lazima ukae
JF-Expert Member
- May 15, 2013
- 791
- 417
Habari wana great thinkers,kuna katabia au tabia ambayo wanayo wakina dada wa humu jf ambayo sio nzuri na inaweza ikawafikisha pabaya.Siku kama tano zilizopita nilipost thread ya kutafuta mchumba na Mungu si athuman akatokea dada mmoja akani PM namba yake na tukapata kufahamiana kiasi flani.Tatizo linakuja pale ambapo kila nikipiga nae story analazimisha kujua kazi yangu na nalipwa kiasi gani kwa mwezi,alinichosha zaidi pale aliponiuliza kama nina gari au la..apo nilichoka kabisa na kukosa hamu hata ya kuzungumza nae...Je hii ni sahihi kwa wanavyotufanyia hawa dada zetu?