kama ifuatavyo:

1. Usafiri

Mfanyakazi anatakiwa apewe usafiri Kwenda kwenye kituo kipya cha kazi, yeye na mke au mume na Watoto wasiozidi 4 walio tegemezi kwa mfanyakazi. Kiutumishi, usafiri au nauli vinatakiwa kulipwa na kituo anachoondoka (kuhama) kabla mtumisji ahajaondoka Kwenda kwenye kituo kipya.

2. Fedha ya kufungashia mizigo (Disturbance allowance)

Hii ni aslimia 10 ya mshahara ghafi wa mwaka wa mfanyakazi, na inatakiwa ilipwe wiki mbili kabla ya mtumishi kuondoka kituo cha zamani.

3. Fedha za kujikimu

Mtumishi anapofika kwenye kituo kipya anatakiwa kulipwa fedha za kujikimu, kwa mujibu wa kanuni za utumishi

4. kusafirishiwa mizigo

Mtumishi anapohamishwa anatakiwa kusafirishiwa mizigo kwa mujibu wa stahiki zake.

Sasa Mheshimiwa Kamishna Mkuu, mtumishi anapoambiwa atafute fedha zake ahame kana kwamba alijihamisha mwenyewe, je hii ni haki ?.

Je Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mama Samia Suluhu Hassan anajua kuwa kuna uonevu wa namna hii TRA ? Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Khasim Majaliwa analijua hili, Mkuu wa Utumishi, na Waziri wa Fedha wanalijua hili ?

Au hawa maafisa wanatarajia tukapokee rushwa kwenye vituo vipya ? wanatarajia tukaibe ? Au wanakusudia nini kama sio kutukomoa.

Mheshimiwa Kamishna Mkuu najua hili liko kwenye uwezo wako, tafadhali fuatilia mwenyewe, waulize hata hao waliohamishwa, utaona hayo mauzamauza yanayofanywa na wasaidizi wako. Kuanzia Makamishna, Wakurugenzi husika na maafisa wao lao ni moja. Wanataka wewe uonekane mbaya kwa wafanyakazi wakati sisi tunajua sio hivyo.

Viongozi hawa sijui wamepataje nafasi hizi ambazo hawazimudu kabisa ?. Uongozi ni Pamoja na kutetea haki za wafanyakazi, jambo ambalo wasaidizi wako hawalifanyi.

Kuanzia idara ya Rasilimaliwatu, kuna huyu Renada ambaye ana majibu ya Manzese utafikiri hajasoma kabisa. Halafu n akule fedha pia ukumulike.

Mimi nimehamishiwa mikoa ya kusini, nina miezi miwili sijalipwa, wengine Mwezi mmoja, wengine wiki mbili watu tunaishi mahotelini. Jamani hii ni kinyume na haki za binadamu.

Nakuomba Mheshimiwa ufuatilie tupate malipo yetu na hawa dhulumati wapewe haki yao ya uonezi.

Nakuomba usianze kutafuta nani kaandika, angalia u ukweli uliopo.

Nimetumia njia hii kwa kuwa kuna ugumu mkubwa sana kukufikia, na victimisation lazima itokee kama nigekuja mwenyewe au hata kukutumia barua

Asante

Johnson
 
Tatizo hata nyinyi mfumo wenu wa utendaji wa kazi pia umejaa dhuluma kubwa.Huwa mnatutesa sana sisi tunaohangaika huku Jua kali. Umeona sasa madhara ya kudhulumiwa yanavyouma. Pole sana lakini liwe pia fundisho, haya maumivu unayoyapitia ndiyo sisi wa jua kali tunayaishi siku zote kupitia nyinyi wafanyakazi wa TRA.
 
Kwenye vituo vyote vipya mabosi walioko huko kawana mafungu ya kumlipa mtu zaidi ya kusema waliohamisha ni makao makuu kwa hiyo ndio watakaolipa. halau kwa nini nikamsumbue kiongozi wa kituo kipyya wakati kanuni ziko wazi ?
 
TRA pana uozo sana ni vile wengine wamechagua kuumiza Wananchi ili wapunguze stress zao na kuchukua rushwa wapo wanaofanya kazi vizuri ila kwa % kubwa ni rushwa kwa kwenda mbele wanatengeneza tatizo ili litatuliwe kwa rushwa...
 
Mheshimiwa Kamishna Mkuu wa TRA, nachukua fursa hii kukuomba uingilie kati uonevu unaofanywa na wasaidizi wako kwenye uhamisho unaoendelea sasa.

Nimefanya kazi TRA miaka mingi lakini hali iliyojitokeza sasa si ya kufumbia macho.

Uhamisho si jambo baya kwenye utumishi, ni kawaida mfanyakazi kuhamishwa kutoka kituo kimoja Kwenda kingine ili kuimarisha utendaji na kuleta ufanisi. Tatizo kubwa ni kuwa wafanyakazi tunahamishwa bila kulipwa stahiki zetu.

Mkuu wa Rasilimali aliyepo hapo anatulazimisha Kwenda kwenye vituo vipya bila kulipwa anasema kama huna hela za kuhama nenda kakope Benki au mahali popote ili mradi uende unakotakiwa Kwenda. Na anatishia kuwa usipokwenda utaona kitakachokukuta ikiwa ni Pamoja na kuhamishiwa TAMISEMI.

Inaonekana kuw TAMISEMI ndio sehemu ya kupeleka watu wasiotakiwa.

Nina uhakika wewe Kamishna Mkuu hulijui hili kwa kuwa tunakufahamu kuwa wewe ni mtu wa haki na hupendi wafanyakazi wateseke.

Kwa mujibu wa utumishi, mfanyakazi anapohamishwa Kwenda kituo kipya cha kazi anatakiwa alipwe kama ifuatavyo:

1. Usafiri

Mfanyakazi anatakiwa apewe usafiri Kwenda kwenye kituo kipya cha kazi, yeye na mke au mume na Watoto wasiozidi 4 walio tegemezi kwa mfanyakazi. Kiutumishi, usafiri au nauli vinatakiwa kulipwa na kituo anachoondoka (kuhama) kabla mtumisji ahajaondoka Kwenda kwenye kituo kipya.

2. Fedha ya kufungashia mizigo (Disturbance allowance)

Hii ni aslimia 10 ya mshahara ghafi wa mwaka wa mfanyakazi, na inatakiwa ilipwe wiki mbili kabla ya mtumishi kuondoka kituo cha zamani.

3. Fedha za kujikimu

Mtumishi anapofika kwenye kituo kipya anatakiwa kulipwa fedha za kujikimu, kwa mujibu wa kanuni za utumishi

4. kusafirishiwa mizigo

Mtumishi anapohamishwa anatakiwa kusafirishiwa mizigo kwa mujibu wa stahiki zake.

Sasa Mheshimiwa Kamishna Mkuu, mtumishi anapoambiwa atafute fedha zake ahame kana kwamba alijihamisha mwenyewe, je hii ni haki ?.

Je Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mama Samia Suluhu Hassan anajua kuwa kuna uonevu wa namna hii TRA ? Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Khasim Majaliwa analijua hili, Mkuu wa Utumishi, na Waziri wa Fedha wanalijua hili ?

Au hawa maafisa wanatarajia tukapokee rushwa kwenye vituo vipya ? wanatarajia tukaibe ? Au wanakusudia nini kama sio kutukomoa.

Mheshimiwa Kamishna Mkuu najua hili liko kwenye uwezo wako, tafadhali fuatilia mwenyewe, waulize hata hao waliohamishwa, utaona hayo mauzamauza yanayofanywa na wasaidizi wako. Kuanzia Makamishna, Wakurugenzi husika na maafisa wao lao ni moja. Wanataka wewe uonekane mbaya kwa wafanyakazi wakati sisi tunajua sio hivyo.

Viongozi hawa sijui wamepataje nafasi hizi ambazo hawazimudu kabisa ?. Uongozi ni Pamoja na kutetea haki za wafanyakazi, jambo ambalo wasaidizi wako hawalifanyi.

Kuanzia idara ya Rasilimaliwatu, kuna huyu Renada ambaye ana majibu ya Manzese utafikiri hajasoma kabisa. Halafu n akule fedha pia ukumulike.

Mimi nimehamishiwa mikoa ya kusini, nina miezi miwili sijalipwa, wengine Mwezi mmoja, wengine wiki mbili watu tunaishi mahotelini. Jamani hii ni kinyume na haki za binadamu.

Nakuomba Mheshimiwa ufuatilie tupate malipo yetu na hawa dhulumati wapewe haki yao ya uonezi.

Nakuomba usianze kutafuta nani kaandika, angalia u ukweli uliopo.

Nimetumia njia hii kwa kuwa kuna ugumu mkubwa sana kukufikia, na victimisation lazima itokee kama nigekuja mwenyewe au hata kukutumia barua

Asante

Johnson
Muosha huoshwaa

Mnadhulumu watuu sana kwa rushwa

Chuma Huliwa na chuma chenzake

Cha mtu huliwa na mtuu

Kwa hiyo kausha ivyoivyo uliwe na wewe na wenzako.

Mwisho Ndugu Alfayo Kidata taratibu za utumishi wa ummaa kiutendaji hatufanyii kazi mitandao ya kijamiii.

Huyu utumishi hana nidhamu ktk utumishi peleka huko wilaya ya Tanganyika
 
Tatizo hata nyinyi mfumo wenu wa utendaji wa kazi pia umejaa dhuluma kubwa.Huwa mnatutesa sana sisi tunaohangaika huku Jua kali. Umeona sasa madhara ya kudhulumiwa yanavyouma. Pole sana lakini liwe pia fundisho, haya maumivu unayoyapitia ndiyo sisi wa jua kali tunayaishi siku zote kupitia nyinyi wafanyakazi wa TRA.

Bwana johnson Mutakyamilwa Angalia huku mlivyo na mikono michafu
 
Sasa mkuu kwani si huwa ninakisikia TRA huwa mnahonga hadi HR ili wawape uhamisho muende kwenye vitengo mahususi na ili msiibue sintofahamu kwenye bajeti ya serikali huwa mnajigharamikia kuhama ili mchezo wenu usigundulike?Au imefika zamu yako ya kwenda pagumu una ulikuwa hujakusanya za kutosha ndo maana unaleta malalamiko?

Kama hii hoja yangu haina msingi nafikiri mods wanaweza kuifuta ila kwa wazoefu waliokaa TRA wanajua kuwa huwa kuna kubadilishana vituo kwa ajili ya kupokezana fursa.Sasa hio ni tofauti na kuhamishwa kituo.

By the way hii taarifa ni tetesi tu haina uhakika wa kweli kabisa so kama huna ushahidi chukulia kama stori ya kijiweni na kamishna wa TRA amlipe Johnson Mpunga wake wa kuhama maana kuwapa watumish STRESS nako kuna changia kufanya RUSHWA izidi kuenea ndani ya Mamlaka
 
Yaani hata TRA mnalalamika?.

Ndio maana wakati mwingine mnapunguzia machungu kwa sisi Wananchi.
 
Hahahahaj eti utapelekwa Tamisemi

Tena wanakutupa halmashauri ya namtumbo huko au mbinga sijui Nyasa Kule kwenye kona kabisa

Utachakaa u-smart wote kwisha mbwembwe na title za kupiga mzigo TRA kwishnei.
 
Back
Top Bottom