Wakosoaji wa Serikali wanatumwa?

Wakosoaji wa Serikali wanatumwa?

Kwa hiyo waliuza mali ya taifa, kusaini mikataba mibovu, kufanya maamuzi ya kuitia serikali hasara si vibaraka!??? Tuache unafiki, penye ukweli tuwe wakweli. Nigger, puliizi!!
Nani aliyeuza mali ya Taifa?
 
MTU anaingia madarakani, anajidai yeye ni tajiri, anataka awauzie wazungu Mitumba..kwa dharau kabisa hataki hata kusafiri kwenda kuongea na wanaomdai..mwisho wa siku eti anawatuhumu kuwa hawafurahii misimamo yake (yeye kama nani???)

Wanachofanya ni kudai tu madai yao halali yaliyoidhinishwa na Mahakama... BASI

HAYA NDIYO MADHARA YA KUTUMIA NGUVU NYINGI KULIKO AKILI
Marekani na ubabe wake wa silahaa anakopa ...hebu jielimisheni kidogo
 
Ndugu Zitto uyasemayo ni ya kweli kabisa, but this has become the game of Tug Of War, hata wanaokosoa wapinzani wanaitwa wasaliti, wanajikomba, vilaza na matusi ya kila aina. Ushauri wangu ni kuwa wavumilivu NA kujaribu kubadisha tabia za kulumbana NA kuwa NA moyo wa kukubali mazuri ya mpizani
 
Fact number moja: Serikali haijawahi kupunguza madai ya deni walilowadai barrick/Accacia ...kama una sehemu ya Taarifa ya serikali inayoonesha hilo iweke hapa jamvini.

Kwa kiashiria hiki kidogo tu ni wazi unadhihirisha kuwa umetumwa kulaghai umma kwa manufaa yako na waliokutuma.

Mnatumwa ndio kwa kuwa hamjawahi kuhoji matatizo halisi ya watanzania na mmekua chanzo cha kuanzisha mijadala isiyokuwa na tija kwa maisha ya kila siku ya mtanzania....yaani mnaanzisha mijadala ya kitaifa katika interests za mabepari na wafabyabiashara walioliibia Taifa.

Ulipotaka Rais atangaze njaa ni janga la kitaifa na ukatuaminisha ni janga ulikuwa hujatumwa?
Sasa kama ukweli unaujua juu ya madeni hayo ya kubumba na kiakili ndogo simyatoe,
Ukitaka usiulizwe kasimamie mali za mke wako na wanao!
Mliingia madarakani na ushamba wa kijijini
Leo mnegeuza ofisi machinjio aibu yetu.
 
kusema trilion 1.5 zimeibwa na magufuli ni kutumwa?.
kusema ndege imekamatwa canada ni kutumwa?
tangu lini kiongozi aliyechaguliwa na watu awe.malaika? asihojiwe? akihojiwa watu wametumwa? kwa kipi ambacho hamjawagawia? mbona wakiwapa misaada mnachukua?
Mtukufu malaika toka chato ndiyo katumwa toka Burundi kuja kuifirisi Nchi, anachukua pesa BOT hovyo hovyo na kufanyia kazi za hovyo hovyo zisizo na tija kwa Taifa.
 
Wakosoaji wa Serikali wanatumwa?

Siku hizi ukisikiliza hotuba za Viongozi Wakuu wa Serikali ya Tanzania pamoja na maandiko ya Vyombo vya Habari vinavyoiunga mkono Serikali kama vile Jamvi la Habari, Habarileo, Uhuru nk utasikia au kusoma madai yanayojirudia rudia kuwa kuna Watanzania wanatumika na mataifa ya Nje kuidhuru nchi yetu. Madai haya yanayotolewa bila ushahidi wowote ni madai yanayoonyesha ni namna gani nchi yetu imeua kabisa utamaduni wa kukosoana.

Wakati wa mjadala wa mabadiliko makubwa ya sekta ya Madini aliyoyafanya Rais Magufuli kufuatia amri yake ya kuzuia kusafirisha makanikia, tuhuma dhidi ya baadhi yetu zilikuwa kubwa mno kiasi cha watu kuonekana wasaliti wa nchi yetu. Katika moja ya hotuba yake, Rais Magufuli alifikia hatua ya kusema kuwa ‘ msaliti dawa yake inajulikana ‘.

Haikuchukua muda Mbunge Tundu Lissu, aliyekuwa mmoja wa wakosoaji wakubwa wa Serikali alipigwa risasi na kukoswakoswa kupoteza maisha. Licha ya matusi yote tuliyotukanwa, madai ya $490bn ambayo Serikali iliyatoa kwa Kampuni ya Barrick yalishuka mpaka $300m ambazo hazijalipwa mpaka sasa na wala hazionekani kwenye vitabu vya Serikali kama Mapato tarajiwa ( receivables). Vijana wanatania mitandaoni kuwa tumetoka ahadi ya Noah kwa kila Mtanzania na kufikia ahadi ya Balimi 7 kwa kila Mtanzania. Hata hizo Balimi hazijapatikana.

Wakati wa mjadala wa Ndege yetu kukamatwa huko Canada, pia zilitengenezwa nadharia kuwa mimi na Tundu Lissu tumelipwa na mabeberu ili kuzuia ndege ile. Kampuni iliyowasilisha amri ya kushikilia ndege ile ililipuliwa na bomu na nchi kuingizwa kwenye taharuki bila sababu. Hatimaye Serikali imelipa zaidi TZS 60 Bilioni ili Ndege iweze kuletwa nchini. Wakosoaji wa Serikali walikosoa namna Serikali inajiendesha kana kwamba Tanzania ni kisiwa na madhara yake ni nchi kupata hasara kubwa Sana. Hivi sasa kuna kesi kadhaa Marekani na Uingereza dhidi ya Serikali yetu kutokana na mikataba mbalimbali ambayo Serikali imeshindwa kuiheshimu au Serikali ilifanya ubabe kuivunja bila kujali sheria za kimataifa. Jumla ya madai tunayodaiwa kwenye mahakama za nje ( ninayoyajua mimi na mengine kuthibitishwa na CAG kwenye Taarifa yake ya mwaka 2016/17 ) yanafika Dola za Kimarekani Bilioni 1.48 Sawa na Shilingi Trilioni 3.3 za Kitanzania [ Madai ya Standard Chartered Bank Hong Kong $614m+$148m, Madai ya Syimbion Power $600m, Madai ya Konoike $63m, Madai ya Airbus $59m ].

Hata sasa kwenye mjadala wa kutoonekana kwa matumizi ya TZS 1.5T Serikali imejaribu kutumia maneno hayo hayo ya kuwaita wakosoaji kuwa wametumwa. Majibu rasmi ya Serikali ndani ya Bunge yamewaita wakosoaji ‘ watu wasioitakia mema nchi yetu ‘. Rais naye alipokuwa anafungua tawi la Benki ya NMB Dodoma akasema ‘ watu wanatumwa na mabeberu ‘. Unachoshangaa ni Kwamba hoja hii ya 1.5T imetoka kwenye Ripoti ya CAG ambayo ndio mamlaka ya kikatiba kufanya Ukaguzi wa Fedha za Serikali. CAG ana mamlaka makubwa kiasi kwamba Rais hana mamlaka ya kumfukuza Kazi hata amchukie namna gani. Iweje utumie Ripoti ya CAG kuihoji Serikali uwe unatumwa na watu wa Nje?

Kwenye mjadala kuhusu zabuni ya pasi za kusafiria pia Gazeti la Jamhuri lilisakamwa na Gazeti la Jamvi kuwa wametumwa na mabeberu. Baadaye naona magazeti haya yalifanya mkataba wa amani ( ceasefire). Hata hivyo gazeti la Jamhuri lilikuwa linafanya Kazi yake ya kuhoji Serikali na kupasha Habari wasomaji wake.

Wakosoaji wa Serikali wanapohoji ni Kwa maslahi ya nchi na sio kwa kutumwa. Dhana kwamba watu wanatumwa ni dhana ambayo haina nguvu na inajaribu kuua Uhuru wa maoni na wajibu wa kukosoa. Kukimbilia kuita watu majina mabaya Kwa sababu ya kuhoji masuala ya Umma tena kwa ushahidi ni dalili za wenye mamlaka kukosa Majibu na hivyo kutumia nguvu dhidi ya wakosoaji. Nadharia kuwa ukosoaji ni kutumwa unaenda kinyume na Mwongozo wa CCM wa mwaka 1981 ambao ulijikita kwenye ‘ kukosoa na kujikosoa ‘ ili kujenga Taifa imara.

Marehemu Mzee Kingunge Ngombale Mwiru amenukuliwa na wanazuoni akieleza kuhusu Mwongozo wa CCM wa mwaka 1981 “ Wakati Mwongozo wa TANU wa 1971 ulijielekeza kwenye mapambano dhidi ya Ukoloni, Ukoloni-Mamboleo na Ubeberu ili kufanikisha Ukombozi wa Afrika na wa Mwafrika na kuweka mkakati wa ulinzi na usalama wa umma ili nchi iwe na uwezo wa kukabiliana na uvamizi wowote kutoka kwa ubeberu au na vibaraka vyake, Mwongozo wa 1981 umejikita katika kufanya uchambuzi kosoa wa kina na mpana juu ya hali ya kisiasa na kiuchumi iliyokuwepo nchini, hali ya maendeleo ya demokrasia nchini na ndani ya chama, n.k., na kutoa mapendekezo ya kuimarisha na kupanua demokrasia katika Chama na nchi”. Mwisho wa kunukuu. Inashangaza kuwa wana CCM wanaotawala sasa wanatafsiri ukosoaji kuwa ni uadui na kwenda kinyume kabisa na misingi ya Chama chao.

Kwa upande wa Chama ambacho mimi ni Kiongozi wake, Msingi wa kwanza Katika misingi kumi ni UZALENDO. Msingi huu unasema, nanukuu “ Uzalendo ndio moyo wa kuanzishwa kwa chama cha Wazalendo ikiwa ni tamko letu rasmi la kuipenda nchi yetu na utayari wa kuipigania na kuilinda. Ubora na umakini wa maamuzi yetu kama chama utapimwa kwa kuangalia ni namna gani maamuzi hayo yana faida kwa taifa letu na wananchi wake kwa leo na kesho”. Hivi sisi ACT Wazalendo kama Chama hufanya ukosoaji kwa kuzingatia maslahi ya Nchi yetu. Kila jambo tunalipima kwa kuangalia nchi inapata faida gani. Tulipoamua kukosoa takwimu za Serikali kuhusu GDP ( Pato la Taifa ) tulijua iwapo Serikali itaendelea na sera fyongo za Uchumi, Wananchi wataumia na nchi itaumia. Tangu tumetoa Tamko lile la Kamati Kuu Serikali imelegeza udhibiti wa ujazo wa Fedha kwenye Uchumi na ukuaji wake umefikia 8% kwa mujibu wa Taarifa za hivi karibuni za Benki Kuu.

Tulipoamua kuzungumzia soko la bidhaa za mbaazi, choroko nk sio kuwa tunainanga Serikali bali tunataka Serikali itimize wajibu wake Kwa raia kufuatia kuanguka kwa soko la mbaazi lenye thamani ya $250m ( zaidi TZS 500 Bilioni) kwa mwaka.

Tulipoamua kuchambua Taarifa ya CAG ya mwaka 2016/17 na uchambuzi uliofutia wa majibu ya Serikali kwa Hoja hiyo ya Ukaguzi lengo letu ni kuisimamia Serikali ambayo ndio wajibu wa Wabunge na Vyama vya siasa visivyo madarakani. Hatukutumwa bali tulijituma na kujiongeza kuonyesha kuwa Fedha za Umma hazisimamiwi vizuri na Serikali ya awamu ya 5 iliyo chini ya CCM.

Wakosoaji wa Serikali wanatimiza wajibu wao kama Wananchi. Hawatumwi na mabeberu. Kwa mujibu wa Sheria za nchi yetu kutumwa na mabeberu kuchafua sura ya nchi ni uasi na adhabu yake ni kifo. Serikali badala ya kulalamika tu kwenye mikutano Kuwa wakosoaji wake wanatumwa, ichukue hatua za kisheria kuwashtaki hao wanaodhaniwa kutumwa ili wakosoaji wa kweli waendelee na wajibu wao. Tuhuma za kutumwa hakiwezi kuwa kichaka cha kujifichia na kukwepa kujibu Hoja za Msingi.

Wananchi sasa waanze kukataa nadharia za kitoto, zilizopitwa na wakati Kuwa wakosoaji wa Serikali wametumwa. Wananchi wahoji ushahidi wa madai hayo. Wasikubali tuhuma hewa zinazotolewa ili kuficha ukweli wa masuala yanayoibuliwa. Serikali ina Vyombo vyenye uwezo mkubwa wa kuchunguza, Wananchi watake ushahidi kutoka vyombo Hivi. Propaganda za ‘ wanatumiwa ‘ zikiachwa tu watu wataumia. Tutajenga Taifa la hovyo, la watu wasiohoji, wanaodanganywa tu.

Kwa mwananchi, hakuna uzalendo bora zaidi kuliko uzalendo wa kuikosoa Serikali ya nchi yako. Uzalendo mkubwa zaidi ni kuitetea nchi yako, si Serikali! NCHI yako.
Juhudi kubwa za kizalendo zinazofanywa na vyama vya mageuzi zinafifishwa, hazionekani, na huenda zisiungwe mkono na walio wengi kutokana na sababu zifuatazo:
1. Kutokupata coverage halisi. Vyombo vya habari karibu vyote au haviripoti michango yenu, au vinaripoti katika njia ambayo ni hasi sana au vinapotosha kabisa michango yenu. Sasa hivi mtu akitaka kujua mchango wa Zitto ni lazima atafute kwenye mitandao
2. Kuondolewa kwa mijadala ya kisiasa kinyemela kwenye TV na radio inayowashirikisha wanamageuzi. Zamani tulizoea kumuona Dr Slaa akipambanishwa na wana CCM kwenye kipima joto. Mwangwi wa hiyo mijadala uliibua tafakuri kubwa kwa hadhira na kupelekea kujadili mambo ya kitaifa yenye tija. Sasa hivi mijadala ni mpira tu. Bongo za watoto wetu zinafubaa, huko tuendako watoto wetu hawatakuwa na uwezo wa kujenga hoja
3. Kuzuiwa kwa mijadala ya wazi bungeni na badala yake kuoneshwa upande wa serikali tu
4. kamata kamata ya wapinzani na kuwafungulia kesi kila kukicha kunafanya watu waanze kupoteza imani nao. Maana hakuna mahali ambapo wanapata nafasi ya kutosha ya kujieleza kinachoendelea.
5. Tuhuma za biashara ya kununua wadiwani na wabunge kukosa coverage halisi, kutokujadiliwa kwenye vyombo vya habari na kupotoshwa ati wanaunga mkono juhudi za mh Rais
Safari ina kiza kikubwa
 
Kukosoa sio tatizo, Kama unakosoa Kwa staha na kuleta way forward, sio majungu na kupakaziana
Make tunajenga nyumba moja, madudu yalishafanyika, Wala hayakuanzia Kwa magufuli, unadhani angefanya Nini? Hi nchi ilishafikia pabaya, ilihitaji mtu Kama huyu kuinyoosha
 
Vyama vya upinzani badi haviko katika core ya kumkombia mtanzania, wanashindwa kubadilisha tactical approach, kaxi ni kuona mabovu tu, Kama watoto na peremende, as if wangekuwa wao Mambo yote yangekuwa sawia, ndugu tukae meza moja nyumba yet tupate kuinua
 
Hahaaaaa sijaimalizia kusoma ila nilipofikia sehemu ya Noah zetu mpaka Balimi nikakata tamaa na maendeleo ya nchi hii tukijumlisha na ndege saba mpya zinakuja
 
Wakosoaji wa Serikali wanatumwa?

Siku hizi ukisikiliza hotuba za Viongozi Wakuu wa Serikali ya Tanzania pamoja na maandiko ya Vyombo vya Habari vinavyoiunga mkono Serikali kama vile Jamvi la Habari, Habarileo, Uhuru nk utasikia au kusoma madai yanayojirudia rudia kuwa kuna Watanzania wanatumika na mataifa ya Nje kuidhuru nchi yetu. Madai haya yanayotolewa bila ushahidi wowote ni madai yanayoonyesha ni namna gani nchi yetu imeua kabisa utamaduni wa kukosoana.

Wakati wa mjadala wa mabadiliko makubwa ya sekta ya Madini aliyoyafanya Rais Magufuli kufuatia amri yake ya kuzuia kusafirisha makanikia, tuhuma dhidi ya baadhi yetu zilikuwa kubwa mno kiasi cha watu kuonekana wasaliti wa nchi yetu. Katika moja ya hotuba yake, Rais Magufuli alifikia hatua ya kusema kuwa ‘ msaliti dawa yake inajulikana ‘.

Haikuchukua muda Mbunge Tundu Lissu, aliyekuwa mmoja wa wakosoaji wakubwa wa Serikali alipigwa risasi na kukoswakoswa kupoteza maisha. Licha ya matusi yote tuliyotukanwa, madai ya $490bn ambayo Serikali iliyatoa kwa Kampuni ya Barrick yalishuka mpaka $300m ambazo hazijalipwa mpaka sasa na wala hazionekani kwenye vitabu vya Serikali kama Mapato tarajiwa ( receivables). Vijana wanatania mitandaoni kuwa tumetoka ahadi ya Noah kwa kila Mtanzania na kufikia ahadi ya Balimi 7 kwa kila Mtanzania. Hata hizo Balimi hazijapatikana.

Wakati wa mjadala wa Ndege yetu kukamatwa huko Canada, pia zilitengenezwa nadharia kuwa mimi na Tundu Lissu tumelipwa na mabeberu ili kuzuia ndege ile. Kampuni iliyowasilisha amri ya kushikilia ndege ile ililipuliwa na bomu na nchi kuingizwa kwenye taharuki bila sababu. Hatimaye Serikali imelipa zaidi TZS 60 Bilioni ili Ndege iweze kuletwa nchini. Wakosoaji wa Serikali walikosoa namna Serikali inajiendesha kana kwamba Tanzania ni kisiwa na madhara yake ni nchi kupata hasara kubwa Sana. Hivi sasa kuna kesi kadhaa Marekani na Uingereza dhidi ya Serikali yetu kutokana na mikataba mbalimbali ambayo Serikali imeshindwa kuiheshimu au Serikali ilifanya ubabe kuivunja bila kujali sheria za kimataifa. Jumla ya madai tunayodaiwa kwenye mahakama za nje ( ninayoyajua mimi na mengine kuthibitishwa na CAG kwenye Taarifa yake ya mwaka 2016/17 ) yanafika Dola za Kimarekani Bilioni 1.48 Sawa na Shilingi Trilioni 3.3 za Kitanzania [ Madai ya Standard Chartered Bank Hong Kong $614m+$148m, Madai ya Syimbion Power $600m, Madai ya Konoike $63m, Madai ya Airbus $59m ].

Hata sasa kwenye mjadala wa kutoonekana kwa matumizi ya TZS 1.5T Serikali imejaribu kutumia maneno hayo hayo ya kuwaita wakosoaji kuwa wametumwa. Majibu rasmi ya Serikali ndani ya Bunge yamewaita wakosoaji ‘ watu wasioitakia mema nchi yetu ‘. Rais naye alipokuwa anafungua tawi la Benki ya NMB Dodoma akasema ‘ watu wanatumwa na mabeberu ‘. Unachoshangaa ni Kwamba hoja hii ya 1.5T imetoka kwenye Ripoti ya CAG ambayo ndio mamlaka ya kikatiba kufanya Ukaguzi wa Fedha za Serikali. CAG ana mamlaka makubwa kiasi kwamba Rais hana mamlaka ya kumfukuza Kazi hata amchukie namna gani. Iweje utumie Ripoti ya CAG kuihoji Serikali uwe unatumwa na watu wa Nje?

Kwenye mjadala kuhusu zabuni ya pasi za kusafiria pia Gazeti la Jamhuri lilisakamwa na Gazeti la Jamvi kuwa wametumwa na mabeberu. Baadaye naona magazeti haya yalifanya mkataba wa amani ( ceasefire). Hata hivyo gazeti la Jamhuri lilikuwa linafanya Kazi yake ya kuhoji Serikali na kupasha Habari wasomaji wake.

Wakosoaji wa Serikali wanapohoji ni Kwa maslahi ya nchi na sio kwa kutumwa. Dhana kwamba watu wanatumwa ni dhana ambayo haina nguvu na inajaribu kuua Uhuru wa maoni na wajibu wa kukosoa. Kukimbilia kuita watu majina mabaya Kwa sababu ya kuhoji masuala ya Umma tena kwa ushahidi ni dalili za wenye mamlaka kukosa Majibu na hivyo kutumia nguvu dhidi ya wakosoaji. Nadharia kuwa ukosoaji ni kutumwa unaenda kinyume na Mwongozo wa CCM wa mwaka 1981 ambao ulijikita kwenye ‘ kukosoa na kujikosoa ‘ ili kujenga Taifa imara.

Marehemu Mzee Kingunge Ngombale Mwiru amenukuliwa na wanazuoni akieleza kuhusu Mwongozo wa CCM wa mwaka 1981 “ Wakati Mwongozo wa TANU wa 1971 ulijielekeza kwenye mapambano dhidi ya Ukoloni, Ukoloni-Mamboleo na Ubeberu ili kufanikisha Ukombozi wa Afrika na wa Mwafrika na kuweka mkakati wa ulinzi na usalama wa umma ili nchi iwe na uwezo wa kukabiliana na uvamizi wowote kutoka kwa ubeberu au na vibaraka vyake, Mwongozo wa 1981 umejikita katika kufanya uchambuzi kosoa wa kina na mpana juu ya hali ya kisiasa na kiuchumi iliyokuwepo nchini, hali ya maendeleo ya demokrasia nchini na ndani ya chama, n.k., na kutoa mapendekezo ya kuimarisha na kupanua demokrasia katika Chama na nchi”. Mwisho wa kunukuu. Inashangaza kuwa wana CCM wanaotawala sasa wanatafsiri ukosoaji kuwa ni uadui na kwenda kinyume kabisa na misingi ya Chama chao.

Kwa upande wa Chama ambacho mimi ni Kiongozi wake, Msingi wa kwanza Katika misingi kumi ni UZALENDO. Msingi huu unasema, nanukuu “ Uzalendo ndio moyo wa kuanzishwa kwa chama cha Wazalendo ikiwa ni tamko letu rasmi la kuipenda nchi yetu na utayari wa kuipigania na kuilinda. Ubora na umakini wa maamuzi yetu kama chama utapimwa kwa kuangalia ni namna gani maamuzi hayo yana faida kwa taifa letu na wananchi wake kwa leo na kesho”. Hivi sisi ACT Wazalendo kama Chama hufanya ukosoaji kwa kuzingatia maslahi ya Nchi yetu. Kila jambo tunalipima kwa kuangalia nchi inapata faida gani. Tulipoamua kukosoa takwimu za Serikali kuhusu GDP ( Pato la Taifa ) tulijua iwapo Serikali itaendelea na sera fyongo za Uchumi, Wananchi wataumia na nchi itaumia. Tangu tumetoa Tamko lile la Kamati Kuu Serikali imelegeza udhibiti wa ujazo wa Fedha kwenye Uchumi na ukuaji wake umefikia 8% kwa mujibu wa Taarifa za hivi karibuni za Benki Kuu.

Tulipoamua kuzungumzia soko la bidhaa za mbaazi, choroko nk sio kuwa tunainanga Serikali bali tunataka Serikali itimize wajibu wake Kwa raia kufuatia kuanguka kwa soko la mbaazi lenye thamani ya $250m ( zaidi TZS 500 Bilioni) kwa mwaka.

Tulipoamua kuchambua Taarifa ya CAG ya mwaka 2016/17 na uchambuzi uliofutia wa majibu ya Serikali kwa Hoja hiyo ya Ukaguzi lengo letu ni kuisimamia Serikali ambayo ndio wajibu wa Wabunge na Vyama vya siasa visivyo madarakani. Hatukutumwa bali tulijituma na kujiongeza kuonyesha kuwa Fedha za Umma hazisimamiwi vizuri na Serikali ya awamu ya 5 iliyo chini ya CCM.

Wakosoaji wa Serikali wanatimiza wajibu wao kama Wananchi. Hawatumwi na mabeberu. Kwa mujibu wa Sheria za nchi yetu kutumwa na mabeberu kuchafua sura ya nchi ni uasi na adhabu yake ni kifo. Serikali badala ya kulalamika tu kwenye mikutano Kuwa wakosoa. Leji wake wanatumwa, ichukue hatua za kisheria kuwashtaki hao wanaodhaniwa kutumwa ili wakosoaji wa kweli waendelee na wajibu wao. Tuhuma za kutumwa hakiwezi kuwa kichaka cha kujifichia na kukwepa kujibu Hoja za Msingi.

Wananchi sasa waanze kukataa nadharia za kitoto, zilizopitwa na wakati Kuwa wakosoaji wa Serikali wametumwa. Wananchi wahoji ushahidi wa madai hayo. Wasikubali tuhuma hewa zinazotolewa ili kuficha ukweli wa masuala yanayoibuliwa. Serikali ina Vyombo vyenye uwezo mkubwa wa kuchunguza, Wananchi watake ushahidi kutoka vyombo Hivi. Propaganda za ‘ wanatumiwa ‘ zikiachwa tu watu wataumia. Tutajenga Taifa la hovyo, la watu wasiohoji, wanaodanganywa tu.

Kwa mwananchi, hakuna uzalendo bora zaidi kuliko uzalendo wa kuikosoa Serikali ya nchi yako. Uzalendo mkubwa zaidi ni kuitetea nchi yako, si Serikali! NCHI yako.
Zito Kabwe at his best. Let truth be told
 
Juhudi kubwa za kizalendo zinazofanywa na vyama vya mageuzi zinafifishwa, hazionekani, na huenda zisiungwe mkono na walio wengi kutokana na sababu zifuatazo:
1. Kutokupata coverage halisi. Vyombo vya habari karibu vyote au haviripoti michango yenu, au vinaripoti katika njia ambayo ni hasi sana au vinapotosha kabisa michango yenu. Sasa hivi mtu akitaka kujua mchango wa Zitto ni lazima atafute kwenye mitandao
2. Kuondolewa kwa mijadala ya kisiasa kinyemela kwenye TV na radio inayowashirikisha wanamageuzi. Zamani tulizoea kumuona Dr Slaa akipambanishwa na wana CCM kwenye kipima joto. Mwangwi wa hiyo mijadala uliibua tafakuri kubwa kwa hadhira na kupelekea kujadili mambo ya kitaifa yenye tija. Sasa hivi mijadala ni mpira tu. Bongo za watoto wetu zinafubaa, huko tuendako watoto wetu hawatakuwa na uwezo wa kujenga hoja
3. Kuzuiwa kwa mijadala ya wazi bungeni na badala yake kuoneshwa upande wa serikali tu
4. kamata kamata ya wapinzani na kuwafungulia kesi kila kukicha kunafanya watu waanze kupoteza imani nao. Maana hakuna mahali ambapo wanapata nafasi ya kutosha ya kujieleza kinachoendelea.
5. Tuhuma za biashara ya kununua wadiwani na wabunge kukosa coverage halisi, kutokujadiliwa kwenye vyombo vya habari na kupotoshwa ati wanaunga mkono juhudi za mh Rais
Safari ina kiza kikubwa
Since kweli unayo sema, haki ya kutofautiana hoja haijapotea, badi hata jamii forum ngefungiwa
 
Ni stupidity kuona mtu kazi yake kutafuta makosa ya serikali tu na kukosoa halafu hakuna zuri analoliona la serikali. Hata kama ni upinzani,hamna jambo kama hili analofanya zito na genge lake.
Zito amesema sawa, lakini upinzani wajipange upya, game limebadilika
 
Kukosoa sio tatizo,je mmewahi kupongeza pia?!

Au hii serikali hamna jema ililofanya?
 
Washirika gani wa Maendeleo unaowataka wewe?
Kama baadhi wa Wapinzani walipambana mpaka kupata Wafadhiri wa miradi flani ya Maendeleo na walio kwenye Madaraka wakazuia!! Je! Unataka ushirika gani wa Kimaendeleo?
Hukusikia Malalamiko ya Meya wa UBUNGO???
 
Zitto H. Polepole alishakwambia 2020 katafute kazi ya kufanya, labda Ridhwani Kikwete au Mangi Kimambi watakupa kazi lkn Bunge letu sahau, haurudi!

2025-2025 say no Mafisadi, no Usaliti!

Zito Kabwe, Tundu Lisu &Co. Out!
Wasiporudi bungeni ndiyo watashindwa kuwahoji zilipo 1.5 trln?
 
Juhudi kubwa za kizalendo zinazofanywa na vyama vya mageuzi zinafifishwa, hazionekani, na huenda zisiungwe mkono na walio wengi kutokana na sababu zifuatazo:
1. Kutokupata coverage halisi. Vyombo vya habari karibu vyote au haviripoti michango yenu, au vinaripoti katika njia ambayo ni hasi sana au vinapotosha kabisa michango yenu. Sasa hivi mtu akitaka kujua mchango wa Zitto ni lazima atafute kwenye mitandao
2. Kuondolewa kwa mijadala ya kisiasa kinyemela kwenye TV na radio inayowashirikisha wanamageuzi. Zamani tulizoea kumuona Dr Slaa akipambanishwa na wana CCM kwenye kipima joto. Mwangwi wa hiyo mijadala uliibua tafakuri kubwa kwa hadhira na kupelekea kujadili mambo ya kitaifa yenye tija. Sasa hivi mijadala ni mpira tu. Bongo za watoto wetu zinafubaa, huko tuendako watoto wetu hawatakuwa na uwezo wa kujenga hoja
3. Kuzuiwa kwa mijadala ya wazi bungeni na badala yake kuoneshwa upande wa serikali tu
4. kamata kamata ya wapinzani na kuwafungulia kesi kila kukicha kunafanya watu waanze kupoteza imani nao. Maana hakuna mahali ambapo wanapata nafasi ya kutosha ya kujieleza kinachoendelea.
5. Tuhuma za biashara ya kununua wadiwani na wabunge kukosa coverage halisi, kutokujadiliwa kwenye vyombo vya habari na kupotoshwa ati wanaunga mkono juhudi za mh Rais
Safari ina kiza kikubwa
Mtukufu malaika toka chato na Naibu Rais Maliyamungu Bashite wanatumia katiba ya marehemu idd na Mabutu kuitawala Tanzania.
 
Back
Top Bottom