Wakosoaji wa Serikali wanatumwa?

Wakosoaji wa Serikali wanatumwa?

Wakosoaji msiotaka kukosoa ubadhirifu katika halmashauri ya kigoma ujiji kwa nini msionekana mnatumika?
 
H. Polepole alishakwambia 2020 katafute kazi ya kufanya, labda Ridhwani Kikwete au Mangi Kimambi watakupa kazi lkn Bunge letu sahau, haurudi!

2025-2025 say no Mafisadi, no Usaliti!

Zito Kabwe, Tundu Lisu &Co. Out!
Pole sana naona dawa imeingia.
 
Ikumbukwe kuwa wakosoaji wa serikali hawajaanza leo bali wamekuwepo siku zote.

Mimi naona dhana ya kuwa wakosoaji wa serikali wanatumwa na maadui au washindani wetu hazina mashiko. Hata ukisoma kwa umakini hivyo vyanzo mbalimbali utagundua tu kuwa habari hizi zipo ki-propaganda zaidi kwa manufaa ya chama kinachoongoza.
 
Ukiona mtu kila siku yeye ni kukosoa tu ujue huyo ni adui wa maendeleo.

Wapinzani wanatakiwa kuwa washirika wa maendeleo sio maadui. Hawatakiwa kukosoa tu kila kitu. Wanatakiwa kukosoa kwa malengo ya kuboresha.
maana ya mkosoaji ni nini? wanalitumia vyema hili jina sivyo?
 
nchi
Niko hapa kusimamia ukweli tu kwa manufaa ya wanyonge...vibaraka wa wazungu wametumia suasa kutuharibia nchi kwa muda mrefu sana
inaharibiwa na wanaowapa tenda na kuwafukuza huku wanajua wakifanya hivyo nini kinatokea, wanawachagua wasio weza kazi ili wachote mabilioni then wakivurunda wanawafukuza, ngoja tuone vitambulisho vya taifa na e passport
 
Hii ni propaganda kama ile ya mahakama ya mafisadi cha ajabu hakuna kesi hata moja.
 
Kinachoendelea Tanzania, kuna adui kapanga kutuangamiza na wanaoangamizwa hawana taarifa. Kitajachofata kitakuwa ni uchokozi feki ili apate sababu ya kututeka.
 
. Wanatakiwa kukosoa kwa malengo ya kuboresha.

Toka lini CCM wakawa wasikivu? Siku zote tunaokosoa lengo ni kuboresha. Tulikosoa sera ya ubinafsishaji chini ya Mkapa. Tukakosoa mikataba ya madini chni ya Mkapa na Kikwete. Tutakosoa deals za Meremeta, Kiwira, EPA, Escrow, IPTL, Richmond a.k.a Dowans a.k.a Symbion. Tunakosoa Katiba inayomfanya Rais mungu-mtu. Tunakosoa CAG kuzuiwa kisheria kukagua sekta ya madini. Tunakosoa 1.5T kutojulikana zilipo.

Tunachopata ni kuitwa wasaliti, tunatumiwa na 'mabeberu' n.k. Sasa chifu, unataka tukosoeje?
 
Ukiona mtu kila siku yeye ni kukosoa tu ujue huyo ni adui wa maendeleo.

Wapinzani wanatakiwa kuwa washirika wa maendeleo sio maadui. Hawatakiwa kukosoa tu kila kitu. Wanatakiwa kukosoa kwa malengo ya kuboresha.
Pia ukiona mtu anashangilia kila akifanyacho magu kama wale lumumbabuku7, huyo ni adui zaidi wa maendeleo!
 
Hebu tupe maana ya opposition kwa kiswahili
 
Ni sinema ya kitoto kuwaita wakosowaji wa serekali kuwa vibaraka
 
Kwanini kama raia anataka tukopi nchi ya China tusikopi Kila kitu?
 
Baada ya kutawaliwa kifisadi na serikali za ccm zilizopita watanzania wamewakataa ccm kwenye uchaguzi wa 2015....walichofanya ili kuwahadaa wananchi watawala wa sasa wamekuja Na janja ya kujifanya wazalendo...huku nyuma ya pazia wakitupiga kifisadi kimajanga....

Na wanafanya hivi kwa kuminya aina yoyote inayofichua maovu yao...iwe kwa kulizima bunge live...au kuwakamata wapinzani au kuwapiga Na hata kuwaua waandishi wa habari...na ku control mitandao.....namna nyingine wanayotumia ni hii ya kuita wakosoaji wao kuwa wasaliti ama wametumwa Na mabepari..

...aliye bepari Na mnyonyaji Mkuu wa RAIA wa tz ni watawala....Hawa ndio wanawakamua rsaia hela yao ya kodi Na kuifuja hovyo...,Na wanapoulizwa wananasema eti wa wanaohoji ni wasaliti....shame on them...wakoloni weusi....
 
Malaika hapendi kukosolewa na ukimkosoa adhabu yake kutumiwa watu wasiojulikana.

Ngoja niendelee kukazia kauli yako ''Tumekabidhi nchi kwa washamba na malimbukeni-ZZK"
Kauli zingine zinapotray weak reasoning ya watz..hivi hadi washamba wachukue nchi wanaojiita wajanja walikuwa wapi, km ulilala hali ikawa hivyo unalalama nini sasa?? na hao wajanja waliokuwepo kabla walileta nini kwa nchi kama cyo kujenga spirit ya uvivu, wizi na short cuts nyingi za uhalifu..kasome historia ya nchi yetu kabla ya uhuru, itakusaidia wapi walikuwa na viongozi hodari na shupavu kulinda watu wao, uongozi sio ujanja kijana na siyo lazima kufanya watu wafurahi!
 
Kauli zingine zinapotray weak reasoning ya watz..hivi hadi washamba wachukue nchi wanaojiita wajanja walikuwa wapi, km ulilala hali ikawa hivyo unalalama nini sasa?? na hao wajanja waliokuwepo kabla walileta nini kwa nchi kama cyo kujenga spirit ya uvivu, wizi na short cuts nyingi za uhalifu..kasome historia ya nchi yetu kabla ya uhuru, itakusaidia wapi walikuwa na viongozi hodari na shupavu kulinda watu wao, uongozi sio ujanja kijana na siyo lazima kufanya watu wafurahi!
Unapoishangaa Iringa kutomchagua Dr Mahiga,wengine tunashangaa CCM kumuacha Mahiga kwenye Urais
Pitia hapo waweza kupata mawili matatu
 
Back
Top Bottom