Wakosoaji wa Serikali wanatumwa?

Wakosoaji wa Serikali wanatumwa?

Na watetezi wa serikali pia wanatumwa
Watetezi wa CCM na serikali ni Tenda kapewa Le mutuz, Cyprian msiba na Jerry muro ndiyo wameajiri vijana kibao wajinga wajinga kwa kazi ya kuitetea serikali, ni kweli wametumwa na serikali na wao wamewatuma vijana wao. Ni matumizi mabaya ya pesa za Umma, le mutuz kubwa jinga na wenzake kulipwa pesa za Umma kwa kazi ya kudhoofisha, kudidimiza Demokrasia ni ufujaji wa pesa za walipa kodi, ni Ufisadi mkubwa sana.
 
Wasukuma wawili washamba toka kolomije na chato wanatumia katiba za madikteta kuitawala Nchi kidikteta, katiba ya marehemu Mabutu na idd Amin Dada za enzi ya Zaire na uganda miaka 1971-79 ndiyo wanatumia kuitawala Tanzania sasa, Tabia zote mbovu wame-copy humo zikiwemo za kujenga viwanja vya ndege vijijini chato kama marehemu Mabutu alivyojenga kijijini kwao, pia wane-copy Tabia za kubadili Gavana Bank kuu pindi akigoma kutoa pesa hovyo hovyo pasipo idhini ya Bunge, sasa wamepachika Gavana wao BOT wanachota pesa hovyo hovyo mda wote wakitaka, hawataki kutumia katiba ya Tanzania maana wanajua itawazuia kuchota pesa hovyo hovyo kwa kazi za hovyo hovyo za kuwabambikia kesi, kuwapiga Risasi, kuwafunga jela Wapinzani na ujinga mwingineo mwingi ikiwemo kuwanunua wabunge, madiwani na kurudia chaguzi kwa gharama kubwa.

Kwa kweli kazi tunayo. Mimi huwa nikiwaza ujinga huu naona heri alqaida na ISIS wanaojilipua kuliko watz tunavyoishi kama kondoo wanaoelekea machinjoni kwa dhuluma hizi
 
Kukosoa dola si uhaini. Ni kuenda njia potofu, kujua unayofanya yana dosari, ndiyo msingi wa kuhofu kukosolewa. Msimamizi mkuu wa matatizo yote ya nchi yetu ni katiba. Katiba iliopo bila kubadilishwa itaidumaza zaidi nchi hii.
 
Hawapendi kukosolewa ili waendelee kutenda maovu
 
Watanzania wanapenda bongo tambarale...wanalia sababu wachache mirija imekatwa.

Kama tulisomea kuiba kwa kalamu
 
Ukiona mtu kila siku yeye ni kukosoa tu ujue huyo ni adui wa maendeleo.

Wapinzani wanatakiwa kuwa washirika wa maendeleo sio maadui. Hawatakiwa kukosoa tu kila kitu. Wanatakiwa kukosoa kwa malengo ya kuboresha.

Kwa hiyo kukosoa wizi wa 1.5trilion ni uadui wa maendeleo? We mbumbumbu na kilaza umetoka wapi huku jamvi la GT.
 
Watanzania wanapenda bongo tambarale...wanalia sababu wachache mirija imekatwa.

Kama tulisomea kuiba kwa kalamu
Umesoma wapi? Kiswahili chenyewe hujuia kuandika? Utamwibia nani kwa mbinu hiyo zaidi ya kula pesa za Umma kwa kazi haramu za kudhoofisha kukandamiza Demokrasia na kuwabambikia kesi, kuwapiga Risasi na kuwafunga jela Wapinzani.
 
Ukiona mtu kila siku yeye ni kukosoa tu ujue huyo ni adui wa maendeleo.

Wapinzani wanatakiwa kuwa washirika wa maendeleo sio maadui. Hawatakiwa kukosoa tu kila kitu. Wanatakiwa kukosoa kwa malengo ya kuboresha.
Sasa kama mtu kakosea tangu mwanzo na anaendelea kukosea ..utaboresha wapi?
 
Haijawahi tokea nchi ikapata Rais malaika kama huyu. Hahaaa, tuliingizwa chaka. Ni kiongozi dhaifu, mwoga na asiyejiamiji. Hana kabisa maono. Anaongoza kwa mihemko na mabavu tuu.
Kaifanya nchi ya kisenge mno
 
Mtukufu malaika toka chato anatawala Nchi kwa kutumia katiba ya marehemu idd Amin Dada na katiba ya marehemu Mabutu wa Zaire, Tabia zao mbovu na mbaya zote wame-copy ikiwemo kujenga viwanja vya ndege vijijini kwao na kuwafukuza Gavana wa Bank kuu na kuwaka Gavana wao wapate kuiba pesa kirahisi zaidi kama wanavyofanya sasa na Naibu Rais Maliyamungu Bashite
 
Ukiona mtu kila siku yeye ni kukosoa tu ujue huyo ni adui wa maendeleo.

Wapinzani wanatakiwa kuwa washirika wa maendeleo sio maadui. Hawatakiwa kukosoa tu kila kitu. Wanatakiwa kukosoa kwa malengo ya kuboresha.
ndo wanachofanya wanakosoa ili mbadilike mnaua hii kantri
 
Hasa huyu zitto anamangamanga tu hana pa kushika, alishajua watanzania wengi hawafuatilii vitu aidha kwa kutokujua au kwa uvivu na dharau akachukulia advantage ya kutaka kutuvuruga na kujifanya anajua vitu vingi. Nilishaligundua hili jamaa ni poyoyo tena zero brain basi tu anatumia mwanya uliopo kwa watanzania. Jamaa linahangaika tu saa hizi kwani hata kwenye chama chake kabaki peke yake hana pa kushika, hela ngumu na mke alishamjulisha ataishi kama malaika. Na bado na ukishaukosa tena ubunge 2020 ndio utachizika zaidi ya hapa. Sijawahi ona cha maana unachoongea, kutwa kujisifia mwenyekiti wa PAC miaka 8, sijui nani sijui nani. Toa basi hata hesabu za chama chako kwa CAG hutaki tukueleweje?? Tafuta kazi nyingine 2020, na utabaki na hii mipoyoyo michache inayowafuata kama minyumbu ambayo itaishia kuliwa na sima na chui. Kweli unatumika, na yule changu wenu wa marekani Mungu saidia hamkuweza kuleta fujo kwenye nchi yetu maana watanzania wamejielewa na hawakutaka machafuko. Mnawashinikiza kwenye mitandao nyie mmekumbajia mapaja chumbani. Anzisha movement halafu tukuone mbele na uso wako uliochoka.
 
Fact number moja: Serikali haijawahi kupunguza madai ya deni walilowadai barrick/Accacia ...kama una sehemu ya Taarifa ya serikali inayoonesha hilo iweke hapa jamvini.

Kwa kiashiria hiki kidogo tu ni wazi unadhihirisha kuwa umetumwa kulaghai umma kwa manufaa yako na waliokutuma.

Mnatumwa ndio kwa kuwa hamjawahi kuhoji matatizo halisi ya watanzania na mmekua chanzo cha kuanzisha mijadala isiyokuwa na tija kwa maisha ya kila siku ya mtanzania....yaani mnaanzisha mijadala ya kitaifa katika interests za mabepari na wafabyabiashara walioliibia Taifa.

Ulipotaka Rais atangaze njaa ni janga la kitaifa na ukatuaminisha ni janga ulikuwa hujatumwa?
Mi huwa ninamfagilia Zito maana he is a critical thinker.
Critisms set your brains searching for want of appropriate answers.
Mtu ambaye hapendi kuwa ctiticised hajiamini, he is weak upstairs.
Mike Zuckerberg wa FACEBOOK, kijana mwenye akili sana, lakini commoners wamemtight kwa maswali logical na ya kiusalama.
Amekubali kukosolewa na kujirekebisha.
Tusiwe na escapist mentality juu ya kukosolewa, ni kwa ajili ya Tanzania yetu sote.
 
Zitto H. Polepole alishakwambia 2020 katafute kazi ya kufanya, labda Ridhwani Kikwete au Mangi Kimambi watakupa kazi lkn Bunge letu sahau, haurudi!

2025-2025 say no Mafisadi, no Usaliti!

Zito Kabwe, Tundu Lisu &Co. Out!

Akiludi au asipoludi wewe unafaidika na nini?
 
Wakosoaji wa Serikali wanatumwa?

Siku hizi ukisikiliza hotuba za Viongozi Wakuu wa Serikali ya Tanzania pamoja na maandiko ya Vyombo vya Habari vinavyoiunga mkono Serikali kama vile Jamvi la Habari, Habarileo, Uhuru nk utasikia au kusoma madai yanayojirudia rudia kuwa kuna Watanzania wanatumika na mataifa ya Nje kuidhuru nchi yetu. Madai haya yanayotolewa bila ushahidi wowote ni madai yanayoonyesha ni namna gani nchi yetu imeua kabisa utamaduni wa kukosoana.

Wakati wa mjadala wa mabadiliko makubwa ya sekta ya Madini aliyoyafanya Rais Magufuli kufuatia amri yake ya kuzuia kusafirisha makanikia, tuhuma dhidi ya baadhi yetu zilikuwa kubwa mno kiasi cha watu kuonekana wasaliti wa nchi yetu. Katika moja ya hotuba yake, Rais Magufuli alifikia hatua ya kusema kuwa ‘ msaliti dawa yake inajulikana ‘.

Haikuchukua muda Mbunge Tundu Lissu, aliyekuwa mmoja wa wakosoaji wakubwa wa Serikali alipigwa risasi na kukoswakoswa kupoteza maisha. Licha ya matusi yote tuliyotukanwa, madai ya $490bn ambayo Serikali iliyatoa kwa Kampuni ya Barrick yalishuka mpaka $300m ambazo hazijalipwa mpaka sasa na wala hazionekani kwenye vitabu vya Serikali kama Mapato tarajiwa ( receivables). Vijana wanatania mitandaoni kuwa tumetoka ahadi ya Noah kwa kila Mtanzania na kufikia ahadi ya Balimi 7 kwa kila Mtanzania. Hata hizo Balimi hazijapatikana.

Wakati wa mjadala wa Ndege yetu kukamatwa huko Canada, pia zilitengenezwa nadharia kuwa mimi na Tundu Lissu tumelipwa na mabeberu ili kuzuia ndege ile. Kampuni iliyowasilisha amri ya kushikilia ndege ile ililipuliwa na bomu na nchi kuingizwa kwenye taharuki bila sababu. Hatimaye Serikali imelipa zaidi TZS 60 Bilioni ili Ndege iweze kuletwa nchini. Wakosoaji wa Serikali walikosoa namna Serikali inajiendesha kana kwamba Tanzania ni kisiwa na madhara yake ni nchi kupata hasara kubwa Sana. Hivi sasa kuna kesi kadhaa Marekani na Uingereza dhidi ya Serikali yetu kutokana na mikataba mbalimbali ambayo Serikali imeshindwa kuiheshimu au Serikali ilifanya ubabe kuivunja bila kujali sheria za kimataifa. Jumla ya madai tunayodaiwa kwenye mahakama za nje ( ninayoyajua mimi na mengine kuthibitishwa na CAG kwenye Taarifa yake ya mwaka 2016/17 ) yanafika Dola za Kimarekani Bilioni 1.48 Sawa na Shilingi Trilioni 3.3 za Kitanzania [ Madai ya Standard Chartered Bank Hong Kong $614m+$148m, Madai ya Syimbion Power $600m, Madai ya Konoike $63m, Madai ya Airbus $59m ].

Hata sasa kwenye mjadala wa kutoonekana kwa matumizi ya TZS 1.5T Serikali imejaribu kutumia maneno hayo hayo ya kuwaita wakosoaji kuwa wametumwa. Majibu rasmi ya Serikali ndani ya Bunge yamewaita wakosoaji ‘ watu wasioitakia mema nchi yetu ‘. Rais naye alipokuwa anafungua tawi la Benki ya NMB Dodoma akasema ‘ watu wanatumwa na mabeberu ‘. Unachoshangaa ni Kwamba hoja hii ya 1.5T imetoka kwenye Ripoti ya CAG ambayo ndio mamlaka ya kikatiba kufanya Ukaguzi wa Fedha za Serikali. CAG ana mamlaka makubwa kiasi kwamba Rais hana mamlaka ya kumfukuza Kazi hata amchukie namna gani. Iweje utumie Ripoti ya CAG kuihoji Serikali uwe unatumwa na watu wa Nje?

Kwenye mjadala kuhusu zabuni ya pasi za kusafiria pia Gazeti la Jamhuri lilisakamwa na Gazeti la Jamvi kuwa wametumwa na mabeberu. Baadaye naona magazeti haya yalifanya mkataba wa amani ( ceasefire). Hata hivyo gazeti la Jamhuri lilikuwa linafanya Kazi yake ya kuhoji Serikali na kupasha Habari wasomaji wake.

Wakosoaji wa Serikali wanapohoji ni Kwa maslahi ya nchi na sio kwa kutumwa. Dhana kwamba watu wanatumwa ni dhana ambayo haina nguvu na inajaribu kuua Uhuru wa maoni na wajibu wa kukosoa. Kukimbilia kuita watu majina mabaya Kwa sababu ya kuhoji masuala ya Umma tena kwa ushahidi ni dalili za wenye mamlaka kukosa Majibu na hivyo kutumia nguvu dhidi ya wakosoaji. Nadharia kuwa ukosoaji ni kutumwa unaenda kinyume na Mwongozo wa CCM wa mwaka 1981 ambao ulijikita kwenye ‘ kukosoa na kujikosoa ‘ ili kujenga Taifa imara.

Marehemu Mzee Kingunge Ngombale Mwiru amenukuliwa na wanazuoni akieleza kuhusu Mwongozo wa CCM wa mwaka 1981 “ Wakati Mwongozo wa TANU wa 1971 ulijielekeza kwenye mapambano dhidi ya Ukoloni, Ukoloni-Mamboleo na Ubeberu ili kufanikisha Ukombozi wa Afrika na wa Mwafrika na kuweka mkakati wa ulinzi na usalama wa umma ili nchi iwe na uwezo wa kukabiliana na uvamizi wowote kutoka kwa ubeberu au na vibaraka vyake, Mwongozo wa 1981 umejikita katika kufanya uchambuzi kosoa wa kina na mpana juu ya hali ya kisiasa na kiuchumi iliyokuwepo nchini, hali ya maendeleo ya demokrasia nchini na ndani ya chama, n.k., na kutoa mapendekezo ya kuimarisha na kupanua demokrasia katika Chama na nchi”. Mwisho wa kunukuu. Inashangaza kuwa wana CCM wanaotawala sasa wanatafsiri ukosoaji kuwa ni uadui na kwenda kinyume kabisa na misingi ya Chama chao.

Kwa upande wa Chama ambacho mimi ni Kiongozi wake, Msingi wa kwanza Katika misingi kumi ni UZALENDO. Msingi huu unasema, nanukuu “ Uzalendo ndio moyo wa kuanzishwa kwa chama cha Wazalendo ikiwa ni tamko letu rasmi la kuipenda nchi yetu na utayari wa kuipigania na kuilinda. Ubora na umakini wa maamuzi yetu kama chama utapimwa kwa kuangalia ni namna gani maamuzi hayo yana faida kwa taifa letu na wananchi wake kwa leo na kesho”. Hivi sisi ACT Wazalendo kama Chama hufanya ukosoaji kwa kuzingatia maslahi ya Nchi yetu. Kila jambo tunalipima kwa kuangalia nchi inapata faida gani. Tulipoamua kukosoa takwimu za Serikali kuhusu GDP ( Pato la Taifa ) tulijua iwapo Serikali itaendelea na sera fyongo za Uchumi, Wananchi wataumia na nchi itaumia. Tangu tumetoa Tamko lile la Kamati Kuu Serikali imelegeza udhibiti wa ujazo wa Fedha kwenye Uchumi na ukuaji wake umefikia 8% kwa mujibu wa Taarifa za hivi karibuni za Benki Kuu.

Tulipoamua kuzungumzia soko la bidhaa za mbaazi, choroko nk sio kuwa tunainanga Serikali bali tunataka Serikali itimize wajibu wake Kwa raia kufuatia kuanguka kwa soko la mbaazi lenye thamani ya $250m ( zaidi TZS 500 Bilioni) kwa mwaka.

Tulipoamua kuchambua Taarifa ya CAG ya mwaka 2016/17 na uchambuzi uliofutia wa majibu ya Serikali kwa Hoja hiyo ya Ukaguzi lengo letu ni kuisimamia Serikali ambayo ndio wajibu wa Wabunge na Vyama vya siasa visivyo madarakani. Hatukutumwa bali tulijituma na kujiongeza kuonyesha kuwa Fedha za Umma hazisimamiwi vizuri na Serikali ya awamu ya 5 iliyo chini ya CCM.

Wakosoaji wa Serikali wanatimiza wajibu wao kama Wananchi. Hawatumwi na mabeberu. Kwa mujibu wa Sheria za nchi yetu kutumwa na mabeberu kuchafua sura ya nchi ni uasi na adhabu yake ni kifo. Serikali badala ya kulalamika tu kwenye mikutano Kuwa wakosoaji wake wanatumwa, ichukue hatua za kisheria kuwashtaki hao wanaodhaniwa kutumwa ili wakosoaji wa kweli waendelee na wajibu wao. Tuhuma za kutumwa hakiwezi kuwa kichaka cha kujifichia na kukwepa kujibu Hoja za Msingi.

Wananchi sasa waanze kukataa nadharia za kitoto, zilizopitwa na wakati Kuwa wakosoaji wa Serikali wametumwa. Wananchi wahoji ushahidi wa madai hayo. Wasikubali tuhuma hewa zinazotolewa ili kuficha ukweli wa masuala yanayoibuliwa. Serikali ina Vyombo vyenye uwezo mkubwa wa kuchunguza, Wananchi watake ushahidi kutoka vyombo Hivi. Propaganda za ‘ wanatumiwa ‘ zikiachwa tu watu wataumia. Tutajenga Taifa la hovyo, la watu wasiohoji, wanaodanganywa tu.

Kwa mwananchi, hakuna uzalendo bora zaidi kuliko uzalendo wa kuikosoa Serikali ya nchi yako. Uzalendo mkubwa zaidi ni kuitetea nchi yako, si Serikali! NCHI yako.
Nakubaliana na wewe Zitto 100% kwamba ni wajibu wa serikali kutoa ushahidi kuhusu hao inaowaita kuwa wametumwa,ingawa si rahisi.Nakubaliana na wewe pia kwamba dhana ya kutumwa inaweza kuwa kichaka cha serikali kujifichia kuhusu masuala kadhaa ya msingi.Hata hivyo nadhani hatuna budi kukubaliana pia kwamba dhana ya kutumwa ina mashiko,ingawa si katika kila jambo.Nadhani Zitto unajua kwamba nchi nyingi duniani zimeingia katika matatizo makubwa kupitia kwa makuadi wa mafisadi wa mabeberu waliotumwa na mifano iko mingi. Naamini mifano hii unaijua Zitto.

Hata hivyo nikiri kwamba si rahisi sana ku-substantiate jambo hili(la kutumwa) with concrete proof and evidence and hence the use of circumstantial evidence.Zitto wanaofanya upuuzi huu wanajua kwamba si rahisi kutoa ushahidi dhidi yao na ndio maana wanakuwa na ujasiri wa kufanya upuuzi huo.Haya yote unayajua Zitto.Let us swim together Zitto,makuadi wa mafisadi ni real ingawa sio in all situations na hata Baba wa Taifa Mwl.Nyerere alilizungumzia sana hili.

Sikatai kwamba serikali ya awamu ya tano ina makosa,yapo,lakini tuishauri kwa kutumia hekima na busara zote, huku tukiweka mbele maslahi mapana ya taifa letu.Tanzania ni yetu sote.Tuki-raise jazba za Watanzania mambo yakivurugika tutakimbilia wapi,let's be careful.Sisi wote ni wanadamu, hakuna aliyemkamilifu.
 
Wakosoaji wa Serikali wanatumwa?

Siku hizi ukisikiliza hotuba za Viongozi Wakuu wa Serikali ya Tanzania pamoja na maandiko ya Vyombo vya Habari vinavyoiunga mkono Serikali kama vile Jamvi la Habari, Habarileo, Uhuru nk utasikia au kusoma madai yanayojirudia rudia kuwa kuna Watanzania wanatumika na mataifa ya Nje kuidhuru nchi yetu. Madai haya yanayotolewa bila ushahidi wowote ni madai yanayoonyesha ni namna gani nchi yetu imeua kabisa utamaduni wa kukosoana.

Wakati wa mjadala wa mabadiliko makubwa ya sekta ya Madini aliyoyafanya Rais Magufuli kufuatia amri yake ya kuzuia kusafirisha makanikia, tuhuma dhidi ya baadhi yetu zilikuwa kubwa mno kiasi cha watu kuonekana wasaliti wa nchi yetu. Katika moja ya hotuba yake, Rais Magufuli alifikia hatua ya kusema kuwa ‘ msaliti dawa yake inajulikana ‘.

Haikuchukua muda Mbunge Tundu Lissu, aliyekuwa mmoja wa wakosoaji wakubwa wa Serikali alipigwa risasi na kukoswakoswa kupoteza maisha. Licha ya matusi yote tuliyotukanwa, madai ya $490bn ambayo Serikali iliyatoa kwa Kampuni ya Barrick yalishuka mpaka $300m ambazo hazijalipwa mpaka sasa na wala hazionekani kwenye vitabu vya Serikali kama Mapato tarajiwa ( receivables). Vijana wanatania mitandaoni kuwa tumetoka ahadi ya Noah kwa kila Mtanzania na kufikia ahadi ya Balimi 7 kwa kila Mtanzania. Hata hizo Balimi hazijapatikana.

Wakati wa mjadala wa Ndege yetu kukamatwa huko Canada, pia zilitengenezwa nadharia kuwa mimi na Tundu Lissu tumelipwa na mabeberu ili kuzuia ndege ile. Kampuni iliyowasilisha amri ya kushikilia ndege ile ililipuliwa na bomu na nchi kuingizwa kwenye taharuki bila sababu. Hatimaye Serikali imelipa zaidi TZS 60 Bilioni ili Ndege iweze kuletwa nchini. Wakosoaji wa Serikali walikosoa namna Serikali inajiendesha kana kwamba Tanzania ni kisiwa na madhara yake ni nchi kupata hasara kubwa Sana. Hivi sasa kuna kesi kadhaa Marekani na Uingereza dhidi ya Serikali yetu kutokana na mikataba mbalimbali ambayo Serikali imeshindwa kuiheshimu au Serikali ilifanya ubabe kuivunja bila kujali sheria za kimataifa. Jumla ya madai tunayodaiwa kwenye mahakama za nje ( ninayoyajua mimi na mengine kuthibitishwa na CAG kwenye Taarifa yake ya mwaka 2016/17 ) yanafika Dola za Kimarekani Bilioni 1.48 Sawa na Shilingi Trilioni 3.3 za Kitanzania [ Madai ya Standard Chartered Bank Hong Kong $614m+$148m, Madai ya Syimbion Power $600m, Madai ya Konoike $63m, Madai ya Airbus $59m ].

Hata sasa kwenye mjadala wa kutoonekana kwa matumizi ya TZS 1.5T Serikali imejaribu kutumia maneno hayo hayo ya kuwaita wakosoaji kuwa wametumwa. Majibu rasmi ya Serikali ndani ya Bunge yamewaita wakosoaji ‘ watu wasioitakia mema nchi yetu ‘. Rais naye alipokuwa anafungua tawi la Benki ya NMB Dodoma akasema ‘ watu wanatumwa na mabeberu ‘. Unachoshangaa ni Kwamba hoja hii ya 1.5T imetoka kwenye Ripoti ya CAG ambayo ndio mamlaka ya kikatiba kufanya Ukaguzi wa Fedha za Serikali. CAG ana mamlaka makubwa kiasi kwamba Rais hana mamlaka ya kumfukuza Kazi hata amchukie namna gani. Iweje utumie Ripoti ya CAG kuihoji Serikali uwe unatumwa na watu wa Nje?

Kwenye mjadala kuhusu zabuni ya pasi za kusafiria pia Gazeti la Jamhuri lilisakamwa na Gazeti la Jamvi kuwa wametumwa na mabeberu. Baadaye naona magazeti haya yalifanya mkataba wa amani ( ceasefire). Hata hivyo gazeti la Jamhuri lilikuwa linafanya Kazi yake ya kuhoji Serikali na kupasha Habari wasomaji wake.

Wakosoaji wa Serikali wanapohoji ni Kwa maslahi ya nchi na sio kwa kutumwa. Dhana kwamba watu wanatumwa ni dhana ambayo haina nguvu na inajaribu kuua Uhuru wa maoni na wajibu wa kukosoa. Kukimbilia kuita watu majina mabaya Kwa sababu ya kuhoji masuala ya Umma tena kwa ushahidi ni dalili za wenye mamlaka kukosa Majibu na hivyo kutumia nguvu dhidi ya wakosoaji. Nadharia kuwa ukosoaji ni kutumwa unaenda kinyume na Mwongozo wa CCM wa mwaka 1981 ambao ulijikita kwenye ‘ kukosoa na kujikosoa ‘ ili kujenga Taifa imara.

Marehemu Mzee Kingunge Ngombale Mwiru amenukuliwa na wanazuoni akieleza kuhusu Mwongozo wa CCM wa mwaka 1981 “ Wakati Mwongozo wa TANU wa 1971 ulijielekeza kwenye mapambano dhidi ya Ukoloni, Ukoloni-Mamboleo na Ubeberu ili kufanikisha Ukombozi wa Afrika na wa Mwafrika na kuweka mkakati wa ulinzi na usalama wa umma ili nchi iwe na uwezo wa kukabiliana na uvamizi wowote kutoka kwa ubeberu au na vibaraka vyake, Mwongozo wa 1981 umejikita katika kufanya uchambuzi kosoa wa kina na mpana juu ya hali ya kisiasa na kiuchumi iliyokuwepo nchini, hali ya maendeleo ya demokrasia nchini na ndani ya chama, n.k., na kutoa mapendekezo ya kuimarisha na kupanua demokrasia katika Chama na nchi”. Mwisho wa kunukuu. Inashangaza kuwa wana CCM wanaotawala sasa wanatafsiri ukosoaji kuwa ni uadui na kwenda kinyume kabisa na misingi ya Chama chao.

Kwa upande wa Chama ambacho mimi ni Kiongozi wake, Msingi wa kwanza Katika misingi kumi ni UZALENDO. Msingi huu unasema, nanukuu “ Uzalendo ndio moyo wa kuanzishwa kwa chama cha Wazalendo ikiwa ni tamko letu rasmi la kuipenda nchi yetu na utayari wa kuipigania na kuilinda. Ubora na umakini wa maamuzi yetu kama chama utapimwa kwa kuangalia ni namna gani maamuzi hayo yana faida kwa taifa letu na wananchi wake kwa leo na kesho”. Hivi sisi ACT Wazalendo kama Chama hufanya ukosoaji kwa kuzingatia maslahi ya Nchi yetu. Kila jambo tunalipima kwa kuangalia nchi inapata faida gani. Tulipoamua kukosoa takwimu za Serikali kuhusu GDP ( Pato la Taifa ) tulijua iwapo Serikali itaendelea na sera fyongo za Uchumi, Wananchi wataumia na nchi itaumia. Tangu tumetoa Tamko lile la Kamati Kuu Serikali imelegeza udhibiti wa ujazo wa Fedha kwenye Uchumi na ukuaji wake umefikia 8% kwa mujibu wa Taarifa za hivi karibuni za Benki Kuu.

Tulipoamua kuzungumzia soko la bidhaa za mbaazi, choroko nk sio kuwa tunainanga Serikali bali tunataka Serikali itimize wajibu wake Kwa raia kufuatia kuanguka kwa soko la mbaazi lenye thamani ya $250m ( zaidi TZS 500 Bilioni) kwa mwaka.

Tulipoamua kuchambua Taarifa ya CAG ya mwaka 2016/17 na uchambuzi uliofutia wa majibu ya Serikali kwa Hoja hiyo ya Ukaguzi lengo letu ni kuisimamia Serikali ambayo ndio wajibu wa Wabunge na Vyama vya siasa visivyo madarakani. Hatukutumwa bali tulijituma na kujiongeza kuonyesha kuwa Fedha za Umma hazisimamiwi vizuri na Serikali ya awamu ya 5 iliyo chini ya CCM.

Wakosoaji wa Serikali wanatimiza wajibu wao kama Wananchi. Hawatumwi na mabeberu. Kwa mujibu wa Sheria za nchi yetu kutumwa na mabeberu kuchafua sura ya nchi ni uasi na adhabu yake ni kifo. Serikali badala ya kulalamika tu kwenye mikutano Kuwa wakosoaji wake wanatumwa, ichukue hatua za kisheria kuwashtaki hao wanaodhaniwa kutumwa ili wakosoaji wa kweli waendelee na wajibu wao. Tuhuma za kutumwa hakiwezi kuwa kichaka cha kujifichia na kukwepa kujibu Hoja za Msingi.

Wananchi sasa waanze kukataa nadharia za kitoto, zilizopitwa na wakati Kuwa wakosoaji wa Serikali wametumwa. Wananchi wahoji ushahidi wa madai hayo. Wasikubali tuhuma hewa zinazotolewa ili kuficha ukweli wa masuala yanayoibuliwa. Serikali ina Vyombo vyenye uwezo mkubwa wa kuchunguza, Wananchi watake ushahidi kutoka vyombo Hivi. Propaganda za ‘ wanatumiwa ‘ zikiachwa tu watu wataumia. Tutajenga Taifa la hovyo, la watu wasiohoji, wanaodanganywa tu.

Kwa mwananchi, hakuna uzalendo bora zaidi kuliko uzalendo wa kuikosoa Serikali ya nchi yako. Uzalendo mkubwa zaidi ni kuitetea nchi yako, si Serikali! NCHI yako.
Chama Cha wazalendo 2025
 
Back
Top Bottom