Wakoloni walioitawala Tanganyika walikuwa na "roho" nzuri kuwazidi watawala wa sasa wa Tanganyika?

Vitu wanavyo fanya ccm na serikali yao leo hii na kujisifia kwamba ni maendeleo vilipaswa kufanyika miaka 30 nyuma huko lakini walivyo kua na akili fupi kama njia ya kwenda chooni baada ya miaka 60+ ya uhuru kwenye Karne ya sayansi na teknolojia ndio wanatamba kabisa kwa kujenga zahanati, madarasa na matundu ya vyoo bado umeme ni shida ufisadi Kila pahala kwa kifupi wale maadui watatu wa taifa wameongezeka wamekua wanne umaskini, ujinga, maradhi na ccm

Nina uhakika kabisa kama mkoloni angekuepo kusingekua na mgao wa umeme na shida maji bila kusahau ufisadi ambao ni tabia ya asili kabisa ya viongozi wa ccm kama ilivyo sasa hivi, Tanganyika ilitakiwa kua chini ya utawala wa mkoloni angalau hadi mwaka 2000 kuna hatua kubwa kimaendeleo tungekua tumeipiga
 
Mzee Nyerere ana mazuri yake ,lakini ameacha katiba mbaya mbaya kwa hili nampa laana
Kwanini usjilaani wewe ambaye huchukui hatua yoyote kuibadili katiba ila unamlaumu marehemu aliyeondoka madarakani miaka 39 iliyopita na kufariki miaka 25 iliyopita?
Kwanini usimlaumu hata mzee wa msoga ambaye alitumia mamilioni kututengenezea katiba halafu akaikataa?
 
Huko mbinguni ndio wapi ndugu? Maana sie wengine wageni humu
mbinguni ni makao ya watu ambako wataishi baada ya kufa kwa kuwa wameyafanya mapenzi ya Mungu duniani, kisha kustahili kukaa na Mungu katika raha ya milele. Yaani watu wanaupokea uzima wa milele.

JESUS IS LORD&SAVOR
 

GoldDhahabu Uko sahihi Mkuu bora Mkoloni kuliko Utawala huu tulonao.​

Sio tu Serikalini bali hata kwenye Taasisi na NGO's mbalimbali sijui sisi Watanzania tuna shida gani.​

Ndugu yangu mmoja anafanya kazi kwenye Kampuni moja kubwa sana ya Uchimbaji madini hapa Tanzania anasema toka Wazungu waondoke kwa wingi na nafasi zao kuchukuliwa na Watanzania hali imekuwa si hali kwa wafanyakazi wengi kwani rushwa, ukabila na uonevu vimeshika hatamu. Inabidi tutafakari na kuchukua hatua kabla Taifa halijazama kabisa.
 
Mzee Nyerere ana mazuri yake ,lakini ameacha katiba mbaya mbaya kwa hili nampa laana
Nyerere kaondoka zaidi ya miaka 25 sasa, tuliobaki tunashindwa nini kujitengenezea katiba nzuri itakayolinda haki na usalama wa kila mtu, tuangalie mbele, kwa sasa mchawi mkubwa ni CCM ndio inaturudisha nyuma na kutuongezea umaskini kila siku
 
Mzee Nyerere ana mazuri yake ,lakini ameacha katiba mbaya mbaya kwa hili nampa laana

Hii katiba ilitengenezwa kwa mahitaji ya muda ule, he was right. Lakini kwa mahitaji ya nyakati hizi tunahitaji mabadiliko makubwa na katiba mpya itakayo kidhi mahitaji ya sasa

Sasa jukumu la kubadili ni la viongoz waliokuja baada yake
 
Back
Top Bottom