Stephano Mgendanyi
JF-Expert Member
- May 16, 2020
- 1,903
- 945
KIJIJI CHA WAKULIMA NA WAFUGAJI STADI CHAUNGANISHWA KWENYE BARABARA KUU
Kijiji cha Kinyang'erere ni moja ya vijiji vinne (4: Bugwema, Kinyang'erere, Masinono, Muhoji) vya Kata ya Bugwema ya Musoma Vijijini.
Vijiji vyote vinne (4) vimo ndani ya Bonde la Bungwema ambalo Serikali imepanga kujenga miundombimu ya kilimo cha umwagiliaji.
TARURA inafanya kazi kubwa na nzuri sana ya kujenga barabara (km 11), yenye madaraja mawili (2), kwenye mito miwili (Sijati & Nyamagusu) kwa ajili ya kukiunganisha Kijiji cha Kinyang'erere kwenye barabara kuu ya Murangi (Musoma Vijijini)-Bugwema-Masinono-Manyamanyama (Bunda)
Mazao makuu yanayolimwa Kijijini Kinyang'erere ni: mpunga, dengu, choroko, mahindi, maharage na alizeti
Mifugo muhimu ya Kijiji hiki ni ng'ombe, kondoo na mbuzi
Barabara hiyo ya kilomita 11 inaunganisha Wilaya za Musoma na Bunda kupitia Kijiji cha mpakani kiitwacho Karukekere (Mwibara, Bunda)
Tafadhali sikiliza CLIP/VIDEO iliyoambatanishwa hapa - shukrani nyingi mno kwa Serikali yetu.
Usisahau kutembelea TOVUTI ya Jimbo letu ambayo ni:
www.musomavijijini.or.tz
Ofisi ya Mbunge
Jimbo la Musoma Vijijini
www.musomavijijini.or.tz
Tarehe:
Alhamisi, 11.5.2023