Quinton Canosa
JF-Expert Member
- Nov 2, 2012
- 1,224
- 1,258
Habari zenu wanajamii forum,
Leo ngoja niongee na kina dada na tabia zao za ubahili.
Yaani utakuta hata mpenzi wako anakuwa mgumu kukusaidia inapotoke shida fulani lakini wao ni wepesi sana kuomba kusaidiwa sijui hizo hela zenu mnapeleka wapi jamani.
Hii nimeishuhudia hata kwa kaka yangu mke wake ni mgumu sana inapofika mumewe kaishiwa.
Hata utakuta msichana mnapendana sana ila suala la kutoa ni wagumu hawa viumbe aisee yaani yupo radhi akuachie ulipie kodi nyumba,ulipie watoto ada na mahitaji mengine yeye anauchunaa mpaka ukute mmekabwa sana ndio utaona anajitoa tena kiubahili.
Labda niwaulize hela zenu wakina dada huwa mnazipeleka wapi hata kusema baba ni kichwa cha familia muda mwingine jamani wanaume tunachoka sana tuwe tunasaidiana jamani sometimes.
Ni hayo tu, nawasilisha