mwanazuoni mgeni
JF-Expert Member
- Sep 11, 2016
- 1,943
- 1,734
mbeya
Karibu Buza mkuuMaisha Yako Na Yangu Ni sawa Lkn Let me Telling u Something Muda Mwingine Nibora Kuwa Pekeako Kuna Mengi Yanakupita Kuliko Kulazimisha Company Itakayo kuingiza Katika Matatizo
Sometimes mm Nikitoka Kazini Najikuta Sina Pakwenda Nalala tu Ndani
Inakera Lkn Bora Maana nikicheki Company Yangu Wengi Mbali Na Kuvaa Nakupendeza Hawana Future
Maisha Sio Kupendeza Mwili tu Hata Ubongo Unahitaji Kupendeza Pia
Ungekuwa DSM Basi Ningekuwa Nikikutembelea
But Never give up soma Mkuu
Sent using Jamii Forums mobile app
Sio lazima uwe na marafiki wengi ili ufanikiwe.Shikamooni wakubwa zangu humu ndani.
Mimi ni kijana wa miaka 19. Ninasumbuliwa na tatizo moja. Najiona kama vile nakua mwili tu lakini akili yangu bado ya kitoto.
Ni kwa kipindi kirefu sasa nimekuwa nikiishi peke yangu kuanzia nilipohitimu darasa la saba mpaka hivi sasa nipo kidato cha tano.
Nimesoma shule ya bweni ila nilipokuwa nikirudi likizo nilipendelea sana kukaa ndani (ndio akili yangu ilichonituma kwa wakati huo), hali iliyopelekea kupoteza marafiki zangu wengi wa shule ya msingi.
Bahati mbaya zaidi mitaa ninayoishi hakuna vijana wa rika langu. Hii imesababisha mara nyingi kuwa mpweke kitu ambacho nadhani kinaniathiri kisaikolojia.
Huwa nikipata pesa (kutoka kwa wazazi bado sijaanza kutengeneza pesa zangu mwenyewe ) huwa sivipi kipaumbele vitu kama mavazi yaani huwa natumia tu mpaka inaisha japo sina mavazi mengi (wazazi walishaacha kuninunulia nadhani kwa sababu ya umri wangu).
Yaani huwa hata nikiwaona madogo niliowaacha shule ya msingi naona wananizidi kimaisha.
Hata shuleni nako sikuwa mtu social sana hivyo sikupata marafiki wengi wapya. Huwa nawakumbuka sana wanafunzi wenzangu niliosoma nao shule ya msingi both boys and girls and actually nawapenda sana.
Huwa nawa search tu social media
bila wao kujua. Wachache nawapata naishia kuangalia tu picha zao lakini nashindwa kuwa approach kwani naona wamenizidi sana I mean wamekua.
Hapa nyumbani marafiki zangu wakubwa ni wadogo zangu tu yaani am very confused.
Nashindwa hata kujua wenzangu wanapigaga dili gani ili kujitengenezea pesa.
Yaani naathirika mpaka shuleni hasa hii A level nashindwa hata kwenda kudiscuss na mtu mambo yakinishinda.
I have lost a lot of people, friends, opportunities, time etc but I want to recover them.
Natamani sana kujenga upya maisha yangu, kuwa na marafiki wa kike na wa kiume wa rika langu nitakaoweza kushare nao mambo mbalimbali.
Naombeni mnisaidie wakubwa zangu nitaanza vipi? Nanyi vijana wenzangu wa miaka 19 au 20 huwa mnafanya nini likizo au mnakutanaga wapi? Nitawezaje kubadilika?
Im always confused and stressed about this mpaka huwa nahisi kurogwa au kuna mkono wa mtu kwenye maisha yangu.
May God will bless you for what you will contribute.
Mbeya sehemu gani
mbeya